Nampenda sana ila simuelewi

Nampenda sana ila simuelewi

Mwananchi B

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
2,050
Reaction score
4,602
Ni mwanamke ninaempenda sana namuamini pia nimempa kila kitu ili asione najificha kwa chochote nyuma ya pazia, kama nywila zote isipokuwa za ATMs, namjali sana, kila mda lazima nijue anaendeleaje kwa njia yoyote ile, nampa kila kitu anachohitaji hata kama mda mwingine ni cha kipuuzi, kiufupi namthamini sana kama mtu wa muhimu sana kwangu.

Nimeanza nae mahusiano mda sasa yapata miaka miwili, tupo nae mbali kidogo yaani mikoa tofauti, ila huwa twakutana baada ya mda fulani, na yale mambo nipo kawaida tu, lakini tatizo ni kwamba ni Kama hatambui uwepo wangu, napokosea kidogo tu hata ambapo kosa si langu inakuwa ni shida ni kama mda mwingi nakuwa napimwa Kwa vimaswali vya ajabu ajabu, sasa kimbembe niteleze ulimi au kidole basi itakuwa balaa.

Mda mwingine nikiangalia hata wastani wa ujumbe mfupi ninaotuma na anaonitumia ni hauna uhusiano ni kama ndani ya jumbe 10, basi mbili ndio zake, pia kuna mda tunaongea katika simu yeye anaongea na wengine wa pembeni yake tena anarudi kwangu, nikimwambia basi ni kununiana, nami nikifanya hivyo basi ndio kimbembe, mara oooh hunijali, mara oooh una visichana vyako huko, balaa apige akute simu bize ni balaa, utaulizwa maswali 700, haniamini, sasa sijui tatizo ni nini?

Au nampenda sana? nipunguze mapenzi kwake? Hivi kumpenda sana ni tatizo maana nasikia ukimpenda sana mwanamke anakuona kanya boya? Au nimuache tu? Maana mda mwingine nahisi hanipendi, labda mie ndio napenda sana, kinachoniuma zaidi mda napokosea kidogo ananifananisha na jamaa yake wa zamani ambae hakuwa mwaminifu, na mie sina ujinga huo, huwa natamani kumwambia aniache.

Ila nikikaa hasira zaisha naendelea nae, kiukweli sipendi kabisa kusingiziwa kitu pia sipendi wala kusikia michepuko nayathamini mahusiano yangu na huyu mbidada. Tena kuna mda tukiwa fresh twapiga stori anamsifia, yaani ni kama uwepo wangu kwake ni mdogo sana. Imekaaje hii wakuu?

Nawasilisha
 
Mwananchi B

Mkuu mimi ni ke!
Ila naomba nikwambie hapo umeiingia miguu yote miwili na amekugundua! Hayuko na feeling na wewe ila kama binti kuonesha ana mtu na coz unaonekana una mpenda ndo maana yuko hapo!

1. punguza mawasiliano kama kweli anakupenda atakutafuta (kama sms zilikuwa 10 peleka 5 kisha 1) hapa utaumia ila baadae utazoea

2. Punguza matunzo fanya pale anapoomba na siyo lazima kila akiomba utimize (kama yeye kakosa hata wewe unaweza kukosa pia )
Utapata shida mwanzoni lakn ni namna nzur ya kujua position yako kwake! Unaweza ukute kakufanya wa back up tu!!!
 
Last edited by a moderator:
Madem wanapenda attention, they live for that. Ila ukiwapa yote they don't know how to act, so they start frontin. Fanya kama unapunguza kumjali hivi, halafu angalia ana-act vipi.
 
utakuja kulia sana siku za mbele maana una kila dalili za uteja kwake. Jitahidi ujinasue.
 
Wewe ndio tatizo. Kuna mahali huwa naona humu watu wanasema imeandikwa hawa viumbe inatakiwa uishi nao kwa akili, hawakukosea kabisa. Ni hivi hapo kuna mawili.
  1. Huyo mdada anakufanya we mchepuko, hakupendi hata nukta.
  2. Ni aina ya wale wasichana ambao wanaamini mwanaume anatakiwa kuwa mbabe na mkali hivyo wakipata watu wanaojali sana wanajikuta tu wanakuwa wakorofi maana hawapati kile wanachotaka. Ninaamini kwa kiasi kikubwa hiki ndicho kinachotokea kwa upande wako. Dawa ya hili tatizo huwa ni ndogo sana, unachotakiwa ni kufanya kama vile hayupo. Mpotezee hivi kidogo, saa nyingine mwambie nakuja kukutembelea halafu usitokee bila taarifa akikuuliza mwambie ulibanwa na majukumu. Halafu akiwa mkali we kuwa mkali mara 100 halafu cheki situation. Kumbuka Sio kila mwanamke anaelewa lugha ya upole.
Ni hayo tu kwa sasa.
 
Poleh sn, usimuache we fanya km ulivyoelekezwa na watu huku kuwa punguza too much caring na vngne, uone atareact vip, je atasononeka, atahoji au ataendelea tu na mambo yake!?
 
Yeye hakupendi halafu nawewe unampenda na pia Unamwogopa,Mwanaume hupaswi kuwa hivyo na hapo ukweli ni kwamba kaonesha ishara zote za kutokukujali wewe na atakuwa na mtu mwingine huyo. Achana naye kwani atakutesa sana halafu pia utapoteza muda mwingi ambao ungeweza kuutumia kuanzisha mahusiano kwa mwingine.
 
Poleh sn, usimuache we fanya km ulivyoelekezwa na watu huku kuwa punguza too much caring na vngne, uone atareact vip, je atasononeka, atahoji au ataendelea tu na mambo yake!?

Shaanza kulifanyia kazi
 
sasa hapa unataka ushauriwe nini......kila kitu kiko wazi au mpaka autoboe moyo wako...potezea wako wengine wanaothamini kupendwa....au ndio unajifunza kupenda
 
sasa hapa unataka ushauriwe nini......kila kitu kiko wazi au mpaka autoboe moyo wako...potezea wako wengine wanaothamini kupendwa....au ndio unajifunza kupenda

Hapana mkuu
 
sasa hapa unataka ushauriwe nini......kila kitu kiko wazi au mpaka autoboe moyo wako...potezea wako wengine wanaothamini kupendwa....au ndio unajifunza kupenda
 
Ulishamkosea mwanzoni mkuu....amsha popo disko lishaingia masai....
 
Mie nakushauri anzisha urafiki na binti mwingine ambaye unaridhika ukipiga naye story kama mpenzi.mtoe toe weekend zen atakusahaulisha yule.hawa mademu sio ws kuwapa moyo.yani unaongea naye afu anaongea pembeni na huku unachoma hela.kwanza unamkoromea sana kama amri ya kijeshi.anatakiwa akuogope
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom