Nani ale chakula meza moja na housegirl!

Nani ale chakula meza moja na housegirl!

ndyoko upo?

Huyo shemejio ni mshamba, subiri siku atiliwe mavi kwenye msosi akili itamkaa sawa

Halafu hg nae ni binadamu hapo anatafuta tu, asipende kudharau watu

Nimesikia eti kuna wengine wanatumia mikojo kama liquid ya kupikia!

na wengine wanatumia mashine zao kuwanyonyesha watoto (h - boys!)

mmh.. hawa jamaa hawa nao wana vimbwanga vyao jamani!
 
hawa watu wapo ila cha kufanya unamwambia hapohapo kwamba si sahihi,niliwahi kupata wageni ilikuwa ni familia ya watu sita baba mama na watoto wao wanne,wakakuta mimi na binti yangu wa kazi tunawaandalia chakula ikabidi nitenge watoto wakae dinning na binti yangu akawa anakula nao,huyu mama mgeni hakupata amani gafla akaanza kumtuma binti yule wa kazi kwa vile nilimuelewa nikamwambia aniagize mimi anachotaka kwani yule anakula,hapo pozi lilimuisha na baadae mume wake akashukuru kwamba mke wake atajifunza maana huwa anawatenda vibaya mabinti(mke hakusikia mume alichosema),kipindi kingine tukaenda kwao nikaona amefanya nilivyofanya kwangu sema akawa anajisahau anamwambia "dada acha kula kwanza njoo utoe vyombo" ambapo angeweza kufanya mwenyewe,tuwathamini na kuwapenda wadada wanaotusaidia kazi,

dadangu popompo, hapo mwanaume jifanye unaingilia kuweka mambo sawa.....nadhani unaweza kuhisi shutuma utakazorushiwa na mamsampu vs huyo h.girl. Ndo maana utakuta wanaume wengi wanaishia kukaa kimya kupisha shari, ila ukweli wanawake baadhi yenu mna maajabu sana
 
Kuna familia moja nilienda kuwatembelea, kwa jinsi wanavyoishi vizuri huwezi kujua nani dada wakazi nani mtoto. Nikamuuliza msichana mmoja unasoma wapi? Akanijibu sisomi, dah! Kumbe alikua ni dada wa kazi. Nilijisikia vibaya sana kumuuliza lile swali.(Kutofautisha mtoto wa mwenye nyumba na HG haikua rahisi).

Hatukatai huenda HG wakawa na mapungufu yao lakini kuwatenga kama sio binadamu sio vizuri na sio utu pia.
 
Hafadhali hata ulio yaona huko.
Niliwahi kupanga nyumba moja na mwarabu walikuwa nyumba kubwa me nilikuwa nyumba ndogo ya nyuma jamani acheni kama kuna binadamu wanaroho mbaya kwa wafanyakazi hata hawa warabu wanaongoza yani ilikuwa nadra mfanyakazi kumaliza miezi 3 pale ikitokea hivyo labda ukute na yeye anashida sanaaaaaa!! lakini bado hata kaa zaidi ya hapo mpaka nikawa nahisi kwa hasira nilizo nazo ninge kuwa mi ninge watafutia hata dawa ya kuwa umisha matumbo na kuhara halafu nasepa..!!
 
Inategemeana na alikotoka huyo mwenye nyumba. Akiwa ametokea kwenye umasikini ghafla akajikuta ana kanafasi kadogo, watu wa jinzi hiyo nakuambia lazima wawakatae watu wadogo. Anamkumbusha mbali atiii.
Jamani, mchele ni safi ukiwa haujatiwa maji, ukiishatiwa maji umeharibika huo. Hicho chakula ni chema hakijaepuliwa, kikiisha epuliwa hayo ni ma.vi tuu. Unawezaje munyima mtu mbolea??
Kwa ufahamisho wako, wengi wenye kiroho hicho cha kuwanyima wengine vyakula vilivyopikwa wana ugonjwa fulani hivi unaowanyima wasile. Utaujua mwenyewe nisipigwe ban hapa.
Housegirl namheshimu mno mno. Ana uhai wangu mikononi mwake. Sili kwa raha nisipomwona akiwa mezani pamoja na sisi. Tena natamani hata aanze yeye kula kwanza ndipo nile kwani kukuua ni rahisi tu.
Wamama wengine wana tenga chakula special kwa waume zao, poleni mabwana wenye matumbo ya aina hiyo. Unatembea na sanda yako weye. Hutajua kilicho kuua.
House girl, ndiye mnamwachia mimali yoote humo nyumbani, anaichunga mpaka mnaporudi jioni. House girl ndiye anawalea watoto wenu wachanga mpaka mnarudi jioni, mama umechoka, baba umechoka na stress za kazi hata kucheka na mtoto huwezi, unafikiri mtoto hajui furaha ya kweli? Mtendee mema housegirl wako ili akikutenda mabaya Mungu amlipe.
Yaani nakubaliana na wewe dah kuna watu wana roho mbaya jamani huu ni UNYANYASAJI WA HAKI ZA BINAADAMU..mwanadamu mwenzie umtreat hivo just coz wamlipa yaani ale makombo ka paka wa mtaa....mi chakula hapo hata kisingeshuka kwenye koo....dah yaani housegirl anaweza kusababisha damage kubwa sana anaweza actually akuue kiutaratibu/slow death ukiwa hata hujijui...mungu anajua hata anaweza akuwekee nini kwenye hiko chakula hata mkojo wa paka for gods sake....Jamani tuache kuwapelekesha hawa viumbe ka mbwa koko...ni viumbe nao wana nafsi ka sisi...tena tunatakiwa tuwaheshimu sanaa!!!!
 
