Nyamesocho
JF-Expert Member
- May 5, 2023
- 489
- 1,268
Hii dawa ya vidonge kwa binadamu kutibu maumivu inashangaza sana kwa namna inavyoua panya bila kubakiza hata mmoja.
Siku za karibuni nilijikuta nimevamiwa na panya zaidi ya 20 na kuzaliana ndani mwangu na kuniharibia mazao, nguo na kuwa kero ndani, nikaanza kutafuta dawa ya kuua, nikaenda dukani kununua rat and rat nikaweka nikaambulia sifuri, hakufa hata mmoja.
Nikauliza watu nifanyeje panya wananisumbua hatari wakanambia nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa Indocini changanya na unga halafu leta taarifa baada ya wiki, aisee kweli hakuna panya hata mmoja ndani.
Nimejaribu kuulizia nani aliyegundua hii dawa kwa panya ni funga kazi na wenyewe wamesema waliambiwa na wengine.
Je, ni nani hasa aliyegundua hii na kufanyia majaribio kwa panya na kugundua ni hatari, kwa nini asijitokeze apewe cheti?