Nampenda lakini simwamini kabisa, nifanyeje?

Hony

New Member
Dec 18, 2021
2
22
Naombeni ushauri,

Mimi ni msichana wa miaka 24, nina mchumba ana miaka 29, tatizo langu ni kwamba mchumba wangu nimekuja kugundua ni muongo sana na mpaka kumgundua uwe na akili ya ziada kabisa, nimekuja kumgundua nimeshampenda tayr, na nisingekuwa nakaa naye pamoja hakika nisingemkamata, alinidanganya ana nyumba akanionyesha kabisa kumbe sio yake, akanidangany hakuwahi kuwa na mpenzi kumbe ana wapenzi wengi t, kanidangany mpaka level yake ya elimu n.k,

Siku yaliponkfika shingoni nikamwambia ukweli na nikamuaga naenda sehemu nikapitie vitu vyangu kisha nielekee nyumbani nikawasalimie, kiukweli nisiwe mnafiki nilikuwa nasepa mazima. Alikubali lkn imefika usiku wa kuamkia siku ambayo naondoka akanibadilikia na tulikuwa tunacheka kabisa, ghafla akaanza kucheka akanishikia kisu usoni akabadilika kabisa lkn anacheka sana, aliniwekea tumboni akasema bora aniue tu maana ananipenda lkn nataka niache Dah kiukweli nilijitetea mpk nilichanganyikiwa, hatimaye baada ya masaa takriban mawili aliniacha akasema nikirudia atanimaliza kabisa.

Siku moja kanikuta na simu nipo instagram naangalia comments nikawa nacheka lkn limekuwa ni tatizo kwake (hili ni la muda mrefu hataki nishike simu, hajawahi kunikuta naongea na mwanaume wala kunasa msg na yeye anajua sina hiyo tabia, nikishika simu nafanya application za kazi nikichoka naingia kujiburudisha mtandaoni sasa kinamuuma sana mm kufanya hivo), hiyo siku akaanza kunigombeza, kwa kuwa ni tabia yake siku hiyo nikamwambia laivu nimechoka na hii tabia, ghafla kaanz kunipiga anasema ko imechoka kuishi na mimi, akaniumiza sana akaona haitoshi kakimbilia kisu dah! Nilipiga kelele watu wakaja ndio akaniachia.

Asubuhi kulipokicha akanifata nilipolala akaanza kulia sana ananiomba msamaha, alijutia alichokifanya mpk leo namuona hayupo sawa, nilimwambia nimemsamehe lakini aliendelea kulia baadae akanyamaz lkn anajuta hadi leo. Tangu siku anipige na kunishikia kisu namuogopa sana, simwamini tena nikimuona nawaza kuna siku ataniua, tunaweza kuwa tunacheka kabisa ghafla hali ya hofu inanitawala, nabadilika kabisa mpaka anaanza kulia tena, hio hali inanisumbua sana, akinikumbatia nakuwa na furaha ghafla tena nashikwa hofu hapohapo,namwambia aniachie, akiniletea zawadi ananiambia fumba macho ili anipe, nafumba ghafla naanza kupiga kelele nafumbua macho!

Dah of course inamuuma sana akiniona na hali hiyo lkn akili yangu najaribu kuirudisha upya imegoma kabisa, nawaza kutoroka tuu muda wowote na inaniuma kuondoka bila kumuaga nifanye je?nisaidiwe nn cha kufanya? Halafu amenihofia je nikitoroka akaninasa njian? Maana ananiwinda sana. Nampenda lakini nipo tayr kujisacrify kumuacha, nitumie njia ipi?
 
Naombeni ushauri, Mm ni msichana wa miaka 24, nina mchumba ana miaka 29, tatizo langu ni kwamba mchumba wangu nimekuja kugundua ni muongo sana na mpaka kumgundua uwe na akili ya ziada kabisa, nimekuja kumgundua nimeshampenda tayr, na nisingekuwa nakaa naye pamoja hakika nisingemkamata, alinidanganya ana nyumba akanionyesha kabisa kumbe sio yake, akanidangany hakuwahi kuwa na mpenzi kumbe ana
Najua we ni mgeni hapa, huenda mwanzo ulikua kama msomaji tu,ukaona ujiunge rasmi ili uombe ushauri, hivyo nawaomba Wana Jf wasikulaumu kutokana na uandishi wako, ispokua wakushauri juu ya matatizo yanayo kukabili.

