Nani aanze,, mtoto wa kike au wa kiume????

NICOLAS ELEUTER

New Member
Jun 12, 2012
1
0
Inavyosemekana wanaume wengi hususani tunaokaribia umri wa kuoa tunakuwa na kipaumbele cha mtoto wa kiume*
hali suala la mwendelezo wa vizazi katika ulimwengu unamhusisha mwanamke moja kwa moja,
,,,,,,,,,,sijajua hili limekaaje kwa nyie wengine!!!!!!
 
Kumbe! Nilikua sijui..
Nijuavyo mie mtoto ni mtoto regardless jinsia yake na kwenye issue ya kuendeleza vizazi wote wanahusika cause wa kiume hawezi kuendeleza ukoo bila kua na mke na wa kike hawezi kuendeleza kizazi bila kua na mume..so acording to me kila mtoto ana umuhimu wake na wote wanategemeana haijalishi nani amekua wa kwanza kuzaliwa kwenye familia au wa mwisho!
 
Kumbe! Nilikua sijui..
Nijuavyo mie mtoto ni mtoto regardless jinsia yake na kwenye issue ya kuendeleza vizazi wote wanahusika cause wa kiume hawezi kuendeleza ukoo bila kua na mke na wa kike hawezi kuendeleza kizazi bila kua na mume..so acording to me kila mtoto ana umuhimu wake na wote wanategemeana haijalishi nani amekua wa kwanza kuzaliwa kwenye familia au wa mwisho!

Naunga mkono hoja.
 
Na ukitaka wa kiume then kila ukijaribu anakuwa huyo huyo wa kiume, will it make you happy?
What if ukataka wa kike then kila ukijaribu tena anatoka wa kike?
Ukiniuliza mimi hata sijui....Kwa experience yangu fupi nliyo nayo na haya maisha nimeona hivi;
Nikitoka asubuhi nyumbani nnakuwa nimeipangilia vyema ratiba ya siku yangu ila matokeo ni hivi-
a) Kuna vitu vinakwenda kama nilivyovipanga na matokeo yake huwa yanajenga maisha yangu
b) Kuna vitu vinakwenda kama nilivyovipanga na matokeo yake huwa yanabomoa maisha yangu
c) Kuna vitu haviendi kama nilivyovipanga na matokeo yake huwa yanabomoa maisha yangu
d) Kuna vitu haviendi kama nilivyovipanga na matokeo yake huwa yanajenga maisha yangu

Well, tumefundishwa kwamba unaweza kupanga ni mtoto wa jinsia gani azaliwe na akazaliwa but nimewauliza wanandoa wenye experience zao wamesema hiyo ni probability bado. Unayajua mapenzi ya Mungu kwa maisha yako na ya wanao? Why unasumbukia mambo ambayo una uwezo mdogo wa kuyacontrol? na ukishayacontrol hujui kama ni ya faida kwa maisha yako?
 
Mtoto ni mtoto hajalishi ni wakike au wakiume. Pia ni majaliwa ya mwenyezi mungu, wewe unatamani, mwenyezi mungu anapanga
 
kuna watu bado wana mawazo haya ya wakati wa UJIMA?
siku hizi kuna tofauti kati ya mtoto wa kike na wa kiume?
kuna siku nilimuudhi sana classmate wangu, alikuwa mkenya ambaye hajui thamani ya wanawake. siku hiyo nikamtolea uvivu, nikamwambia mimi na yeye tuna tofauti moja tu! jinsia....................
vingine vyote tunafanana; wote tunaingia darasani, tunafaulu mitihani, tunafanya kazi, tunavaa suruali......... upuuzi wako peleka kwa mkeo ambaye unataka akae nyumbani tu azae na kulea watoto. akaniambia anamuhurumia mume wangu, lol!
 
Uumbaji ni kazi ya Mungu....Rafiki yangu mmoja alikuwa na mtoto wa kwanza wa kike akaenda kwa gyno...ili next apate mtoto wa kiume...kweli akaconcive kati ya tarehe alizopewa lakini mwishowe akatoka tena wa kike...wakati mwingine kwa ubinadamu wetu tunategemea sana akili zetu na kusahau kuwa kazi ya uumbaji ndani c yetu....omba Mungu atakupa hitaji la moyo wako.....4 ur info...ziko family zenye watoto wa kike wa kutosha na wa kiume wa kutosha...mwishoni katika uzee wa wazazi wa ile family wamegundua kumbe wa kike ndio wenye kukumbuka nyumbani zaidi(bahati yao waliwasomesha wote bila kubagua)
 
Kama iko mikononi mwangu, I would prefer a girl, watoto wakiume takes longer to mature na kuchukua responsibilities. Akioa ndio umemzalia mwanamke mwenzako hakumbuki nyumba. Ningependa kupata boys after I had atlest a girl.
 
Inavyosemekana wanaume wengi hususani tunaokaribia umri wa kuoa tunakuwa na kipaumbele cha mtoto wa kiume*
hali suala la mwendelezo wa vizazi katika ulimwengu unamhusisha mwanamke moja kwa moja,
,,,,,,,,,,sijajua hili limekaaje kwa nyie wengine!!!!!!

hivi kuna waliomfahamu anachosema hapa??
 
Pole pole wakuu msijegombana....ni majaliwa yake MUNGU ee~e~eee kuuona mwaka.
 
Kuna myth nyingi kuhusu watoto; kuna taifa moja europe wanaamini mtoto wa kwanza akiwa wa kike analeta bahati; sijuhi bahati gani lakini. Waafrika wengi hasa wanaume wanapenda mtoto wa kiume kwa sababu ya prestige; wenyewe wanasema kidume cha mbegu. Wanawake mara nyingi hatuna conditionalities kwenye mapenzi ya wanetu. I love my boys regardless of their sex.
 
Back
Top Bottom