Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,535
Wakuu umofia kwenu...................!
Miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini wanaotajwa tajwa kwamba huenda wakajitokeza na pengine kupitishwa kugombe nafasi ya Urais wa nchi hii, ni pamoja na Waziri wa mambo ya nje Mh. Bernard Membe.Ijapokuwa mwenyewe hajatangaza nia, ila zipo dalili kwamba huenda akaishika njia hiyo!.
Binafsi si mfahamu sana Mh.Membe. Ninachojua tu ni kwamba ni waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, wizara ambayo ameweza kuiendesha kwa umahiri na busara kweli kweli!.Ninachojua ni kwamba Mh.Membe ni mwanadiplomasia,tena mwanadiplomasia mahiri na hata tabia yake inamtambulisha hivyo.Ni mtu mtaratibu mwenye busara, busara ambayo ameidhihirisha wazi katika kushughulikia misuguano kadhaa kati ya Tanzania na nchi nyingine.Zaid ya hapo, binafsi simjui sana mwanasiasa huyu.
Ningependa kufahamu yafuatayo kutoka kwa wadau.
1. Je! Mh. Membe ana kashfa yeyote ya ufisadi?
2. je! ana kashfa yeyote katika suala la maadili ya uongozi?
3. Je! ana kashifa yoyote ya kijamii?
Kama hayo yote hana, ningependa kujua historia yake ya kiuongozi pamoja na elimu yake.
Ninachojaribu kuwaza ni kwamba, ikiwa CCM, Watampitisha mwanasiasa ambaye ni msafi na hana kashfa,mwanasiasa mwenye elimu nzuri, upeo mpana, na uzoefu wa uongozi, basi huenda uchaguzi wa 2015 ukapendeza sana sana! Mara huku kasimma Zitto, Mara kule kasima Membe au sijui nani......!.mara kule kasima yule! Basi tutarajie kuona mijadala mikali kwenye TV n.k, mijadala itakayojikita juu ya uchumi, masuala ya kijamii na masuala ya kimataifa ambayo itakuwa inatawaliwa na weledi mkubwa kulingana na upeo wa wahusika. Hii itakuwa ni bora kuliko kusikia siasa za mipasho mara fulani kahongwa na fulani, mara fulani kafanya vile, mara......!: siasa ambazo kwa sasa hazina tija tena.