Hapo ukiendelea kukaa utakua na tatizo la kisaikolojia, yaani mara nyingi utakua unajawa na hofu, hata presha inaweza kukushika kutokana na matendo ya huyo mtu wako.

Pia anaweza kukudhuru, kuna hisia na uhalisia, kihisia unaona bado unampenda, ila kiuhalisia ni lazma umuache uende zako kwa faida ya furaha ya maisha yako na amani ya kweli, hutakaa ufurahie hayo maisha, tena ukisha mzalia ndo kabisa utakua umefunga pingu na matatizo.

Lakufanya: Ondoka bila kumtaarifu, kisha ukishafika kwenu mtumie ujumbe kua wazazi wako wamekuja kukuchukua hivyo asihangaike kukutafuta aendelee na maisha yake, vunja line, badili namba, baada ya mda utarudi na kuimarika tena.
 
Naombeni ushauri, Mm ni msichana wa miaka 24, nina mchumba ana miaka 29, tatizo langu ni kwamba mchumba wangu nimekuja kugundua ni muongo sana na mpaka kumgundua uwe na akili ya ziada kabisa, nimekuja kumgundua nimeshampenda tayr, na nisingekuwa nakaa naye pamoja hakika nisingemkamata, alinidanganya ana nyumba akanionyesha kabisa kumbe sio yake, akanidangany hakuwahi kuwa na mpenzi kumbe ana wa kumuaga nifanye je?nisaidiwe nn cha kufanya? Halafu amenihofia je nikitoroka akaninasa njian? Maana ananiwinda sana. Nampenda lakini nipo tayr kujisacrify kumuacha, nitumie njia ipi?
Tatizo la wasichana wengi hamna ga waamuzi katika mapezi yenu, wewe hapo umenogewa hata, ukiondoka baada ya mwezi utarudi tu, wewe subiri akuue sie tutakulifadhi kwa kutaipu RIP .......
 
We unachongoja hapo ni kufa, endelea kungoja siku anapoamua kukumaliza maana umeamua kua mjinga, umempenda muaaji na atakupa hiyo zawadi na akikupunja atakupa kilema cha maisha, acha upumbavu, acha ujinga au fuata moyo wako kipofu mpaka utakapolala kaburini
 
Tatizo la wasichana wengi hamna ga waamuzi katika mapezi yenu, wewe hapo umenogewa hata, ukiondoka baada ya mwezi utarudi tu, wewe subiri akuue sie tutakulifadhi kwa kutaipu RIP .......
Nami namuona akirudi baada ya kuondoka!
Nashauri awasimulie wazazi wake visa na mikasa yake na 'mmewe' ili hata akirudi nyumbani wazazi wasaidie kumuonya kujirudisha kwa mzee wa visu!
 
Jaribu kuangalia mambo yenye tija, kama familia, uchumi wako na muhimu kuliko yote, peace of mind. Mapenzi hayana umuhimu sana hasa ukiwa na mtu ambaye ni chenga. Na kwa mlivyoanza mwisho wake siyo mzuri.
Miaka 24 bado una mengi sana ya kujifunza kwenye maisha, pole sana. Na uache kujipa mizigo mizito iliyo nje ya uwezo wako.
 
Kupitia haya maelezo yako; unatakiwa kuchagua mambo mawili tu!

La kwanza ni kuondoka kwa huyo mpuuzi wako unaye muendekeza, ili uishi maisha marefu hapa duniani!

Au uendelee kubakia naye hapo mnapoishi kienyeji, ili ndani ya miaka michache tu kuanzia sasa akuue na hivyo kwenda kuishia kuliwa na finyi kaburini.

NB: ogopa kuishi na mtu wa aina hiyo katika maisha yako yote kuanzia sasa. Maana mapenzi hayako hivyo mdogo wangu. Sisi wakubwa zako mpaka leo tunadunda, ni kwa sababu hatukuwahi kuwa na wapenzi wa aina hiyo. Usiendelee kuishi na mwendawazimu! Atakuua.
 
Back
Top Bottom