Namshauri Nape aache visasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namshauri Nape aache visasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mhoja, Apr 28, 2011.

 1. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana JF, nimemsikia jioni hii BBC Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Bw. Nape kuhusu kujivua gamba. Ila kwa matamshi anayoyatoa ya kumchafua Ndg. Edward Lowasa siyo ya kiungwana wala kianaume, kwa sababu mi naamini wanaume kama kuna matatizo huwa wanakaa na kuongea na kuyamaliza au kutoyamaliza na kuchua hatua. Kwa habari za maamuzi ya NEC kama waliazimia kuwatosa watuhumiwa wa ufisadi ni jambo jema, kinachotakiwa ni kutekeleza maamuzi ya kikao na siyo kila siku bwana mdogo amekuwa akiongea majukwaani jambo hilo hilo badala ya kulitekeleza na kupeleka taarifa kwenye vikao vilivyoagiza kama watuhumiwa wamepima wenyewe au wamekataa. Ugonvwi wake na Lowasa wakati alitaka kugombea uenyekiti wa UVCCM asitumie jukwaa alilopewa kumharibu kisakiolojia adui yake, maandiko yanasema mpende adui yako. Mimi naheshimu sana maamuzi ya NEC ila kinachonishangaza ni uropokaji wa kila siku wa katibu mwenyezi mpaka inakera. Kwa sababu kuna ugumu gani kama barua anasema zimeandikwa lakini mpaka leo bado hawajapewa, ina maana Ofisi ya CCM inakosa mesenja wa kuzipeleka kwa dispatch au kwa EMS? Cha kushangaza kiongozi aliyebaki kuropoka majukwaani ni Nape peke yake, kwa nini wengine wote wapo kimya? Labda kama hayo anayoyaongea awe ametumwa, lakini kama atakuwa ametumwa ajue kuwa waliomtuma watapita kama wengine walivyopita, na anaweza kuja kuhangaika sana baadaye.
  Ninachomuomba barua watuhumiwa wapewe kwa mujibu wa taratibu wa kufikisha barua, kama watazijibu, watakaa kimya au lolote watakalolifanya apeleke taarifa kwenye vikao na siyo kila siku kutoa taarifa zingine za chama ambazo hazina maana kwa watanzania.
   
 2. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Visasi....!

  Hakuna kisasi kwa muharifu. Lugha ya visasi ilitumiwa wakati Kikwete anatafuta Urais, eti kuna watu walionyesha kumuogopa kwa visasi vyake. Lakini kama kweli wewe ni mwizi, tukufute kwa mtindo gani? Au tuendelee kusema ni ajali ya kisiasa wakati tuna hakika kabisa kwamba wewe ni fisadi. Hakuna Kisasi. Hiyo ni haki yao kwa ushetani wao.

  Ktk CCM kunaweza kuwa na malengo meeengi kwa maamuzi yale yale! Siamini kama Kujivua gamba kuna lengo moja kati ya Nape na Kikwete na wengineo.
  Tusimuhukumu Nape. Kama kweli Barua ni kwenda kwa Lowasa, Chenge na RA basi ni lazima aitumie nafasi ya uenezi vizuri. Lazima watu wanaomuhusudu Lowasa waandaliwe kwa taarifa kama hizo za Nape

  Hawa, ki-historia ni 'wahalifu sugu' bahati mbaya kabisa wana wafuasi wasiotaka kuona ukweli. Wao binafsi hawako tayari kuikubali hasara inayotokana na vitendo vyao. Taarifa zinaonyesha kwamba Lowasa na wafuasi wake bado haamini kama hataweza kuwa Rais wa nchi hii. Ni kwa gharama yoyote na akikosa basi anasema tukose wote. CCM wakimwaga mboga, naye atamwaga ugali, wote tufe kwa njaa.

  Anachohangaikia ni umaarufu wake urudi. Ataanzisha vituo vya redio na hata TV ili aanze kujisifu kwa vyombo vyake.

  Hawa wote waache wapate matusi yote yanayowezekana ili wapate elimu ya matendo yao na iwe elimu kwa wengine.
   
 3. m

  makaomakuu Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna visasi hapo.muacheni nape afanye kazi yake.
  Huyo kijana ni mjasiri sana.kama unataka kujua nape ni mjasiri kwa kiasi gani ..leo hii nenda kamuulize jk,ni maneno gani nape alimwambia kipindi kile jk anaomba fursa ya kuiwakilisha ccm kwenye urais(kura za maoni ccm 2005).
   
