Namshukuru Mungu....

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
21,239
36,274
Habari zenu,

Yaani.leo jumatatu, kwa yaliyonikuta hata napata nguvu na utashi wa kuandika hapa..... acha namshukuru Mungu.... acha niimbe siku nzima leo. Ushuhuda baadae.

Ni kwa Neema tuu na Rehema.

Update:

Habari za muda wa ndugu, poleni kwa kuwaweka hewani. Ilinibidi kuweka uzi asubuhi kwa namna ile sababu sikuwa na muda.

Kasie amekuwa mtu wa matukio sana, na mengi yapo huyaleta humu.
Kilichotokea leo asubuhi ni kuwa, huku kazini kulikuwa na fukuto la mabosi kuondoshwa kazini, sasa ikatokea fitina. Msione hivi mjue hata wazungu nao wanafanyiana fitina na mizengwe, immediate supervisor wangu na bosi walikuwa kwenye hali hata ya kutimuliwa kwenye kampuni sababu ya fitina tuu wala hakuna kosa la kiutendaji.
Kwanza kitengo chetu ndo huwa kinachangia faida kubwa kwenye kampuni. Sina. Leo tumekuwa surprised kitengo chetu tumepewa barua za nyongeza ya mshahara, posho ya makazi usafiri na mawasiliano. Wale waliokuwa wanaleta fitina wamepewa barua za warning kwa utendaji mbovu. Si kuwa nafurahia wao kuonywa bali sikutegemea jamani looh, nnavopenda kusafiri na kula bata walaah ntakuwa kifutu kwa furaha.

Jambo moja likanijia, mie ni mkristo, huku SA nasali kanisa la walokole napenda sana kuimba na kuabudu na huku ibada yao asilimia 70 ni kuimba na kuabudu. Nikipata off nikija bongo ntaenda kufufua kadi yangu ya sadaka kanisani niwe naweka zaka na fungu la kumi kuanzia sasa. Maana kama Mungu amenitendea haya bure wacha sasa nami nirudishe shukrani walau kwa kadri alivyonibariki.

Pia ntaongeza kiasi cha akiba nnayotenga kwa ajili ya kujiandaa kustaafu. Zinazobaki ni kutumbua tuu.

Kutoka moyoni namshukuru Mungu.

Nna furaha sanaa.

Kasie Cough Kasiba.
 
Nachukia siredi ambazo hazina kichwa wala miguu. Kwaio unataka watu wakuulize pm kilichokutokea
 
Kasie Kasiba.
 
Natamani nikuwekee wimbo wa GOD IS WATCHING FROM A DISTANCE by BETE MIDLER, ila simu yangu imeniangusha.

Aaawww you..... where have you been friend.... don't disappear that much you are missed you know.....

You just left my mouth woowed..... open like a bowl..... I know the song and I like it.
Tulikuwa tunaimba wakati nasoma shule za masista miaka hiyo.....

Thanks for the song best.

Here it is..

Kasie Cough Kasiba, asante kwa kunisaidia kuweka huo wimbo. Thanks.

Kazini kuna mambo mengi sana mama, na katika hayo, MENGI ni fitina tu. Waswahili wanasema FITNA. Na kuna watu wanajua FITNA!!!!!! Ahhhh Acha kabisa.

Ila try me, watu wengi wanaofanya FITNA makazini huwa hawana raha wala amani, sio kazini wala majumbani mwao, pathetic fools.

Mungu ni mwema wakati wote, huwa hakubali upate shida kwa muda mrefu kwa figisu ambazo hazikuhusu.

Daudi kwenye Bible anasema, nitaamka usiku wa manane nilisifu jina lako. Sio kuomba, no no no!!! Only to praise HIM.
 
Back
Top Bottom