Mahakama yaamuru baadhi ya mali za Ngurdoto Hoteli kupigwa mnada ili kulipa mishahara ya waliokuwa Wafanyakazi wa hoteli hiyo

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha masjala ndogo ya kazi imeamuru baadhi ya mali za Hotel ya Kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo eneo la mji mdogo wa Usariver Wilayani Arumeru Mkoani Arusha zikamatwe kwa ajili ya kupigwa mnada kufidia mishahara ya waliokuwa wafanyakazi 93 wa Hoteli hiyo wanadai kiasi cha Tsh. Milioni 129.

Naibu msajili wa Mahakama hiyo John Nkwabi alitoa maamuzi hayo jana katika mahakama Kuu kanda ya Arusha masjala ndogo ya Mkoa katika kesi ya msingi namba 140 ya mwaka 2020, ya madai ya waliokuwa wafanyakazi 93 dhidi ya mwajiri wao Hotel ya Ngurdoto Mountain Lodge.

Kesi hiyo iliyosajiliwa oktoba 16 Mwaka 2020 iliendeshwa katika hatua mbalimbali na kufidia tamati jana ambapo Msajili Nkwabi kwa kuzingatia sheria za kazi alitoa hukumu ya kukamatwa ili baadae zipigwe mnada kwa baadhi ya mali za Hoteli hiyo ili kupata kiasi cha shilingi 129,570,000 za kuwalipa madai ya mishahara ya wafanyakazi hao.

Nkwabi alitaja mali hizo kuwa ni vitanda 139, Gari aina ya Coaster bus lenye namba za usajili T847 DPH, kiwanja namba 418 kilichopo Block A eneo la Leganga, Usariver, Arusha na mashine nne za nguo za kufulia.

Msajili huyo alimuagiza dalali Allan Mollel wa kampuni ya udalali ya “First World Investment Auctioneers Debt” ya jijini Arusha kukamata mali hizo mara moja ili kusubiri amri ya mahakama tarehe 4.5.2021 kwaajili ya kuuzwa kufidia mishahara ya wafanyakazi.

Pamoja na mahakama waliondesha shauri hilo mahakamani ni Ofisa kazi mfawidhi wa Idara ya kazi Mkoa wa Arusha kwa niaba ya Kamishna wa kazi dhidi ya upande wa uatetezi wa wakili Edmund Ngemela.
 
Yule kijana angeacha tu dada yake aiendeshe kwa ushauri wa wataalam badala ya kujisimika kwa mfumo dume. ona sasa mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

Au wangeajiri wataalam kisha wao wakajiweka kando kusubiria mshiko kila mwisho wa mwezi.
 
Ngoja nichukue private jet Gulf stream yangu hapa nikiongozana na jopo la wanasheria na financial advisors wangu kuwahi huo mnada na fursa nyingine za kiuchumi nchini na uwekezaji.
 
Yule kijana angeacha tu dada yake aiendeshe kwa ushauri wa wataalam badala ya kujisimika kwa mfumo dume. ona sasa mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

Au wangeajiri wataalam kisha wao wakajiweka kando kusubiria mshiko kila mwisho wa mwezi.
Mkuu usidhani ni rahisi kihivyo jinsi unavyoeleza. Hii biashara ya hotel ilishaanza kuporomoka dikteta alipochukua nchi aliivurga sana na janga la corona ikaimaliza kabisa.

Kuna hoteli ina menejment nzuri kama kibo palace? Angalia ilivyo chali sasa hivi.
 
Unamuonea huyo unayemuita dikteta kwani yeye ndie aliyewashauri wategemee tenda za serikalini? biashara za ujanja ujanja sio nzuri mambo yakienda ndivyo sivyo
Mkuu usidhani ni rahisi kihivyo jinsi unavyoeleza. Hii biashara ya hotel ilishaanza kuporomoka dikteta alipochukua nchi aliivurga sana na janga la corona ikaimaliza kabisa.

Kuna hoteli ina menejment nzuri kama kibo palace? Angalia ilivyo chali sasa hivi.
 
MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha masjala ndogo ya kazi imeamuru baadhi ya mali za Hotel ya Kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo eneo la mji mdogo wa Usariver Wilayani Arumeru Mkoani Arusha zikamatwe kwa ajili ya kupigwa mnada kufidia mishahara ya waliokuwa wafanyakazi 93 wa Hoteli hiyo wanadai kiasi cha Tsh. Milioni 129.

Naibu msajili wa Mahakama hiyo John Nkwabi alitoa maamuzi hayo jana katika mahakama Kuu kanda ya Arusha masjala ndogo ya Mkoa katika kesi ya msingi namba 140 ya mwaka 2020, ya madai ya waliokuwa wafanyakazi 93 dhidi ya mwajiri wao Hotel ya Ngurdoto Mountain Lodge.

Kesi hiyo iliyosajiliwa oktoba 16 Mwaka 2020 iliendeshwa katika hatua mbalimbali na kufidia tamati jana ambapo Msajili Nkwabi kwa kuzingatia sheria za kazi alitoa hukumu ya kukamatwa ili baadae zipigwe mnada kwa baadhi ya mali za Hoteli hiyo ili kupata kiasi cha shilingi 129,570,000 za kuwalipa madai ya mishahara ya wafanyakazi hao.

Nkwabi alitaja mali hizo kuwa ni vitanda 139, Gari aina ya Coaster bus lenye namba za usajili T847 DPH, kiwanja namba 418 kilichopo Block A eneo la Leganga, Usariver, Arusha na mashine nne za nguo za kufulia.

Msajili huyo alimuagiza dalali Allan Mollel wa kampuni ya udalali ya “First World Investment Auctioneers Debt” ya jijini Arusha kukamata mali hizo mara moja ili kusubiri amri ya mahakama tarehe 4.5.2021 kwaajili ya kuuzwa kufidia mishahara ya wafanyakazi.

Pamoja na mahakama waliondesha shauri hilo mahakamani ni Ofisa kazi mfawidhi wa Idara ya kazi Mkoa wa Arusha kwa niaba ya Kamishna wa kazi dhidi ya upande wa uatetezi wa wakili Edmund Ngemela.
Sa hiv pale si ni Chuo cha Uhasibu(IAA) Arusha.au wao wamepanga.maana tulisikiaga watoto wamehamishiwa pale.ijapo miundo mbinu inasemekana si rafiki inawatesa sana wanafunzi.
 
Watulize akili, wajiweke kando watafute CEO mpya atayewavusha kwa taaluma uzoefu na weledi kwa kazi hiyo, Na taratibu watarejea relini.
 
Yule kijana angeacha tu dada yake aiendeshe kwa ushauri wa wataalam badala ya kujisimika kwa mfumo dume. ona sasa mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

Au wangeajiri wataalam kisha wao wakajiweka kando kusubiria mshiko kila mwisho wa mwezi.
Ngurdoto anaendesha yule dada n hela wanayo sijui shida ni nini,impala imefungwa ni mda sasa
 
tuseme ushauri mwingine hujauona. ugomvi wao sidhani kama umeisha. Tungefanikiwa kuwaiga wahindi hata na baadhi ya wazungu kwenye misingi ya biashara zao tungekua mbali sana
Unajua lkn hio ngurdoto iko chini ya huyo dada?
 
Back
Top Bottom