Nampenda ila simuelewi

Mwambie mwaka huu unataka muishi pamoja muwe mume na mke,akileta sababu ambazo hazieleweki piga chini songa mbele.
 
Habari zenu wana jf,kama hapo juu panavyosomeka,Nilianza naye mahusiano mwaka 2017,tumekuwa wote kwa mwaka na miezi kadhaa
Mwaka jana mwenzi wa 10 nilipata mimba na wakati huo hatukuwa kwny mahusiano mazuri,lakini tuliongea akasema kwamba tupo wote sababu ya mimba,nilipata stress sana sababu sipendi nije kuwa na watoto wa baba tofauti,stress ambazo kwa kiasi kikubwa zilipelekea nikapata miscarriage, kipindi chote cha mimba mpka miscarriage alikuwa ananisupport kwa asilimi kubwa na pia upendo baina yetu uliongezeka kiasi fulani japo siwezi jua kama upendo wake ulikuwa unamaanisha,baada ya mimba kuharibika nikarudi nyumbani Mkoani kwa family issues,
Wiki ya mbili za mwanzo toka nije mkoani mawasiliano yalikuwa mazuri tu,wiki ya tatu baadaye mawasiliano yakapungu nisipomtafuta hanitafuti na akinitafuta ananilaumu kwanini simtafuti,na mimi kama binadamu sikupenda nikamwambia tu kwamba ww unataka utafutwe tu na unajitia busy,tuligombana sana baada kama ya siku mbili akaniambia kwakuwa siku za wiki yuko busy then tutafutane weekend atatenga mda kwa ajili yangu sikutaka kubishana naye,weekend ikifika bado anakuwa busy nikamwambia kama huwezi kunipa mda hata weekend basi unitafute ukijisikia akasema nampangia,yeye ashasema atanitafuta weekend,sikutaka kubishana naye nikamwambia tu kwny mahusiano mawasiliano ni jambo la kwanza hasa ukizingatia mimi na wewe tuko basi ikiwa kama nimeanzisha ugomvi tukagombana sana,mpka akaniambia kwamba ananipa ruhusa niwe na mwanaume mwngne ili tu nione kama mahusiano yapo kama nnavyodhani nayeye nafasi yake nimuachie palepale anataka tu nipate experience,
Kiukweli nampenda sana lakini kwa hii kauli yake nipo njia panda nahisi hata upendo wangu kwake unapungua kila siku na sitaki kumpoteza ni mtu ambaye amenifundisha mambo mengi na anamchango mkubwa kwenye maisha yangu ukitoa familia marafiki,
Jamani nifanyeje ili huu usiano uendelee

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanaume akikutamkia kua amekuacha basi ujue wewe ni kimeo, itakubidi ukafanyiwe maombi. - JamiiForums
 
Mara ugomvi unakurupua unanitukana mimi

Hata zawadi nikikuletea hausemi asante

Tena nashare hata bila kujua we hulidhiki kwa nini

Kuna wakati nilijisumbua mwenzangu usiwaze

Kwangu moyo we unauchanganya ah

Umekuwa kivuruge unavuruga sana baba wee

Kitu gani kwako mi sijafanya, eeh eeh

Ama kuna mtu mnapendana sana



Leo sina thamani ndo mana

Unawafata ma-sister-du oh baba

Leo sina thamani eeh ndo mana

Unawafata ma-sister-du oh baba

We niache ee



Nitapona mdogo mdogo nitapona (niache)

Nitapona mdogo mdogo nitapona (nitapona kidogokidogo)

Nitapona mdogo mdogo nitapona (nitapona mi)

Nitapona mdogo mdogo nitapona

Aiyoyoiyoooh

(Nandy - Kivuruge)
Ngoja nikaongeze macho yangu yawe manne, yawezekana kwenye hili shairi la kimapokeo kuna ujumbe kuntu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom