Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa DSM?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam.

Ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya Makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa hali ya juu kuliko hata ofisi ya rais.

Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana matumizi?
Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na wananchi wenye hali ngumu na maisha yasiyoridhisha.picha zaidi za ukarabati huu ziko instagram page ya. QUALITY HOMES

mkuumkoa.jpg
 
Vijana wengi wanapenda sana kujikweza ndio tatizo. Ofisi ya serikali sio dhambi kuwa mzuri Bali ilitakiwa iendane na aina ya serikali ziwe sawa na mikoa mingine amepita hadi baadhi ya ofisi za mawazir lakini ndio ujana huo
 
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam...ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa halo ya juu kuliko hata ofisi ya rais,Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana natumizi? Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na t
Yote kheri. Hata wanangu nawaambia wasimwage chakula wengine wanashinda na njaa, wanakuwa Kama hawanielewi. Personally kuonyesha obvious wealth wakati wengine ni maskini, I find offensive. Hizi ni hisia zangu binafsi.
 
Mgongano wa maslahi! ! Hao ni wafanya biashara huyu sio kama yule mgambo! Huyu atakuwa simu zile , anapokea! Utaelewa hapo hapo
 
Picha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao kuonyesha ufahari wa hali ya juu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dar es salaam...ofisi hiyo imekuwa tofauti kabisa na ile ya Mkuu wa mkoa aliyepita bwana Sadick, ofisi ya makonda ina kompyuta kadhaa za apple,mapambo mengi ya kila aina yanayoashiria ufahari na utukufu wa halo ya juu kuliko hata ofisi ya rais,Nani aligharamia ufahari huu wakati hata ikulu haijabadili muonekano? Kulikuwa na umuhimu wa kuweka ufahari huo katika kipindi hiki cha kubana natumizi? Nini kilipungua katika ofisi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa mpaka ufahari uongezwe katika jiji ambalo limezungukwa na t
Ukimjua aliyegharamia halafu wewe itakusaidia nini? Kwa mfano akiamua kutumia sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kununua computer au mapambo kuna shida? Acheni hizo.
 
Back
Top Bottom