Kuna watu wana roho mbaya sana utafikiri wataishi milele

Na mbaya zaidi ni kuwa: mi rahisk kuhujumiwa na hg iwapo mnamtenga kwenye msosi. Akiwawekea mambo mabaya msosini je?
 
AAaaaahhhhhhh huyo tajiri kapewa utajir na shetan maana kwa mungu hatuko hivyo ,mbona pua inaangalia chini au atazikwa juu .............huyo tajir cha kwanza hamjui mungu chapili hajui mlango wa kanisa cha tatu shetan anamchangany .........................

MLETE KWA YESU APATE WOKOVU.
 
Nimesikia eti kuna wengine wanatumia mikojo kama liquid ya kupikia!

na wengine wanatumia mashine zao kuwanyonyesha watoto (h - boys!)

mmh.. hawa jamaa hawa nao wana vimbwanga vyao jamani!
Nipo ndugu yangu. Siku hizi naishi porini mtandao hadi upande juu ya mti na huu mchina ndo kabisaaaa!
 
Hoja yako haina mantiki kwa kuwa, kama mnakula pamoja ndiyo hawezi kuchanganya kitu chenye madhara kwa kuwa na yeye si atakula hicho hicho?!

Ila kama wakati wa kula mnamtenga wakati yeye ndiye alikuwa mpishi si ajabu akawachanganyia!
Kulingana na mada ilivyo huyo mama huwa anakula zaidi ya ma.vi.Hawa watu hasira zao huzidi kutokana na vitendo kama hivyo, maana wengi wao wananyanyasika sana.
 
Nilihuzunika sana mama mwenye nyumba alipotamka maneno haya.

Hii imenitokea nilipoenda kwa rafiki yangu niliyesoma naye O level miaka ya 90. Nilishangaa kuona ingawa yeye ndiye aliyeandaa chakula, kilipofika mezani yeye alikuwa ameketi kwa mbali anangojea tumalize kula ili naye aje kusaza mabaki.
Nilishindwa kuvumilia baadae nikauliza-wakati tunaendelea kula - iwaje msichana wa kazi hajajumuika nasi mezani.
Shemeji aliibuka na kujibu, nanukuu 'nani ale chakula meza moja na housegirl? Niliposikia maneno hayo nilikaa kimya, maana shemeji alionekana wazi hapendi kula chakula pamoja na housegirl.
Chondechonde mnaoishi na hawa mugro, jamani tuwachukulie mamugro aka beki tatu kama binadamu, kama anakupikia mlo, anakulelea wanao, na mambo mengine mengi, inakuwaje unamchukulia kama mbwa au paka anayengojea bosi ale halafu yeye atupiwe mifupa au makombo! Tubadilike jamani hasa nyie kina mama wenye nyumba, mweeeeee!

Hata statement yako bado ina madhara mabaya sana. Huwezi "binadamu ukamchukulia kama binadamu" kwa sababu kwa kufanya hivyo utakuwa unamnyang'anya hadhi ya ubinadamu. Kitu kingine kisicho binadamu kv ng'ombe mbuzi, kondoo nk ndiyo unaweza ukavichukulia kama binadamu ukipenda, kwa sababu vyenyewe si binadamu. Watu waache kucheza na binadamu kwa sababu kwa kufanya hivyo wanamchezea Mungu
 
Chakula kapika HouseGirl halafu unajidai KUMNYANYAPAA, ngoja akuwekee SUMU kwenye chakula kisha ATOWEKE!
 
Khaaaa ungemwambia Huyo mama.. What goes around...very stupid
 
Mara nyingi ni ushamba na ujinga mwingi wa hao wanaojiita mama mwenye nyumba.
 
Back
Top Bottom