Gesi Asilia(CNG) Gari inatembea Km 290 kwa Tsh. 30,000 tu

protogonist

Senior Member
Feb 27, 2018
179
226
Nimekutana nayo mahali nimeona nishee (Copy&Paste),

Makadirio ya chini ya umbali kwa cc 1400s hadi 1500s

GAS KILO 1 NI SHILINGI 1590

Kg 15 inatembea km 230
Kg 11 unatembea km 180
Kg 9 inatembea km 120
Huu umbali unatofautiana kulingana na cc za engine yako.

Ukifunga gas kwenye gari haimaanishi mfumo wa zamani wa mafuta unaondoka hapana!! Ila unakuwepo na ukiamua kuswitch unaswitch mwenyewe kwamba sasa nataka kutumia mafuta au sasa nataka kutumia gas.

Sisi tuna-iset gari iji switch automatically kwenda kwenye gas ikifika r.p.m ya 500. Tunafunga gas kwenye magari ya petroli kwa mkoa wa dar es Salaam TU kwa utaalamu wa hali ya juu unaofanywa na wahandisi wa magari wa NIT na kuifanya gari yako kutembea bila gharama kubwa za mafuta.

Pia ukifunga gas kwenye gari yako utaifanya engine yako kuishi maisha marefu zaidi kwa kuwa gas ni clean zaidi ya mafuta hivo inachomwa vizuri na inasaidia kutunza mazingira kwa sababu inafanya complete combustion.

WARRANTY MIEZI 6

“Kanuni mpya ndani ya sheria ya Mazingira inamtaka mwekezaji mpya wa kisima cha mafuta kuhakikisha anaweka miundombinu ya gesi asilia yani CNG Vinginevyo hatopatiwa leseni” hayo yamesemwa na Waziri wa muungano na Mazingira. Selemani Jaffo

Bei (gharama) za ufungaji
A;
~ Milioni 2.5 kwa mtungi wa kilo 15
~ Milioni 1.9 Kwa mtungi wa kilo 11
~ Milioni 1.8 kwa mtungi wa kilo 9

B;
Pia kuna kufunga kwa mkopo wa Maendeleo Bank ambapo wao wanakulipia kila kitu na gharama zote na mteja anatakiwa kupeleka Tsh. elfu 50 kila week hadi anamaliza deni lake.

Kumbuka, hii system ukifunga inakuwa ni ya kwako hivo ukiuza gari unaweza ukaitoa na kufunga kwenye gari lingine utakalo nunua.

Location: Tunapatikana NIT Mabibo
Namba: 0683477676
WhatsApp: 0683477676
 
Km 290 hapo ni kwamba Moro to Dom km 265 hapo zinabaki km 25 za ziada kupiga misele viunga vya Dodoma kwa tsh 30,000

Au gesi ya tsh 60,000 nitakuwa na km 580. kutoka Dar to Dom ni km 450 so hapo maana yake nafika Dodoma na chenji ya km 130 inabaki ya kupiga misele dodoma na viunga vyake kwa cost ya tshs 60,000.

Inawezekana sijui lakini,May beee
 
GAS KILO 1 NI SHILINGI 1590
emoji95.png
emoji95.png

Kg 15 inatembea km 230
Kg 11 unatembea km 180
Kg 9 inatembea km 120
Huu umbali unatofautiana kulingana na cc za engine yako.
... tunafanyiana timing wengi wakishahamia huko Serikali itapandisha kodi na tozo ghafla bei itakuwa sawa na mafuta tu kwa kisingizio cha kujenga madarasa, huduma za mama na mtoto, na matundu ya vyoo!
 
Huaga mnasema faida tu je hasara zake Ni zipi
hasara zake ni kwamba ukipata ajali,kwa mgongano mkubwa kuna uwezekano huo mtungi wa gas ukawa bomu moja matata sana na tukaja kuzoa majivu tu.

huwa na najiuliza mnafunga hiyo mitungi ya gas kwa ajili tu ya kupunguza gharama au mmetazama na usalama wa mtu anayetumia hayo magari?
maana haiingii akilini gari limetengenezwa liende kwa mafuta,wewe unaweka mfumo wa gas tu,vipi mtikisiko wa gas hauwezi kuleta shida?,je mmefanya tafiti za kutosha?,

nauliza kuhusu usalama sio gharama.
 
