Nilihuzunika sana mama mwenye nyumba alipotamka maneno haya.
Hii imenitokea nilipoenda kwa rafiki yangu niliyesoma naye O level miaka ya 90. Nilishangaa kuona ingawa yeye ndiye aliyeandaa chakula, kilipofika mezani yeye alikuwa ameketi kwa mbali anangojea tumalize kula ili naye aje kusaza mabaki.
Nilishindwa kuvumilia baadae nikauliza-wakati tunaendelea kula - iwaje msichana wa kazi hajajumuika nasi mezani.
Shemeji aliibuka na kujibu, nanukuu 'nani ale chakula meza moja na housegirl? Niliposikia maneno hayo nilikaa kimya, maana shemeji alionekana wazi hapendi kula chakula pamoja na housegirl.
Chondechonde mnaoishi na hawa mugro, jamani tuwachukulie mamugro aka beki tatu kama binadamu, kama anakupikia mlo, anakulelea wanao, na mambo mengine mengi, inakuwaje unamchukulia kama mbwa au paka anayengojea bosi ale halafu yeye atupiwe mifupa au makombo! Tubadilike jamani hasa nyie kina mama wenye nyumba, mweeeeee!