Habari zenu Wadau:
Naombe ushauri:
Nampenzi wangu ambae ni mpangaji kwny nyumba ya Mama yangu ingawa mi siishi hapo, tuna miezi 3 mpaka sasa ktk mahusiano yetu, Upande wa ndugu zangu naochangia mama wapo vizuri kimaisha ila kwa kinvuli chao nami huonekana hivyo ingawa ni tofauti, Nikamweleza mpenzi wangu mtarajiwa hali halisi ya maisha yangu ila nilimficha ile code ya kinvuli cha ndugu zangu kinachofanya nionekane na mimi nipo vizuri kimaisha, Miezi yote 3 mpaka sasa sijatembea nae tukiahidina mpaka tufunge ndoa, Nikiwa nachumguza kumbe nae pia alikuwa akinichunguza ndipo akapewa taariifa na wadau wanaonijua vizuri kama mi nimchovu tu nabebwa na kivuvu cha ndugu zangu!! hivi kimenuka huku najaribu kumtuliza mpenzi wangu na kumuelewesha sababu ya kumficha ilikuwa nikupata uhakika kama kweli ananipenda ama alikuwa na yeye anajitega kupitia kivuli cha ndugu zangu kama kuna neemaaa...
Naombeni ushauri nifanyeje: naona ameanza na kuniwekea pozi sasa hv napomuita tofauti na mwanzo alikuwa anapigia simu nikimuita fasta anakuja!!!
Kweli ndoa za siku hizi tusipoangalia tutavua chura badala ya samaki!!!