Hii gas ni baridi mno hailipuki na pia kama kulipuka ungeanza kuhofia petrol maana ndio hatari zaidi hasa pale tank linapopasuka...
 
kitu kulipuka haijalishi ubaridi wake,pia tank na njia za kupeleka mafuta (liquid) kwenye injini na zile za gas zitakua tofauti,shida ni kwamba gari halikuandaliwa kupark huo mtundi wa gas,sasa pale wanapouweka huwa ni salama kwa watumiaji?,
 
Unafikiri Chuo cha Usafirishaji Tanzania(NIT) Na wahandisi wake wote na Mamlaka husika zote hazijafanya uchunguzi kuhusu usalama wa mtumiaji? na juzi Waziri Jaffo kupitia Azam media ametoa tamko na sheria zimetungwa kuhusu CNG huduma inatolewa na wahandisi wa NIT na inatolewa pale chuoni NIT, kwa mujibu wa hiyo thread. Watanzania Tupunguze Ujuaji
 
mkuu mimi sina taarifa,nimeuliza hapo nijulishe kama hayo yamefanyika na yamefanyikaje,sio hayo mambo unayonijibu sijui waziri kasemaje haihusiani na usalama naouliza hapa.

Wewe umepigia chapuo bei,mimi nimehoji usalama wake,nijibu kitaalamu kuwa tumefanya hivi na vile kwahiyo usalama nibhakika 100%.
Naamini wewe ni mhusika wa uwekaji wa mitungi hii kwenye gari,je unazingatia nini kuhakikisha usalama pale inapotokea ajali?,

Swali langu la kwanza ulijibu eti gas ni ya baridi🤔🤔🤔🤔 haiwezi kulipuka,kweli umejibu kihandisi kwa hoja hizo?,

Hem usifanye nikaona naongea na dalali hapa sio mtaalam wa fani husika.
 
Unafikiri Chuo cha Usafirishaji Tanzania(NIT) Na wahandisi wake wote na Mamlaka husika zote hazijafanya uchunguzi kuhusu usalama wa mtumiaji? na juzi Waziri Jaffo kupitia Azam media ametoa tamko na sheria zimetungwa kuhusu CNG huduma inatolewa na wahandisi wa NIT na inatolewa pale chuoni NIT, kwa mujibu wa hiyo thread. Watanzania Tupunguze Ujuaji
Jaffo ni engineer?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
mkuu mimi sina taarifa,nimeuliza hapo nijulishe kama hayo yamefanyika na yamefanyikaje,sio hayo mambo unayonijibu sijui waziri kasemaje haihusiani na usalama naouliza hapa.

Wewe umepigia chapuo bei,mimi nimehoji usalama wake,nijibu kitaalamu kuwa tumefanya hivi na vile kwahiyo usalama nibhakika 100%.
Naamini wewe ni mhusika wa uwekaji wa mitungi hii kwenye gari,je unazingatia nini kuhakikisha usalama pale inapotokea ajali?,

Swali langu la kwanza ulijibu eti gas ni ya baridi haiwezi kulipuka,kweli umejibu kihandisi kwa hoja hizo?,

Hem usifanye nikaona naongea na dalali hapa sio mtaalam wa fani husika.
Mkuu mm ni mtumiaji tu sina elimu yoyote na uinjinia mm ni mkulima nimefunga kamtungi kangu naenjoy sasa kama una maswali zaidi fanya kuwapigia nimefanya kushare tu....sharing is caring
 
mkuu mimi sina taarifa,nimeuliza hapo nijulishe kama hayo yamefanyika na yamefanyikaje,sio hayo mambo unayonijibu sijui waziri kasemaje haihusiani na usalama naouliza hapa.

Wewe umepigia chapuo bei,mimi nimehoji usalama wake,nijibu kitaalamu kuwa tumefanya hivi na vile kwahiyo usalama nibhakika 100%.
Naamini wewe ni mhusika wa uwekaji wa mitungi hii kwenye gari,je unazingatia nini kuhakikisha usalama pale inapotokea ajali?,

Swali langu la kwanza ulijibu eti gas ni ya baridi haiwezi kulipuka,kweli umejibu kihandisi kwa hoja hizo?,

Hem usifanye nikaona naongea na dalali hapa sio mtaalam wa fani husika.
Mwanzo kabisa wa uzi nimeandika kuwa nimecopy na kupaste...
 
Back
Top Bottom