Namuombea msaada mlemavu aitwaye ndugu Erneus Athanas

Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,733
1,648
Habari wana-JF,
Nimekuja kwenu ndugu zangu kwa ajili ya kumuombea msaada mlemavu aitwaye ndugu Erneus Athanas Mhagama wa Jijini Mbeya.

176582d9ad6f397f18119688a7280bdb.jpg

a1517b35a6bd4e2c6c6bb8dbc187ca20.jpg

d35e400e5949c15f8e707817deb8ad0a.jpg

Mhagama


Msaada anaouhitaji yeye ni kupata bajaji ili aweze kwenda sehemu mbalimbali maana hupata tabu sana barabarani pia itakuwa kama mtaji ili aendeshe maisha yake na asiwe ombaomba barabarani. Hivyo ndugu zangu kama unaweza kumpa msaada au kumtafutia shirika,kampuni au mtu binafsi atakayeweza kumsaidia kwa kadri alivyobarikiwa unaweza kumtafuta kwa namba yake ambayo ni 0755160025.


MUNGU AKUBARIKI PALE UTAKAPOGUSWA NA KUFANYA KITU KWA AJILI YAKE
 
Naomba utuwekee namba ya tigo pesa, wanasema usitangaze unachotoa ila mimi nataka nimtumie ka-msimbazi asap.
Note: Hakikisha unaweka namba ya Tigo pesa.
 
Naomba utuwekee namba ya tigo pesa, wanasema usitangaze unachotoa ila mimi nataka nimtumie ka-msimbazi asap.
Note: Hakikisha unaweka namba ya Tigo pesa.
Namba ya Tigo hana ila unaweza kutuma kwa namba hii 0712349789 nitamfikishia mchango wake

Note; Naomba ukituma hela utume hata sms ili kujua ni nani na kujua ni kwa ajili yake.
 
kuna watu hapa duniani tangu kuzaliwa kwao wao ni huzuni nwanzo mwisho na mmoja wapo in huyu ndugu.
minguu ndo hivyo tena,macho nayo moja hakuna hali yake kiuchumi inaonekana tuu ya kwamba ni mbaya sanaa,lugha ya picha inajidhihirisha eeehhh M/Mungu wape watu moyo was kutoa apate walau unafuu maana kwa umri huo ni wazi kwamba matatizo mengi saana ameshayapitia.
Hima tumsaidie ndugu yetu huyu wakuu
 
Nisaidie jinsi ya kupata mawasiliano yake
Nakumbuka kipindi fulani nilikuwa nasoma Mbeya chuo fulani. Siku moja akaja jamaa mmoja bubu na ''anaongea'' kwa kuandika kwenye karatasi. Akatumbia yeye ni yatima anakenda chuo cha viziwi na alipokuwa njia ameibiwa vitu vyote. Wanachuo wakahurumia na kuchangia fedha ya nauli na kununulia mahitaji mengine. La haula... jioni moja tukamkuta klabu ya pombe ananywesha mademu. Wala sio bubu! I hope na wewe hufanyi utapeli.... Na ingekuwa vizuri sana ukatafuta njia ya kuaminisha watu kuwa wanamsaidia mtu anayehitaji msaada kweli kweli na si utapeli!
 
Back
Top Bottom