Nampenda lakini simuelewi kwa tabia zake

Jay_the_analyst

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
206
151
Za asubuhi ndugu zangu..

Natumaini mmeamka salama.

Ndugu zangu, dhumuni la kuleta uzi huu hapa jamvini ni kuomba msaada
hali ya mahusiano yangu imefikia pabaya.

Na sijui nafanyaje mpenzi wangu huyu amekuwa ni mtu wa visirani visivyo isha na majibu machafu hata kwa kosa dogo nilijaribu kumuonya kwa miaka miwili sasa tuliyokuwa kwenye mahusiano lakini hajirekebishi.

Kama binadamu wengine kuna makosa madogo madogo kama kuchelewa kufika eneo fulanu kutokana na kubanwa na shughuli na vingine vingi. Ila ninachoshindwa kumwelewa huwa ananijibu hovyo alafu anakimbilia kuachana kuliko kawaida kosa dogo amekimbilia kuachana sio mtu wa kusamehe anabeba visasi mno ukumkosea leo anakumbushia na ya zamani nimemvumilia lakini sasa nachoka nimesha jaribu kuongea na mzazi wake dada zake waongee nae.

Ata pretend wiki moja yuko sawa lakini baada ya hapo anarudia tabia zake nikijichunguza mimi sina kosa sijawahi hata kumsaliti nimekuwa mwanifu kwake lakini yeye hataki kuelewa kiburu kimemjaa nimemsaidia mambo mengi kwenye maisha yake, haswa kutokana na hana kazi ya kueleweka lakini naona juhudi zangu hatambui.

Akitishia kuachana nikikubali kukaa kimya baada ya wiki ananitafuta anaomba msamaha ("huwa anadai kuwa anachanganyikiwa mpaka kufikia hiyo hali ya kuniacha alafu baadae ndio anashtukia kuwa amenikosea, anadai kuwa ananipenda").

Naombeni ushauri ndugu zangu, nifanyaje?
 
Ndugu yakupasa kujua hayo maneno ya visasi yasiyoisha na kupenda kukumbusha yaliyopita HUYO NDIVYO ALIVYO na kumbadilisha ni taratibu mno unless atambue ni nini anafanya katika mahusiano yenu.

Maisha ya mahusiano ni changamoto kubwa hasa pale mchango wako ukiwa hauthaminiwi lakini huwa inauma sana pale unapojitoa kwa mtu ambaye umuhimu wako hauoni ila wewe unahitaji afanye vivyo hivyo ingawa sometimes ni vizuri kama girl/boy friend kumsadia mwenzake ili kuimarisha mahusiano.

Piga moyo konde kama utabeba hayo mapungufu ya mwenzako tho visasi na maneno mengi yasiyo na msingi si dalili ya health relationship Kwa mtazamo wangu hayo yote ni ndivyo alivyo, jaribu kwenda kiroho zaidi omba Mungu ambadilishe na wewe mweke Mungu mbele sio unaendaesha mahusiano yako kwa akili zako. Sali na mweleze mwenzako ili mjenge ndoa iliyo bora baadae.
 
Wewe ndo unamjua na ushamvumilia kwa kiasi gani and how far you can go...Fuata vile moyo unataka.

Otherwise,there is a lot of fish in the sea..
Every time niki move on... yeye hutokea na kuomba misamaha kibao na kuahidi kujirekebisha.. but then hurudia matope tena. ni mtuanajielewa.. nilisha muonya na akasema hii hali hata yeye haipendi...
lakin hii sitaki nataka yake ndio inanichosha
 
Je moyo wako uko tayari kusema basi kwake? kama umeshajaribu kumsaidia na kumuelewesha kua hupendi tabia hiyo
how long utakua ukichukua machungu na kauli zisizofaa,au moyo wako unaweza kuhimili kiasi gani? mapenzi nikupenda kusaidia kuelewana nakuliwazana,sio kutiana stress,unahitaji amani ili ufanye shughuli zako za kawaida,sasa ikiwa kila leo una tafran mara hili mara lile huyo mwanamke au Stress Dume?...
Mpe nafasi ya mwisho ongea nae ukiwa serious kua moyo wako hautochukua tena tabia yake mbovu kama hatobadilika itakulazimu ujipange kua nae yeye isiwe ndio sababu yakukutia maradhi ya wasi wasi na kukurejesha nyuma kwenye maisha,na wewe mwenyewe pia nilazima ujiulize jee nilipata mpenzi au msugua ROHO? na ukisema basi iwe basi ya kiume sio ya staki nataka...
 
Za asubuhi ndugu zangu..
Natumain mumeamka salama.
Ndugu zangu dhumuni la kuleta uzi huu hapa jamvini ni kuomba msaada
Hali ya mahusiano yangu imefikia pabaya.

Na sijui nafanyaje Mpenz wangu huyu amekuwa ni mtu wa visirani visivyo isha na majibu machafu hata kwa kosa dogo nilijaribu kumuonya kwa miaka miwili sasa tuliyokuwa kwenye mahusiano lakin hajirekebishi.

Kama binadamu wengine kuna makosa madogo madogo kama kuchelewa kufika eneo fulanu kutokana na kubanwa na shughuli Na vingine vingi. Ila ninachoshindwa kumwelewa huwa ananijibu hovyo alafu anakimbilia kuachana kuliko kawaida.

kosa dogo amekimbilia kuachana sio mtu wa kusamehe anabeba visasi mno ukumkosea leo anakumbushia na ya zamani nimemvumilia lakin sasa nachoka nimesha jaribu kuongea na mzazi wake dada zake waongee nae.

Ata pretend wiki moja yuko sawa lakini baada ya hapo anarudia tabia zake nikijichunguza mimi sina kosa sijawahi hata kumsaliti nimekuwa mwanifu kwake lakini yeye hataki kuelewa kiburu kimemjaa nimemsaidia mambo mengi kwenye maisha yake, haswa kutokana na hana kazi ya kueleweka lakin naona juhudi zangu hatambui.

Akitishia kuachana nikikubali kukaa kimya baada ya wiki ananitafuta anaomba msamaha ("huwa anadai kuwa anachanganyikiwa mpaka kufikia hiyo hali ya kuniacha alafU baadae ndio anashtukia kuwa amenikosea, anadai kuwa ananipenda").
Naombeni ushaur ndugu zangu... nifanyaje?
umempendaje mtuambaye humuelewi
 
Back
Top Bottom