Namtafuta ndugu yangu anaitwa Ester Wilbard

Namtafuta ndugu yangu anaitwa Ester Wilbard

Ndugu yangu anaitwa Ester Wilbard, nilipotezana nae mwaka 2012 akiwa Katoro Geita, alikua anajihusisha na kazi ya mama ntilie ila kwao ni mzaliwa wa Ngara.

Lengo la kumtafuta aliacha mtoto wake mdogo sasa hivi kawa mkubwa anatamani kumuona mama yake.

Kama kuna mtu anamfahamu au anafahamu alipo naomba tuwasiliane

Ukafanikiwe kumpata.
 
Sijui kwa nini moyo wangu umeingia simanzi na hii habari....kukosa upendo wa mama ni kitu kinaumiza Bora ujue ametangulia mbele za haki...kila lenye kheri
 
Hili swali linakwepwa sana, "HUYU MTOTO ALIFIKAJE KWAKO? HUYU MWANAMKE NI DADA YAKO AU NI NDUGU YAKO KIVIPI?"
Hili swali hata nikijibu sidhani kama itasaidia sana, ndo maana najibu maswali yenye mlengo wa kusaidia kumpata
 
Inamaana hapo geita alikua Hana rafiki, alipokua anauza chakula hakua na mtu anamshirikisha mambo yake?Fatilia kuanzia alipokua anafanyia biashara ama kukaa, nenda hatua kwa hatua. Ni njian ndefu ila itakusaidia
 
Dah huyu dada bwana ,Sasa uliacha binti masikini ila hautaki kumkumbuka walau umuone ? Shida ni nini ndugu ?

Wacha na Mimi nichukue hii picha nikenda mjini nitawauliza uliza watu anaweza kupatikana maana watu wa hivi wanakaaga mijini huko
Huwezi jua, huenda hata alifariki.
Yote Mungu anajua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom