Hoteli maarufu za kitalii mkoani Arusha, Impalla na Ngurdoto Mountain Lodge zimetangazwa kuuzwa

Status
Not open for further replies.

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Hoteli maarufu za kitalii mkoani Arusha, Impalla na Ngurdoto Mountain Lodge zimetangazwa kuuzwa na Benki ya Exim (T) Limited.

Hoteli hizo ambazo zinamilikiwa na wafanyabiashara kadhaa nchini, ambapo Mkurugenzi wake Mkuu, Melau Mrema alifariki mwaka 2017 zinauzwa na kampuni ya uwakili ya Locus ya jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa matangazo ya kuuzwa hoteli hizo, mnunuzi anatakiwa kutuma zabuni kwa kampuni hiyo kupitia wakili Dk Onesmo Kyauke kabla ya April 15 mwaka huu.

Hata hivyo, mmoja wa wakurugenzi wa hoteli hizo, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake alisema hana taarifa za hoteli hizo kudaiwa na Exim Bank.

"Tumeshangazwa na hili tangazo, sisi Exim hawatudai tunadaiwa na NBC bank ambao ndio wana hati zetu na leo nimewauliza kuhusu deni hili nao wameshangaa" alisema.

Hata hivyo, alisema wanafuatilia kujua chanzo cha tangazo hilo ambalo pia linataja viwanja viwili vya Impalla hoteli.

Hata hivyo, Dk Kyauke alipotakiwa kuelezea juu ya tangazo hili alijibu kwa ujumbe wa simu yupo mahakamani.

Katibu mtendaji wa chama cha wamiliki wa kampuni za Utalii Tanzania (TATO), Sirili Ako alipotakiwa kuelezea juu ya tangazo hilo alisema ameliona lakini wao wanachohitaji ni watalii kupata huduma bora.

"Nimeona Tangazo TATO hatuhusiki kufuatilia umiliki wa hoteli sisi tunataka watalii wapate huduma bora" alisema.

Hoteli za Impalla na Ngurdoto ni maarufu sana nchini kwani zimekuwa zikipokea watalii na mikutano mikubwa ya kimataifa.

Lakini siku za karibuni mikutano imepungua ambapo pia mikutano ya Serikali inafanyika kumbi za Serikali.

Ngurdoto Mountain lodge ilipata umaarufu serikali ya awamu ya tatu na nne kwa kupokea mikutano mingi ikiwapo mikutano ya semina elekezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona naona wanadaiana billion kumi huku. Au ndiyo taarifa hii hii ya kuweka mali sokoni!
IMG_20190403_214947_265.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara nyingi za sisi Watanzania wezi yunakosa kuandaa succession plan. Ukiondoka nazo zinaondoka. Kitu hii huikuti kwa Wahindi au wengine wetu kama kule Kenya. Mfano Rais Kenyatta yuko na zile family business hazikufa kabisa. Likewise biashara kubwa DSM za kipindi zote za kurithi tu.

Marehemu Mrema alikuwa anakesha kupitia kazi zake. Je alimishirikisha nani Dos and Donts za biashara zake? Mke, ndugu, watoto au nani? Poor Us.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom