Head teacher
JF-Expert Member
- Mar 10, 2012
- 1,796
- 413
Najuta kuolewa na mwanamume nisiye mpenda. Ni stori ndefu lakini kwa kifupi...nilikuwa na boyfriend wangu tuliyependana sana. Tulipanga kuoana na barua ya posa alishaleta kwetu. mchumba wangu muda huo alikuwa anasoma chuo kikuu na mimi nilikuwa form six. Baadae nilisikia kuwa mchumba wangu ana mahusiano na binti mmoja ambapo baadae ikasemekana alimpa mimba na kisha kuzaa mtoto wa kiume. Nilipo muuliza alikana kutembea na mwanamke huyo na alikataa kuwa mtoto si wake. Lakini kadiri siku zilivyoenda palionekana kila dalili kuwa mtoto ni wake kwani walifanana sana. Kwa hasira nikaamua kumwacha nami nikatafuta mwanamume nizae naye kulipiza kisasi. Ingawa ulikuwa uamuzi mgumu kwangu nikazaa na mvulana mmoja ambaye kusema ukweli sikumpenda kama mchumba wangu. Nikiwa mjamzito yule mchumba wangu aliniomba tuendelee na mahusiano kwa lengo lile lile la kuoana. Mchumba angu hakujali sana kile kitendo cha kupata mimba. Na tuliendelea uhusiano wetu kama kawaida ila safari hii nikiwa na waume wawili tena wanaofahamiana.
Mwanamume huyu wa sasa kwa kuhofia kunyang'anywa mke alipeleka barua fasta kwa wazazi na taratibu za kufunga ndoa zilianza mara. Mpaka sasa nimefunga ndoa kanisani na mwanamume huyu nisiyempenda na nina watoto wawili. Mchumba angu aliamua kumuoa yule mwanamke na amezaa naye jumla ya watoto watatu ila hajafunga ndoa akidai ananisubiri mimi niamue lini tutaoana, huku akijua nimefunga ndoa. Kwani naye anasema hampendi mwanamke anayeishi naye. Kwa upande mwingine wazazi na ndugu wa mchumba wangu hawampendi mke wake , wakati wazazi na ndugu zangu hawampendi mume wangu. Hivyo nipo dilema. Lakini ukweli ni kwamba mimi ninampenda zaidi sana mchumba wangu wa zamani na hapa nilipo nina mimba yake na ninatarajia kujifungua hivi punde. Natarajia baada ya kujifungua nianze ukurasa mpya na man of my dream........ Kama kuna ushauri wowote nitashkuru sana