Namshukuru mungu sikusoma UDSM

TAFADHALI SANA nakusihi kwa paa na ayala wa angani usionyeshe ujinga kwenye forum kama hii ambayo imeitwa ya watu wenye uwezo wa kufikiri sana. Sidhani kama ulishirikisha ubongo wako wa ufahamu na hekima kutoa mada hii hewani. Nafahamu kua waliosoma na wanaoendelea kusoma katika chuo kikuu cha DAR ES SALAAM ni waungwana na wastarabu na wala hawata jihusisha na kujibu ujinga huo. Hilo sio jambo la KUMSHUKURU MUNGU KABISA nadhani katika fani uliyosoma kama kweli umesoma kati ya mapungufu makubwa uliyo yapata ni kuto pita katika mlima ule. POLE SANA najua unajutia kwa kua kama umesoma hivi vyuo vinavyo itwa vya kata ni kutokana na kufaulu kwako kwa kiwango kidogo.

Nna uhakika kabisa ulipo pata usaili katika chuo hicho ulichosoma au unachosoma ulisema tu haya ila hamu yako kubwa ilikua kupitia pale. samahani sana hebu jaribu kama kukosea uende kijijini useme unasoma chuo kikuu halafu jutaje hicho chuo chako cha kata ulichosoma kama watakuelewa. Tafadhali kama ni muungwana hata wa asilimia sufuri tutake radhi kwa kauli yako.
 
I will always say, UDSM is still the best not only in Tanzania but in Africa and the world at large.. Nimesoma pale, nimemaliza nimefanya kazi nimerudi pale now. Hawa wanaongea kishabiki tu wanafkiri kufika Mlimani ni lelemama' Angalia ni watu wangapi wenye heshima duniani wanakuja na wanazidi kutaka kuja Mlimani, Thabo Mbekhi alikuja, Samir Amir alikuja achilia mbali wasomi wa nchi nyingine ambao kila siku wanakuja pale kwa either joint programs na mambo kama hayo. Wanakiamini UDSM na wanajua tu sio historia ila pia na idadi ya machapisho inayofanywa na watu walioko pale.

Lakini pia kuna nduigu zetu wamesoma pale hawataki kurudi, kila wakitaka kuongea wanaenda UDOM, wanajua UDSM ina utamaduni wake ni chuo cha kimapinduzi kihistoria na na kinatoa watu makini na walimu wake wengi ni watu makini na wanaoheshimika sana duniani' Na kama hawajui sidhani kama Dr. Asha Rose Migiro ana opinion sawa na wewe juu ya UDSM. Na kila siku anasema anatamani kurudi pale.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba UDSM si pahala pa vilaza, Watu makini wanapapenda na kila siku wanataka kurudi ili kuleta mawazo makini, ila vilaza na wababaishaji hawataki kuja wala kurudi maana si pahala pao pale'

UDSM is the best in the country na kwa kuangalia watu wengi waliopo pale najua itabaki kuwa hivyo, yatachoka majengo ila mawazo imara na utamaduni wa chuo kile utabaki imara pia!!

Kaka nimesoma UD lakini kwa sasa sipafagilii kama enzi hizo za 1990's. Naona sijui ni ukali wa maisha walimu wengi wamejitosa kwenye Consultancy zaidi na kuacha kufundisha. Watoto wamekuwa wanakalia masesa tu vitabu hawasomi. Naona chuo changu UD kinaenda kupoteza umakini wake na kupitwa na chuo kama Mzumbe. Vijana waliokuwa vipange enzi zetu tumaliza form six chaguo lilikuwa twende UD lakini kwa sasa naona vipanga wanaenda Mzumbe. Kuna kijana wa jirani yangu alimaliza form six mwaka juzi ana Division one ya point 4 kakataa kwenda UD kaenda Mzumbe, kumuuliza dogo imekuwaje anasema hapafagilii watu ni wengi madarasani ufundishaji emebaki kukomaa na madesa. Najiuliza kwa nini wachukuwe wanafunzi wengi kiasi hicho wakati vitendea kazi ni vichache? Madarasani vijana wanakaa wanapumliana kwenye shingo tu unatokwa jasho utafikili hauko darasani.

Nikaabatika kupata elimu ya wenzetu waliondelea nikaona ni kweli wanastahili kuitwa watu wa ulimwengu wa kwanza, upo darasani unafeel kweli unasoma, hakuna mwalimu mwenye degree ya pili /Masters anaruhusiwa kufundisha hata kutoa semina elekezi kwa watoto wa degree ya kwanza, lazima uwe na PhD na umeshapata uzoefu kwa mda. Sasa leo hii Chuo changu UDSM vijana wanamailiza degree ya pili bila uzoefu waliunga toka ya kwanza wengine wanapewa na vipindi kufundisha. Mapinduzu makubwa yanahitajika katika chuo mama UD Ili heshima iweze kurudi. Mwishoe chuo kinaweza kupitwa na vyuo vya CBE, IFM na Tumaini kama mabadiliko ya makusudi yasipofanyika.
 
Mbona kama Nancy umesema kitu hakijakamilika. Ni kweli kuna matatizo mengi sana UDSM.. Ila dawa sio kukimbia matatizo. Ni kuyarekebisha. Kwa bahati mbaya unasema ubaya wa UDSM kwa kuangalia majadiliano ya JF. Una uhakika watu wote waliomo humu ndani wamesoma UDSM?Siyo mchezo
 
Back
Top Bottom