Nani alyeumba linunda la Frankenstein'?

Nani alyeumba linunda la Frankenstein'?

tubalayya

Member
Joined
Apr 16, 2010
Posts
69
Reaction score
105
Kisa kwa ufupi: Viktor Frankenstein, mwanasayansi kijana hodari, anashikwa na jazba kuu ya kutaka kugundua siri ya uhai. Hatimaye anafanikiwa kuunda linunda hai kutokana na viungo vya binadamu alivyovikusanya. Lakini ghafla anashikwa na woga na kutishika kwa linunda lile na anaamua kulitelekeza.

Linunda lile lilikuwa lina werevu wa kipindukia, lina hisia kali za kupenda, kuchukia..... tatizo watu wote hawalitaki na kila anayekutana nalo hulikimbia. Akiwa mnyonge kwa upweke na uchungu wa kutokuwa na mwenza, kiumbe yule akaamua kujifunza lugha ya binadamu na pia miondoko yao. alifanya hivyo kwa kuifuatia familia moja kwa siri. Lakini kila muda ulivyoendelea, upweke ulimfanya awe na chuki, hasira na ghadhabu dhidi ya binadamu.

'Siku moja likamtokea aliyelimbuni, Viktor, likamwambia: 'maadamu mambo yako hivi, basi nitengezee mke!
Viktor akakubali, akalitengezea mwenzi. Lakini muda mfupi baadaye akamwangamiza yule mke akihofia matokeo ya baadfaye kama lile lidudu lingezaa!

Likipandwa na hasira, lile dudu likaanza kulipiza kisasi kwa kuwauwa jamaa wote wa karibu na wapenzi wa Viktor- kakaye, rafikiye, na hata mchumba wake!

Akiwa amezongwa na hisia za dhambi, huzuni na majuto, Viktor akaanza kulitafuta lile lininda ili aliuwe. Nalo likawa lakimbia Ulaya nzima, kisha likakimbilia Amerika na hatimaye kwenye Bara la mgando la Aktiki.
Viktor akafariki katika hekaheka za kulikamata na kuliuwa dudu lile. Linunda lilipojua hatima ya muumba wake, likaanza kuhuzunika na likatokomea mbali kwenye barafu za Aktiki, likiapa kumaliza uhai wake!
Hadith imeishia hapoo.

Umefahamu nini? Kwanza, kisa hiki kimo katika fasihi karibuni zote duniani. Uingereza kinasomeshwa katika Shule za Sekondari, na Marekani kinachambuliwa katika vyuo vikuu katika vitivo vya fasihi.

Bila shaka mada kuu hapa ni juu ya hatari ya ' uncheked ambitions' tamaa na uchu usio mipaka.
Pili> Jukumu la mbunifu wa jambo, kitu.
Tatu> Hatari ya kutengwa na kususiwa.
Nne> Kisasi hupelekea mauti, hata kama si kutoka kwa aliyeumizwa.
Kwa viongozi, kisa hiki kinawakumbusha kwamba, tamaa zisizo mipaka za kutaka ufanisi wa kubuni, madaraka na nguvu bila ya kufikiria maadili (Viktor aumba Linunda bila kujali), matokeo yake ni hilaki!
Aidha, Kisa kina ishara ya umuhimu wa kuwajibika kwa muumbaji (kiongozi). Kiongozi hana budi kuwajibika, si kwa kuanzisha 'linunda' tu, bali kuliongoza, kulisimamia na kulikaripia.

Ama upweke wa Linunda uliopelekea kukimwa na kutaka kuangamiza....ni ishara ya umuhimu wa 'inclusive leadership' kiongozi apupie kuwashirikisha wengine. Lile linunda lilianza kuwa liharibifu, libomoaji na liuwaji mara baada ya kuhisi kutengwa na kutosikilizwa.

Laiti viongozi wetu wangetenga wakati wa kusoma na kuchambua visa kama hivi....tungejiepusha kuuumba Linunda!singeumba Linunda! Kisa hiki kiliandikwa 1817 !
 
Wansiasa wa CCM wapo kwenye denial mood, viongozi wamepuuza utu na thamani ya wananchi.
 
Back
Top Bottom