Nampenda lakini simuelewi kwa tabia zake

Nampenda lakini simuelewi kwa tabia zake

haha si ndo zenyewe aisee ungeanza kuzielewa tabia zake ndipo mapendo yasike kasi wewe ulitamani kabla ya kupenda sasa inakutafuna
Mwanzoni hakuwa hivi... tulikuwa tunaelewana.. hata ndugu zake wananifaham.. upendo ulishamiri. Laki gafla akabadilika tabia... na tabia zenyewe ndio hizo.. ma anajitambua, anajua madudu anayofanya si mazuri... lakini kwa nini aendelee ? ina maana si makusudi kabisa hiyo
 
Kama dini yako inaruhusu kuowa mke zaidi ya mmoja ni vema ukaoa mke mwingine huyo anachokifanya kwako ni kudeka tu na wala sio kweli kama anataka muachane anatingisha kibeliti kuona kama kina njiti
 
nilisha muonya na akasema hii hali hata yeye haipendi...

Ndugu huyo ana psychological condition! Unaweza dhani anafanya makusudi lakini ndivyo alivyo. Wengine ni kutokana na alivyozaliwa (hormonal imbalance ama insanity) na wengine ni malezi.

Help her to seek medical care - see a psychiatrist - na uonane na daktari pia akueleze kama her condition can improve with treatment ama ni permanent then you can make an informed decision.

Niliwahi kusoma article about that nikiikumbuka I will update this comment. Usichukulie easy mkuu msaidie apate msaada wa kiafya.


huwa anadai kuwa anachanganyikiwa mpaka kufikia hiyo hali ya kuniacha alafU baadae ndio anashtukia kuwa amenikosea,

Halafu unavyoendelea kukaa naye na wewe utadevelop tatizo linaitwa, Stockholm Syndrome (Love and Stockholm Syndrome). Utafika mahali hata ukiachana naye utajikuta unatamka maneno kama, "Siamini alikuwa ananitendea vile lakini bado nampenda/nammiss" Chunga sana brother kuna mambo mengi we take for granted lakini kumbe ni magonjwa na yanaweza kuwa sugu na kukuathiri hata unavyoishi na watu wengine.

Nendeni hospitali - ningekushauri zaidi Muhimbili - onaneni na pyschs wote wewe na yeye (ingawa kila mtu individually) ili mpate tiba stahiki. Kama daktari akikuambia her condition can change then unaweza kumvumilia until her condition improves. lakini kama ni in born, then you will have to practice 'letting GO'.

Ni kazi ngumu lakini lazima uifanye..adios brother!!!
 
Mwanamke wa dizaini hii atakusumbua sana anachokifanya ni kupretend ili aiteke akili yako wenyewe wanasema amekuweka kiganjani yaani hufurukuti kwake. Ukimuona mwanamke anarudia yale yale kila siku jua akili yake hajaiweka kwako peke yako bali mko wawili mnamchanganya akili zake.
Siku akikutamkia neno baya ndio utamjua vizuri
 
Mapenzi hayashauriki ndugu....mchana tunakushauri umuache halafu usiku unapewa mgegedo huku ukisema ''JAMII FORUM WALINISHAURI ETI NIKUACHE''...nae anakujibu ''WAAMBIE NA KESHO WAKUSHAURI''
 
Kwa mtazamo wangu huyo amelichoka penz na mwanamke ambaye habadiliki huyo ndio tabia yake, nikusih ukae pembenii mana kumpenda kwako ndio fimbo yakukuchapia, mana huyo hawez kubadilika ila kama unaweza kuvumilia hayo mazaifu yake bas muendelee ila hapo hamjaoana tatizo, mkiooona nahis itakua shida zaid
 
Mhesabu makosa penzi haliwezi.

Yupo anaemzuzua na ukimuendekeza atakuacha kweny mataa.
 
Kama yuko ivo tu bado hujamuoa, ukimuoa si ndo utajinyonga kabisa
Jaribu kumsoma ni vitu gani haswa vinavyomfanya awe anakasirika sana afu jaribu kuacha ivo vitu. . . Kama bado atakua anakukasirikia bora ujitahidi umuache
 
ukatili hauepukiki hali inapokuwa hatari .....
 
umesema hujawahi msaliti hilo ndio kosa lako
 
Za asubuhi ndugu zangu..
Natumain mumeamka salama.
Ndugu zangu dhumuni la kuleta uzi huu hapa jamvini ni kuomba msaada
Hali ya mahusiano yangu imefikia pabaya.

Na sijui nafanyaje Mpenz wangu huyu amekuwa ni mtu wa visirani visivyo isha na majibu machafu hata kwa kosa dogo nilijaribu kumuonya kwa miaka miwili sasa tuliyokuwa kwenye mahusiano lakin hajirekebishi.

Kama binadamu wengine kuna makosa madogo madogo kama kuchelewa kufika eneo fulanu kutokana na kubanwa na shughuli Na vingine vingi. Ila ninachoshindwa kumwelewa huwa ananijibu hovyo alafu anakimbilia kuachana kuliko kawaida.

kosa dogo amekimbilia kuachana sio mtu wa kusamehe anabeba visasi mno ukumkosea leo anakumbushia na ya zamani nimemvumilia lakin sasa nachoka nimesha jaribu kuongea na mzazi wake dada zake waongee nae.

Ata pretend wiki moja yuko sawa lakini baada ya hapo anarudia tabia zake nikijichunguza mimi sina kosa sijawahi hata kumsaliti nimekuwa mwanifu kwake lakini yeye hataki kuelewa kiburu kimemjaa nimemsaidia mambo mengi kwenye maisha yake, haswa kutokana na hana kazi ya kueleweka lakin naona juhudi zangu hatambui.

Akitishia kuachana nikikubali kukaa kimya baada ya wiki ananitafuta anaomba msamaha ("huwa anadai kuwa anachanganyikiwa mpaka kufikia hiyo hali ya kuniacha alafU baadae ndio anashtukia kuwa amenikosea, anadai kuwa ananipenda").
Naombeni ushaur ndugu zangu... nifanyaje?

Mpuuze
 
Wapo si ndio kama huyu...design ya wale wanaosomesha kuanzia secondary mpaka Masters.
Duh!!!......Kuna mdada nampenda hapa ofisini kwetu nahisi nimeshaanza kuteseka,Mungu baba naomba niepushe kupenda jamani!![emoji24] [emoji30] [emoji24]
 
Back
Top Bottom