Nampongeza Rais, tulisubiri ulianzishe....

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,084
2,000
Mimi VUTA-NKUVUTE alias Mzee Tupatupa, kada nguli wa CCM na 'Shushushu' mstaafu, nampongeza Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Dr. John Pombe Magufuli kwa anachokifanya sasa kuhusu madini. Nampongeza Rais kwa kuanzisha 'vita' hii ya kusaka haki yetu kama Taifa na kupata tunachostahili.

Mhe. Rais, nimekusikiliza vya kutosha bila kutisha. Nakupongeza hasa kwa kuliona tatizo linalozunguka mambo yote haya: ubovu wa Sheria zetu mbalimbali zinazosimamia madini. Hakuna haja ya kunyoosheana vidole kwa wale waliokuwa wakijadili tofautitofauti lakini kwa hoja moja ya ubovu wa sharia.

Mhe. Rais, kuhusu wahusika waliotajwa na Kamati Maalum ya Prof. Osoro leo, ulipaswa kuagiza kwa kutaja majina wahusika wa kuhojiwa. Wametajwa wengi kwenye Ripoti, kwa mazuri na mabaya. Wametajwa wasiotajika na watahojiwa wasiohojika. Madini ni yetu sote. Tutayalinda hadi tone la mwisho la damu yetu kama watanzania. Tulitaka Rais uanze.

Mhe. Rais, umefanya vyema kumkabidhi kazi ya kisheria Nguli wa Sheria, Prof. Kabudi. Yeye anawajua waliokuwa wanafunzi wake bora, imara, waaminifu na walinda maslahi ya nchi. Anawajua waliopo Serikalini na wale walio sekta binafsi. Anawajua waliopo chamani-CCM na wale waliopo upinzani. Kwakuwa hili sasa ni jambo la kitaifa, atawachagua kutoka popote.

Kuwa na 'neutral pool' ya Wanasheria wazalendo ni jambo kubwa na la kupongezwa. Ulinzi wa nchi kiuchumi upo kwenye sheria. Mhe. Rais, ulipaswa kuwataja wakuhojiwa waziwazi: Chenge, Yona, Salula, Mwanyika, Kafumu na kadhalika. Kwakuwa wote ni wanaCCM, nakushauri uwashughulikie pia kichama ili 'kukisafisha' chama.


Tutalinda mali zetu, tulisubiri Rais alianzishe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 

vicdala55

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
945
1,000
Aisee kwa hili hata mimi nampongeza ila shida moja tu bado anaona wanaopiga kelele bungeni na kupewa adhabu na kina Ndugai ndio wakosaji wakati wakosaji ni hao wa chama chake na ndio walio tufikisha hapa
Hapa ndipo ninashawishika kuona anafanya maigizo! Yaani waliokuwa wanahoji hii mikataba ndo anataka watolewe nje ya bunge? Kwa hili rais anapaswa afute kauli!
 

denoo49

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
6,109
2,000
Mwenge wa Uhuru na Nguo za Chama Cha Makanika, ndio wachawi wakuu wa hili taifa. Mbinuke, Mlale, mruke, hili hizo nguo hazitoliacha Taifa salama.
Kama Mwalimu alizishtukia ninyi mnamapenzi gani kuliko mwalimu.?
 

ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
2,507
2,000
Nisaidieni kumwelewa Rais wangu jamani; Sheria irudishwe bungeni ijadiliwe upya na wale walioupitisha alafu watolewe nje wale waliokua wanaitaji irudishwe waijadili upwa.

Au Mimi ndo sijaelewa hapa; uTaifa wetu umepotelea wapi?
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,347
2,000
sasa hao wenye dhamana ya kuhoji waende fyongo waone! hapo wamepewa mtego ukicheza vibaya unakula red card unaenda kusubiri kupangiwa kazi nyingine
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
42,827
2,000
Siku mikataba inasainiwa ulimpongeza hivi hivi Rais aliyekuwepo wakati ule. Shame on you
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
42,827
2,000
Nisaidieni kumwelewa Rais wangu jamani; Sheria irudishwe bungeni ijadiliwe upya na wale walioupitisha alafu watolewe nje wale waliokua wanaitaji irudishwe waijadili upwa.

Au Mimi ndo sijaelewa hapa; uTaifa wetu umepotelea wapi?
Huyu mzee huwezi kumwelewa hata siku moja, kama anakashifu viongozi wa dini sembuse wanasiasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom