Nani ameiua hotel ya kifahari ya Ngurdoto Mountain Lodge-Arusha kiasi cha kubaki magofu?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Hii Hoteli ilikuwa Maarufu sana awamu ya 4 Kwa kufanyika Kwa Biashara ya mikutano,seminar na kutumiwa na Watalii Matajiri na Marais mbalimbali Kwa kushirikiana na AICC.(Almaarufu Hoteli ya Semina elekezi).

Lakini tokea hapo hakuna kinachoendelea na inasemekana imebakia Magofu Kwa mujibu wa Muongoza Watalii aliyehojiwa na Clouds.

Aidha ningependa kufahamu mmiliki wa Hoteli,Je ni Serikali au mtu binafsi? Na kama ni Serikali Kuna tatizo gani Hadi ife? Kwa nini isikodishwe Kwa wawekezaji ikizingatiwa Kuna kumiminika.kwa Watalii awamu hii ya 6?

Mwisho,ni nani au nini kimepelekea Hoteli hii ya Kifahari kufa kifo Cha Mende?

View: https://www.instagram.com/p/CxMs9vas0Sz/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

Pia som hapa 👇
 
Inategemea fedha ya kujengea ilipatikanaje, kama ilikuwa haramu basi hayo ndiyo malipo kwa mwenye nayo
 
Mmiilki jina kitu kama mrema alishakufa mwaka juzi.

Na biashara za kiAfrika, nguvu ya menejimenti huwa ni mmiliki mwenyewe.

Akishakufa na miradi yake inafuata!
Asante kwa taarifa hii

Wazazi Watanzania ambao wamefanikiwa ni waoga sana kuwatumia watoto wao kuendeleza miradi yao ya kibiashara iliyofanya wafanikiwe tofauti na wenzetu wenye asili ya Asia (Waarabu na Wahindi)

Nikupe mfano utakuta baba alikuwa mkulima mzuri sana, mkubwa na mwenye mafanikio hata watoto wake kawasomesha kupitia hiko kilimo

Cha ajabu akiwasomesha watoto wake haukuti anawasomesha waje waendeleze biashara hiyo ya familia waje na idea mpya. Watoto watasoma waje kuajiriwa, baba umri ukienda (uzee) au kifo na biashara ya kilimo inakufa

Leo hii MO au MeTL isingekuwa kampuni kubwa Afrika na Afrika Mashariki na kati ikiwa Mohammed Dewji angeamua kuajiriwa baada ya kutoka masomoni pale Georgetown University nchini Marekani.

Baada ya kumaliza masomo MO akarudi na idea za kisomi kuiendeleza kampuni ya baba yake, leo tunaiona MeTL iking'ara na yeye akiwa tajiri namba moja Afrika Mashariki na kati

The same ukifuatilia historia ya GSM, ASAS n.k hii ni mifano michache, ukitembelea familia za hawa wenzetu kuna vingi vya kujifunza

Watanzania tunakosa kujiamini sana kuendeleza biashara za kifamilia. Tunapenda sana kuajiriwa. Wenzetu wanatengeneza brands
 
Back
Top Bottom