Wakuu Habari za muda huu, niende moja kwa moja kwenye mada.
Hii inanihusu Mimi mwenyewe na hapa Nawaza na kuwazua na sipati jibu sahihi, Nachanganyikiwa.
Mimi Ni kijana mwenye miaka 26, Elimu yangu Ni kidato Cha Sita na pia nilisoma Certificate in Clearing and Forwarding, Naishi Dar kwa Wazazi Ila nakaa chumba Cha nje Cha Peke angu,
Kwa muda Sasa nilikua nikitamani kuwa na familia, Yani mke na mtoto, ukizingatia rafiki zangu karibu wengi Wana maisha Yao na familia zao, niliwahi kuajiriwa lakini kwa Sasa Sina Kazi ya uhakika nadandia tu mishe yeyote itakayokuja mbele yangu.
Sasa Kuna huyu binti, mtoto wa Kanda ya ziwa, mzuri, binti mdogo miaka 20(Asomi) alikua akifanya Kazi za usaidizi za ndani, Muuni nikamuelewa nikaanzisha mahusiano nae, baada ya miezi kadhaa mwajiri wake akayumba Kiuchumi na kumuachisha Kazi.
Binti Hana ndugu mjini, kwao Ni mbali na maisha ya kwao pia wanamuangalia yeye ndio mwokozi wao, Kimsingi binti ananipenda na Mimi pia Nampenda na ndio msichana ninaetamani kuishi nae na kutengeneza familia.
Tatizo linakuja hapa, Mimi Jobless, kula kwa kengele japo sio kila siku kwasababu nikiwa na mishe zangu napenda kujitegemea kuliko kusumbua home, huyu mtoto wa watu nataka kumsaidia, nataka asiwe mbali na Mimi kusudi Mambo yangu yaki tiki niishi nae.
Kwa Sasa nimemuombea hifadhi kwa Dada yangu japo ya siku kadhaa na tayari Nina siku tano tu mbele za kujua hatma yake.
Nawaza nifanye Nini?? Nimtafutie nauli arudi kwao?? Nikae nae kibishi, atakula Nini? Ana mahitaji mtoto wa kike na Mimi Ni hohe have?? Naomba ushauri wakuu.
Natanguliza Shukrani.