JAMAN BROTHERS NAENDA F5 COMB YA PMC(PHY,MATHEMATICS,COMPUTER) NATAMAN KUPATA DIVISION 1.3 NAOMBENI USHAURI WENU NA TECHNIQUE ZA KUSOMA
Kama uwezo wa kwenda chuoni upo wahi mapema usisubiri hadi umalize form 6, wahi chuoni ukaanze kusomea taaluma kama computer engineering, computer science, IT, n.k.
Ada huwa ni laki 8 hadi milioni na laki 2 hivi, hostel makadirio laki 6, Pesa ya matumizi kuanzia laki na nusu sio mbaya.
Hio kombi ina somo moja tu la computer huwezi linganisha na wenzako wanaoenda chuoni kusoma masomo hata 10 ya computer kila mwaka, wanaruhusiwa kumiliki laptops zao sio mpaka kusubiri kuingia computer lab, wanaweza kushiriki mashindano ya computer ya kitaifa na kimataifa ya computer, kuweza kwenda maofisini kufanya kazi kwa vitendo, n.k.
Form 6 hata ukipata 1 ya 3 hicho cheti hakina uzito popote, ni mpaka uende chuo ambako utakutana na wenzako waliotokea diploma ila mkimaliza degree wao watakuwa na uwanja mpana wa ajira sababu wanaweza kuomba ajira za Diploma na Degree huku wewe umebanwa kuomba za Degree tu sababi cheti cha form 6 sio cha taaluma, halafu wenzako watakupiga gap CV zao zitaonesha wamekuzidi kusomea taaluma miaka mingi tangu walipomaliza form 4 na wamepitia mazoezi ya vitendo maofisini kukuzidi, pia vyeti vingi vya kitaaluma diploma + degree, n.k.
Utachowazidi labda na kuwahi kuingia degree, wewe utaingia degree mwaka 2027, wao wataingia 2028 lakini wakiwa na advantage ya ziada maana hata wakikosa ada za kwenda degree tayari Diploma zao ni taaluma zinazoweza kuwapa ajira ila wewe ukiishia form 6 hicho cheti si chochote hata kiwe ni division 1 ya 3,
VYuo nahisi vinaanza mwezi wa kumi ila maombi kuanzia mwezi huu au ujao
Computer Science –
- Arusha Tech – Arusha
- MUST – Mbeya
- IAA - Dar, Arusha na Manyara
- IFM - Dsm
Computer Engineering
IT – vyuo vingi ila mifano ni
- UCC (Tawi la chuo kikuu UDSM) – Dar na Dodoma
- MUST – Mbeya
- DIT - Dar
- IAA - Dar, Arusha na Manyara