Namtongoza wife kwa mara ya pili

Namtongoza wife kwa mara ya pili

socket

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
305
Reaction score
435
Kwa miaka zaidi ya 7 sasa nimekuwa nikibadili wanawake.

Kuna usemi kwenye kitabu cha dini unasema utajijaribu kwa tamaa zako mwenyewe.
Mwanaume unaenda kufanya manunuzi au unaenda kupiga balimi na mda mwingine mishe za kazi unakutana na mrembo anakuhudumia vizuri na story mbili tatu mwisho mnapeana namba na appointment mnaenda out.

Siku zinavyoenda matumizi mnapokuwa out yanaongezeka, hapa utaanza kugharamikia nguo, salon, kucha, vocha, simu kama anataka kubadili, kodi na mtaji. Ndani ya miezi 6 unaweza kujikuta umedate na wanawake hata wa3, hapa nazungumzia wale wenye matumizi ambayo kwa mwezi si chini ya 200K yaani 600k.

Baada ya tathmini ya matumizi nikaona hapa sitakuwa na wakumlaumu uzee ukikaribia na sina kitu pamoja na kuwa kwa sasa nayafaidi maisha.

Mwezi wa 6 nilibahatika kuwa kwenye safari ya kwenda kuona viwanja maeneo fulani Wilaya ya Kigamboni ambayo unaweza kulipa kwa awamu kuanzia miezi 6 -20 na viwanja viko pembezoni mwa bahari ya hindi kwa bei ya 18,000/sqm. Maana yake ni kwamba Tsh 600,000 kwa mwezi unapata sqm 33 (mita za mraba 33) na kwa mwaka ni sqm 400. Kwa miezi 20 unaweza kuwa na sqm 800. Nilifanya maamuzi ambayo mwezi wa 12 nitamaliza deni dogo baada ya kuchukua sqm 1100 ( hapa ni baada yakuunga akiba zangu pamoja na ile 600k).

Toka muda huo hata nikikutana na pisi bila kujali mazingira huwa sikuchukui namba maana najijua ni dhaifu na haitapita wiki nitakuwa nimesharusha nyavu na matumizi yameanza.

Sasa hapa nimeamua niwe namtongoza wife na nitawapa mrejesho jinsi kimasihara itakavyofanya kazi kwa wife.

Itaendelea.
 
Asante kwa wazo zuri
Ila usisahau kumwambia “nikinywa maji nakuona kwenye glass”
 
Muwe mnasemaga kweli sio mnafanya watu wanajiona hawafai kumbe mnashindia mihogo[emoji12][emoji12]
 
Kwa miaka zaidi ya 7 sasa nimekuwa nikibadili wanawake.

Kuna usemi kwenye kitabu cha dini unasema utajijaribu kwa tamaa zako mwenyewe.
Mwanaume unaenda kufanya manunuzi au unaenda kupiga balimi na mda mwingine mishe za kazi unakutana na mrembo anakuhudumia vizuri na story mbili tatu mwisho mnapeana namba na appointment mnaenda out.

Siku zinavyoenda matumizi mnapokuwa out yanaongezeka, hapa utaanza kugharamikia nguo, salon, kucha, vocha, simu kama anataka kubadili, kodi na mtaji. Ndani ya miezi 6 unaweza kujikuta umedate na wanawake hata wa3, hapa nazungumzia wale wenye matumizi ambayo kwa mwezi si chini ya 200K yaani 600k.

Baada ya tathmini ya matumizi nikaona hapa sitakuwa na wakumlaumu uzee ukikaribia na sina kitu pamoja na kuwa kwa sasa nayafaidi maisha.

Mwezi wa 6 nilibahatika kuwa kwenye safari ya kwenda kuona viwanja maeneo fulani Wilaya ya Kigamboni ambayo unaweza kulipa kwa awamu kuanzia miezi 6 -20 na viwanja viko pembezoni mwa bahari ya hindi kwa bei ya 18,000/sqm. Maana yake ni kwamba Tsh 600,000 kwa mwezi unapata sqm 33 (mita za mraba 33) na kwa mwaka ni sqm 400. Kwa miezi 20 unaweza kuwa na sqm 800. Nilifanya maamuzi ambayo mwezi wa 12 nitamaliza deni dogo baada ya kuchukua sqm 1100 ( hapa ni baada yakuunga akiba zangu pamoja na ile 600k).

Toka muda huo hata nikikutana na pisi bila kujali mazingira huwa sikuchukui namba maana najijua ni dhaifu na haitapita wiki nitakuwa nimesharusha nyavu na matumizi yameanza.

Sasa hapa nimeamua niwe namtongoza wife na nitawapa mrejesho jinsi kimasihara itakavyofanya kazi kwa wife.

Itaendelea.
Unamtongoza wife....una wife tayari au unamtongoza mwanamke atajayekuja kuwa wife?
 
Back
Top Bottom