Nampenda sana Sky Eclat

DEFAMATION

Senior Member
Jun 19, 2017
110
69
Asalaam aleykum wana JF. Poleni na majukumu ya hapa na pale ya kutafuta riziki.

Lengo kubwa la kuleta huu Uzi mbele yenu ni kwamba nimetokea kumpenda sana huyu mdada SKY ECLAT. Umekuwa ukinitokea ndotoni mara nyingi sana nimevumilia nimeshindwa.

Ndotoni nimekuwa nikikuona mrembo uliyejaaliwa hivi vitu;
•mrembo uliyeenda hewani.

•mwenye umbo namba nane na msambwandwa wa kubinuka.

• Rangi ya chocolate( Rangi ya pesa)

• Una guu la champaign.

•Una mashimo mashavuni hata usipocheka yanaonekana.


•Midomo yako mizuri.

Nampenda na nina hisia kali sana juu yake. Napenda sana siku moja ndoto yangu itimie yani tuwe kitu kimoja( mume na mke) tujenge familia iliyo imara.

Sky Eclat naomba unielewe mdada kwa upendo million nilio nao juu yako.kila nikiona bandiko au hata comment yako kiukweli huwa napata faraja ya moyo asilimia 45℅.

Hivyo ili nipate faraja na amani ya moyo kwa asilimia zote mia inabidi hizo asilimia 55% uzikamilishe kwa kunipenda Kama navyofanya kwa upande wangu.

Nakupenda sana sky Eclat. Nina mengi ya kueleza juu yako ingawa maandishi hayatoshi kueleza Upendo wangu kwako isipokuwa tu moyo wangu.

Naomba kama hautojali nije PM tuyajenge mtoto mzuri Sky Eclat!
 
Back
Top Bottom