Kofia Baya
Member
- Sep 28, 2017
- 9
- 38
Habari za wakati huu
Kama kilivyo kichwa cha habari hapo juu
Mimi ni kijana ambaye nipo katika msongo mkubwa wa mawazo baada ya kulamba sumu ya penzi ambapo mwisho wa siku hata nikijaribu kunywa maziwa hali inazidi kuwa mbaya ukilinganisha na awali kwani moyo unataka lakini akili inakataa, nisiwachoshe sana stori iko hivi.
Kwa kipindi cha muda mrefu sana nimekuwa na tabia ya kununua machangudoa hii tabia niliianza punde tu baada ya mpenzi ambaye nilikuwa nae kwa kipindi kirefu nikitarajia awe mke wangu kwenda kuolewa na mtu mwengine kwa sababu kwangu future hamna kitu kwani kwa kipindi hicho nilikuwa juu ya mawe baada ya kumaliza chuo na kusota kupata ajira bila mafanikio na mwaka mmoja baadae na yeye alimaliza chuo alikuwa anasomea ualimu na longolongo kwao likaanza baada ya uncle kuzuia ajira kwa walimu hivyo nae kuanza kupata joto la jiwe la mtaa.
Baada ya muda nilianza kuona mawasiliano yanapungua baada ya yeye kwenda mkoani ambapo anaishi na wazazi wake, kuna siku moja baada ya kuzungumza na kuonekana hayupo sawa baada ya mazungumzo yetu alinitumia meseji ambayo mpaka leo ilibadilisha maisha yangu ya mapenzi ilikuwa meseji iliyoniuma mithili ya mtu aliyechomwa na kaa la moto kwenye moyo.
Ile meseji ilikuwa na vitu vingi sana ila kwa kufupisha tu ni kwamba aliniomba msamaha na kuniambia kwamba ilibidi aolewe maana alikuwa anaona mambo hayaeleweki na umri unazidi kwenda (unaweza ukasikiliza nyimbo ya barua ya Daz Nundaz barua utanielewa zaidi) hapo ndipo nikagundua kwamba shida zimeyeyusha barafu wa moyo wangu.
Mungu si Athumani wala Juma Hamduni nilipata kazi ingawa ni part time kwenye shirika moja hivyo mia miambili nilikuwa sikosi kwenye mfuko wangu.Nilijaribu mahusiano na wanawake wengine lakini hayaku work out.
Hapo ndipo nilipoanza tabia ya kuwanunua madada poa tabia hiyo nilianza kutokana na kwanza kuhitaji kuwa free sihitaji pressure za kuambiwa utanioa lini, pili kubadili ladha tofauti tofauti na tatu na kubwa zaidi kuogopa kuumia tena maana nilipata heart break na moyo una P.O.P.O bado na sitaki kutoneshwa.
Katika pilika pilika zangu hizo siku moja nilipata kabinti ambacho kalikuwa kabichi na anaonekana hana experience za kutosha na hiyo kazi. Baada ya makubaliano na kutafuta nyumba ya wageni ndipo nilipogundua kitu tofauti yaani nilianza kupenda tena.
The girl was charming na tulipiga stori nyingi sana na nilihisi kutreatiwa kama mpenzi na kama sio mteja aisee niliona dunia imeumbwa tena huku mimi na eva wangu tukizurura bustani ya eden ingawa niliogopa kumuuliza kwa nini anajiuza kwani na mimi ningeulizwa kwa nini nanunua.
Ikawa tabia kila nikienda ile baa huwa namchukua yeye tu tunapiga stori then kama kuna la kutokea linatokea. Penzi lake lilioanza kama mchicha sasa linazidi kukua na kuwa mbuyu na moyo wangu umeridhia kabisa kumfanya mke na kuwa mama wa wanangu ila shida akili inabisha inaniambia jasiri haachi asili na huku ikiniuliza kwa nini nimuoe changudoa wakati wapo wasichana wengi wanaostahili kuolewa.
Nimejaribu kuwaeleza watu ninaowaamini wamesema nimuache tu kama shida ngono niwe naenda ingawa nawaelezea kwamba shida sio ngono ila damu zimeendana kwani hana tofauti na wengine. Kiukweli wadau nimekwama je kuna mtu ameshawahi kuwa na hali kama yangu au kuna ushauri wowote ambao mnaweza nipatia maana sasa nahitaji familia lakini wahenga wanasema heri ukosee kujenga nyumba na sio kuoa.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.