 4. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Tatizo Nape hana ujasiri wa kuwataja hao mafisadi wanaotaka waondoke CCM maana hana uhakika wala ushahidi wa ufisadi bali anatumia hoja za watu wengine for cheap popularity, kama anajiamini na ana huakika kuna fisadi ndani CCM awataje japo mmoja basi.

  Hawezi kuondoa ufisadi mwa maneno ya propaganda.
   
 5. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Waache wafu wazikane! Yetu macho na mkono shavuni!
   
 6. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ok wakubwa nimewaelewa, nilikuwa nazungumzia ubinadamu zaidi kuwa kama mtu amekosa mwadhibu mara moja. Maadamu mmeeleza anachokifanya Nape siyo bisasi nami sina objection. Aendelee.
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Ule mkutano mliofanya pale Ubungo na hela mkapewa na mafisadi ndio matokeo yake ehe?
   
 8. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  mkuu haya mambo ni siri kubwa lakini kwa mwenye macho ahambiwi tazama, ccm walimkata NAPE , KWENYE UVCCM kama mwenyekiti, wakamtema kwenye ubunge kule ubungo,
  ghafla wamemleta kama katibu mwenezi kutoka huko MASASI,
  kwa wenye HEKIMA majibu ni haya
  MWENYEKITI WA CHAMA HANA UBAVU MBELE YA HAO RACHEL, WAO NDIO INGINI YA YEYE KUWA HAPO MAGOGONI, SASA BASI NANI WAKUWA JANITOR ?

  ndio hapo anatafutwa mtu hasiye na huruma na RACHEL, na ni NAPE hafanyi haya kwa masilahi ya taifa anafanya kujipoza nafsi yake maana hawa mmoja wao yaani EL ni adui binafsi kwake,
  wasiwasi angu ni pale atakapoliza hiyo kazi yake ya U-JANITOR kwa manufaa yake na mkuu wa kaya,
  huyu mimi namuweka kundi la ngiri anasahau mapema sana kifuatacho kwake kwenye mbio za kujiokoa na kukomoana.
  KWA NINI ANASHINDWA KUJIULIZA TWO BROTHERS kati ya mkuu wa kaya na EL ilikufa wapi?
   
 9. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nape hana lolote mafisadi hawafukuzwi kupitia majukwaaa kama vikao vilishaamua Nape anatakiwa atekeleze maazimio kama yeye ndiyo mtekelezaji sio kunanga akina Lowasa kila siku majukwaani huku akiwa hana ubavu wa kuwagusa wala kuwafikishia hizop barua. Hapo Nape analipiza tu visasi wala sio kwamba eti anafanya kazi. Kama kweli ccm inawaondoa mafisadi na kwa kuwa JK ni mhusika mkuu wa igizo kwa nini NEC haikuweka kaimu Mwenyekiti kabisa.
  Mana sote tunajua mapato ya kifisadi yamemsaidia JK kuwa rais na kama wanafukuzwa ni wote wanaenda, swali Je, nec ilishatangaza Kaimu Mwenyekiti wa chama??
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nape hajui anachokifanya...si ndiye huyu huyu aliyechakachua cheti cha kuzaliwa Ili mradi agombee UVCCM?
   
 11. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu tumia maneno rahisi maslahi binafsi
  vijana wengi walioko ccm wana stress kuliko wazee maana walijua
  watakua watawala lakini kwa jinsi watanzania walivyoa shituka sasa wana force king
  kuingia ikulu
   
 12. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nape na CCM yao wanafiki tu..anyway waache wafu wazike wafu wao!
   
 13. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa nyepesi zinazovuma Lumumba ni kuwa Msekwa anasita ile mbaya kuweka mkono kwenye hizo barua. Mukama alijitoa mapema kuwa yeye bado ni mpya, ni mtendaji tu, maamuzi ni Mwenyekiti au Makamu. Kazi sasa nani atamfuata Mwenyekiti kuweka mkono wake ili barua zitolewe.

  Mmojawapo katika RACHEL keshaipata draft copy ya hizo barua, anavuta tu pumzi kusubiri barua rasmi.

  Hii ngoma tamu sana.

  Pamoja na visasi na chuki Nape hawezi kuwataja RACHEL hana ubavu huo, na pia hasemi hizo siku 90 zinaanzia lini na zinaishia lini. Je, zilianza baada ya kikao cha NEC/CC, au zitaanza baada ya kupewa barua?
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,642
  Likes Received: 1,915
  Trophy Points: 280

  - Mkuu sana kwani kazi ya Katibu Mwenezi wa chama cha siasa ni nini hasa? Hebu weka wazi hilo kwanza halafu ndio utoe hukumu, Rais wa Jamhuri majuzi amesema wazi kwamba kila analolisema Nape ni lake yeye, sasa hebu tumpe nafasi Nape afanye kazi mpya aliyopewa na CCM, moja ya kazi zake mpya ni msemaji mkuu wa chama, kwa hiyo anapoongea ni chama kinaongea.

  - Mwacheni Nape, afanye kazi ya chama chake, maaana kama mantiki yako ni hoja basi ungeanza na Dr. Slaa kwanza, kwani hajamuona Mtikila, anavyowahi kwenye sheria akiwa na ushahidi? Pleaseeee!

  William @ NYC, USA.
   
 15. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapo sio Sawa hata kidogo..Nape hakuchakachua Umri wake kipindi cha kugombea uwenyekiti wa UVCCM taifa...waliochakachua ni wale walokuwa vingiozi wa kipindi hicho kwa kusogeza uchaguzi mbele ili kufanya baadhi ya watu kupoteza sifa za kugombea na kama wewe ni mfuatiriaji Mzuri utakumbuka siku ile ya uchaguzi ,mwenyekiti wa chama alipotoa hotuba ya kufungua mkutanoo mkuu wa chama alisema kuwa "Kama umri wa mtu umezidi hata kwa siku moja,basi mtu huyo hana sifa za kugombea ndani ya UVCCM"..wajumbe waliokuwepo mle wakajua tu hilo dogo linamuendea nape "direct" hasa ukikumbuka kuwa Nape alienguliwa kwa kigezo cha umri.
   
 16. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Ni ugomvi wa makundi ndani ya CCM. Usije shangaa wanaonekana wanashangilia muda huu,baada ya mwaka mmoja ndiyo watuhumiwa
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani toka lini JF ikiwa washabiki wa Lowassa au mimi ndio sijui?
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  tanzania yetu ya nyerere ilishakufa

  hii tanzania ya leo kama kenya hivi au nigeria hivi.....

  unbelievable
   
 19. S

  Songasonga Senior Member

  #19
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachojua Nape ni Katibu mwenezi moja ya kazi yake kuongea sasa we Mhoja hutaki aongee?waachie hoja zao CCM mbona Wanaotajwa hawasemi lolote? Mbona hujamsema Makongoro Nyerere? Au ?
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hapa Kikwete ametafuta pakuamishia lawama Nape na Msekwa! Kikwete ni Rafiki wa Lowasa kufa na kupona hawakukutana barabarani kama alivyosema Lowasa, Kinacho waumiza kichwa ni jinsi ya kuokoa CCM wao wameshauriwa na Msomali mmoja kuwa kuwafukuza hao itaipa CCM credit kubwa na kuifufuwa! sijui kama ni kweli au la!

  Ujinga waliofanya na ambao CCM wamesahau ni kuwa staili wanayotumia ni kama ile ya Kikwete kwa SAS 2005. Kama CCM walitaka na kama Kikwete amedhamiria kwa dhati hili swala kazi ingemalizwa kilaini kupitia Dola maana ndio wanaoshughulikia Mafisadi na ndio wana-sheria na kuzilinda, sasa iweje CCM iseme leo hao watu ni mafisadi wakati waliwai kukana hapo nyuma? Mbona Kikwete alitumia hadi vyombo vya Dola kuwasafisa hao watu leo watawashikia wapi? Kazi siyo rahisi hivyo maana wanapaswa pia kutwambia Ufisadi waliofanya! na itakuwaje iwapo hao watu hawata shughulikiwa na Dola labda hata walisha forgy na kupoteza ushahidi maana nijuavyo asilimia karibia 80 ya wachunguzi makini waliokuwa wanajua vyema mafaili ya EPA na Richmond wameshakufa hasa wale wa PCCB na Polisi?

  Hapa wanafanya mchezo mchafu hawashughulikii mafisadi nakataa, hapa wameanza kampeni za Urais hawa jamaa, kama ni Ufisadi tunataka kusikia NAPE yupo kimia, bali tunataka kusikia Kikwete, Pinda, Luhanjo, Rashid, Hoseah na Mwema ndio wanaongea na kutwambia mikakati na mipango dhidi ya Ufisadi wote uliowai kufanywa, hao ndio watutangazie majina ya watuhumiwa wa Ufisadi na lini wanafikishwa mahakamani siyo kelele za Nape.

  Hata hivyo kuna wakati nahisi baadhi ya wanachama wa CCM hawakumuelewa M/kiti wao! hasa aliposema wanavua gamba, maana nyoka akivua gamba bado anakuwa nyoka tu! yamkini anakuwa hatari kuliko awali!

  Ila yote hiyo ni kumsafishia njia Mwinyi mdogo ndani ya CCM kama itapona lakini maana ipo ICU
   
Loading...