Namtafuta baba yangu Gervas Kalilo

Umeiona comment yangu?

Kuna kina kalilo nawafamu nijibu maswali yangu hapa hapa then nitakupa namba hapa kama uko tayari niambie
Ndio niko tayari mpen
Maumivu yake ni makali mnoo 😪 pole yake pia
 
Nitajie majina kamili ya baba yako?
kabila lake?
Dear simfaham ningejua majina yake kamili na kabila huenda ningekua nishampata lakini sijui nachojua ni majina hayo tu mawili (GERVAS KALILO) na jina la balozi kwenye card la clinic waliandika samson gwagu
 
Dear simfaham ngejua majina yake kamili na kabila huenda ningekua nishampata lakini sijui nachojua ni majina hayo tu mawili na jina la balozi kwenye card la clinic waliandika samson gwagu
Naweza kukusaidia lakini maelezo yangu ni hayaridhishi.
KALILO MZEE.
huyu alifariki mwaka Jana
ana watoto wengi mmoja aliwahi kufanya kazi milembe, mwingine nmb, mpiga picha na mmoja muwindaji.
1. Huyu muwindaji ana vistori na ndio kidogo hiyo story yako imekonnect kwako. huyu aliwahi kufanya kazi miaka hiyo uhindini kahama katika ukoo wa gogadi.
kwa sasa anaeendelea na maisha yake yuko
Anapatikana sehemu moja kama unaenda nyakanazi panaitwa kasilo. na kasilo iko jirani na runzewe.
lakini bado maelezo yako ni machache mno. jaribu kuongea na ndugu wa mama yako akupe maelezo kidogo.
 
Wakunipa story kamili kuhusu baba yangu ni mama yangu pekee nae alifariki ningali mdogo upande wa mama hakuna anaemfaham baba yangu maana mama yangu maisha yake mengi yalikuwa kahama uhindini pia hakua mtu wa kutangaza mambo yake angekua mwingine vile mjamzito na mimba ya kwanza angerudi kwao lakini yeye hakurudi wala hakuotoa taarifa kama ni mjamzito nahis angejifungua kawaida angerud nyumban na mtoto kilichofanya boss wake aende masumbwe kumchukua bibi nahis ni kwa sababu ya C-section yaan kwao alikua anaenda tu kutembea kusaidia mahitaji na kurud Kahama hakuwahi kuniacha kwao na history ya kifo hakuumwa muda mrefu kwa kifupi bibi hamjui baba yangu na baada ya mtt wake kufariki hakufatilia kule Kahama kwa boss wake mama cha kunisaidia ni labda unipe contact za mmoja wa watoto wa KALILO unaemjua wewe kisha nitawatafuta kama mimi ni ndugu yao tutajua na kama ni majina tu yamefanana tutajua pia.
 
Sawa, nitawapa hilo jina la Gervas kalilo na kama wanafahamu chochote nitakupa namba hapa hapa.
 
Mungu akujalie hitaji lako
 
Nenda hapo unapoambia mama alikuwa anafanya kazi. Tafuta huyo mtu aliyekuwa akifanya kazi kwake kisha muulize. Na huyo bosi aliyekuwa wa mama yake mtafute rafiki mkubwa wa bosi wa mama yako. Kingine tafuta aliyekuwa karibu na mama yako au rafiki wake kipindi hicho. Kwanini uwatafute marafiki? Wao ndio wana siri kubwa za marafiki zao.

Unapokuwa katika mahusiano huwa, kuna rafiki yako ambaye anajua hali na kile kinachoendelea katika mahusiano hayo. Kwaiyo ni rahisi kupitia rafiki kujua ukweli
 
Ni kweli lkn nampatia wapi huyo rfk wa mama kwa jinsi tangazo nilivyolipost sehemu nyingi nilitegemea boss wake atajitokeza lkn haijawa hivyo ndug labda wajitokeze wao maana mimi binafsi siwajui hata alipokuwa anafanya kazi mama sipajui pia
 
Facebook Kuna ppl age ya Club Tz,naona wengi wanakutanishwa na wapendwa wao waliopotezana muda mrefu,,,Kuna Mmoja hakuwahi kumuona baba yake,kama wewe hivi,,,uzuri yeye baba yake alikuwa injinia alienda site huko singida akaacha mimba,,,

Utampata.
Huyo club tz club amenipostia tangazo zaidi ya mara 4 hata jana kalirudia ni kweli wengi wamefanikiwa kupitia page yake lakini mimi bado sijafanikiwa mkuu
 
Hii ndiyo comment imesuuza roho yangu! Kongole bwashee na Hongera kwa Pierina Vicka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…