Namwombea Msamaha Job Ndugai

Namwombea Msamaha Job Ndugai

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,934
Job Ndugai ni mwanachuo mwenzangu pale UD miaka hiyo.

Mengi yasiyopendeza yamesemwa dhidi yake kwa nafasi aliyo nayo, hasa kwa namna alivyolifuta Bunge na kulifanya kuwa idara ya SerikaliRais kipindi cha uongozi wa Marehemu.

Kipindi cha uongozi wa marehemu, Bunge lilibakia jina tu, lakini halikuweza kufanya kazi yoyote ya kibunge zaidi ya kubakia kuwa kaidara ka Serikali.

Lakini Ndugai huyu hakuwa hivyo mwanzo, na anataka kutokuwa hivyo kwa sasa. Tujiulize, nini kilimtokea hata akawa vile?

Tusisahau kuwa ambaye alitenda kinyume cha utu, imani, na msimamo wake wakati wa utawala wa marehemu, hakuwa pekee yake, walitofautiana tu kwa viwango.

Rais wetu Samia anayesisitiza haki, demokrasia, kodi zisizo za uonevu, hakuweza kutamka hivyo akiwa chini ya marehemu.

Mwigulu ambaye sasa anasema TRA wasiwabambikie kodi wafanyabiashara, hakuweza kunena hivyo enzi za marehemu, tena alimsifia marehemu kama vile ni mtakatifu aliyeshushwa toka mbinguni.

Musukuma anayesema sasa kuwa walionyang'anywa viwanda na utawala wa marehemu walionewa, hakuthubutu hata kuota kama angeweza kutamka jambo hilo. Kila siku bungeni alibaki kuimba mapambio ya kumsifu marehemu.

Kimei anayesema walioonewa na kubambikiwa kodi, Serikali iwarejeshee, akiwa mkurigenzi wa CRDB aliwahi kuidhinishwa kujengwa jengo la ghorofa kijijini Chato wakati hakuna wateja.

Kabudi aliwahi kumwita Magufuli Mungu. Mwanrwi aliwahi kunena kuwa Mungu anatakiwa amshukuru Rais Magufuli. Kangi Lugola alisema Rais Magufuli ni Yesu. Hawa wote, kama kweli wanamwabudu Mungu wa kweli, wanatakiwa wafanye toba ya pekee kwa kukufuru.

Lakini kwa nini hawa wote watende na kunena ya ajabu kiasi hicho? Sisi wengine hatujui, lakini wao waliokuwa karibu na marehemu wanajua kwa undani ilikuwa hatari kiasi gani kutokubaliana na aliyokuwa anayataka.

Kutokana na Ndugai anayoyanena sasa mara kadhaa Bungeni, unapata ujumbe wa aina 3:

1) Anajutia kwa kuunga mkono udhalimu
2) Anataka kuwaomba msamaha Watanzania lakini anakosa ujasiri
3) Anataka ayahitimishe maisha yake katika nafasi aliyo nayo kwa heshima, lakini anajua kuwa aliyoyatenda yamemwondolea heshima na kumfanya aonekane mtu asiye na msimamo, mnafiki, kigeugeu na asiyeaminika.

Kwa kuwa huyu collegemate inamwia vigumu kusema anaomba msamaha kwa kauli ya moja kwa moja, naomba tumsamehe na tumwombe aungane na Mama Samia katika kuhakikisha Taifa linapata katiba iliyo bora. Katiba ambayo vizazi vijavyo vitatenda kazi kwa mujibu wa sheria na katiba bila ya hofu yoyote toka kwa yeyote.

Najua Ndugai amewakera wengi, lakini kwa yale mazuri machache aliyoyatenda, yatoshe kupata msamaha wa mabaya aliyoyatenda. Kumbukeni hapo mwanzo, hata wapinzani walimpenda Ndugai, na siyo Tulia. Alivyorudi toka kwenye tiba, wabunge wengi walifurahia. Hapa kati, aliingiwa na nguvu ya shetani iliyozidi uwezo wa kuihimili.

Namwombea msamaha.
 
Tukitaka kuwalaumu watenda kazi waliopo, tuanze na Raisi mwenyewe mana alikuwa ofisi moja na mheshimiwa ambaye tunamtupia lawama Kwa mambo mengi.

Kwa nini awaone wenzake hawafai , wakati walikuwa kapu moja na yeye ndo alikuwa karbu zaidi na mheshimiwa kuliko mtu yyte Yule ...... Waanze tu upya wote wasilaumiane Kwanza.

Angalau baada ya mwaka mmoja hv ndo waanze kuwajibishana. Sio wengine wageuzwe mbuzi wa kafara.
 
Job Ndugai ni mwanachuo mwenzangu pale UD miaka hiyo.

Mengi yasiyopendeza yamesemwa dhidi yake kwa nafasi aliyo nayo, hasa kwa namna alivyolifuta Bunge na kulifanya kuwa idara ya SerikaliRais kipindi cha uongozi wa Marehemu...
Tutamsamehe kwa masharti kuwa awezekufufua mjadala wa katiba pendekezwa ya Jaji warioba,aisimamie tupate katiba mpya tuondokane na uwezekano wa kupitia tena kipindi kigumu kama kilichopita hivi karibuni.
 
Tukitaka kuwalaumu watenda kazi waliopo, tuanze na Raisi mwenyewe mana alikuwa ofisi moja na mheshimiwa ambaye tunamtupia lawama Kwa mambo mengi ....Kwa nini awaone wenzake hawafai , wakati walikuwa kapu moja na yeye ndo alikuwa karbu zaidi na mheshimiwa kuliko mtu yyte Yule ...... Waanze tu upya wote wasilaumiane Kwanza.....!!!angalau baada ya mwaka mmoja hv ndo waanze kuwajibishana...!!! Sio wengine wageuzwe mbuzi wa kafara ....
Hatari na nusu
 
Shirikisha ubongo wako ndugu,mama alikuwa msaidizi wa mwendazake ilihali dungai alikuwa mkuu wa Mhimili Kama alivokuwa magu
 
Job Ndugai ni mwanachuo mwenzangu pale UD miaka hiyo.

Mengi yasiyopendeza yamesemwa dhidi yake kwa nafasi aliyo nayo, hasa kwa namna alivyolifuta Bunge na kulifanya kuwa idara ya SerikaliRais kipindi cha uongozi wa Marehemu...
Amekutuma? Alishalikoroga hana budi kulinywa mwenyewe!
 
Mmerudi enzi za business as usual,kuwadanganya watu tu ili muibe,misemo yenu ya kula na kipofu mmeanza kuongea sasa
 
Kama kweli anatubia toba ya kweli hebu aanze na kuwashughulikia wale wabunge 19 wa CHADEMA ambao sio tu hawatambuliki na chama chao bali hata wana CCM kadhaa wameonyesha kutoridhishwa na ukiukwaji wa waziwazi kabisa wa katiba ya nchi. The bigest culprit katika hili na yeye mwenyewe Spika Ndugai na ofisi yake kwa ujumla

Marehemu hawezi kurudi. Na naamini hana cha kuogopa kwa sasa. Akichukua hatu za haki kwa hao "wabunge" ninaimani uma utamsamehe kama ulivyomuombea
 
Arudishe $12 million alizopewa na mwendazake eti za matibabu yake kule India pia atubu kuhusu kuhusika kwa kuondolewa kinyemela CAG Assad. Vinginevyo hastahili kusamehewa kwa chochote huyo dhalimu.
 
Binafsi nakusehe wewe kwa makosa mawili.
1. Kukubali kuwa collegemate naye
2. Kujaribu kumwombea msamaha mtu ambaye bado hajui kosa lake. Badala ya kumpigia na kumkanya, unatumia mda mrefu kumwombea msamaha.
Ila nakusamehe bure
 
Shirikisha ubongo wako ndugu,mama alikuwa msaidizi wa mwendazake ilihali dungai alikuwa mkuu wa Mhimili Kama alivokuwa magu
Kati ya Mimi na ww wa kushirikisha ubongo ni Nani we kilaza , Kati ya ndugai na mama Samia Nani alikuwa boss kwa mwenzake...ni mpuuzi Tu anayeweza kumlaumu ndugai alaf ukamwachia Samia ,na hili hata Kigogo analisemea
 
Job Ndugai ni mwanachuo mwenzangu pale UD miaka hiyo.

Mengi yasiyopendeza yamesemwa dhidi yake kwa nafasi aliyo nayo, hasa kwa namna alivyolifuta Bunge na kulifanya kuwa idara ya SerikaliRais kipindi cha uongozi wa Marehemu...
Kumbe alisoma UD. Mwaka gani na kozi gani?
 
Job Ndugai ni mwanachuo mwenzangu pale UD miaka hiyo.

Mengi yasiyopendeza yamesemwa dhidi yake kwa nafasi aliyo nayo, hasa kwa namna alivyolifuta Bunge na kulifanya kuwa idara ya SerikaliRais kipindi cha uongozi wa Marehemu..
Kumbe ndugai unatumui hii ID pia? Omba mwenyewe Kama alivyofanya kheri James.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Kati ya Mimi na ww wa kushirikisha ubongo ni Nani we kilaza , Kati ya ndugai na mama Samia Nani alikuwa boss kwa mwenzake...ni mpuuzi Tu anayeweza kumlaumu ndugai alaf ukamwachia Samia ,na hili hata Kigogo analisemea
Unaona Sasa ulivo ng'ombe? Mama alikuwa mkuu wa Mhimili? Au hata hujui maana ya Mhimili.Ndugai alikuwa na nguvu Kama Angekuwa na akili sema akili zake ni Kama zako tu
 
Back
Top Bottom