Namna ya kuomba scholarships China

Namna ya kuomba scholarships China

Joined
Feb 18, 2019
Posts
8
Reaction score
15
Yafuatayo ni maelezo ya namna ya kuomba fursa za kimasomo nchini China

Maelezo haya yameandaliwa na Watanzania wanaosoma China-
kupitia HEOCT (Higher Education Opportunities in China for Tanzania).

Mpango huu unahudumia takribani Watanzania 3000 wanaopewa maelekezo ya namna ya kuomba fursa za masomo Nchini China🇨🇳

{Huduma hii inaendeshwa BURE kwa kujitolea}

Huduma hii inaratibiwa na Shirikisho la Jumuiya za Watanzania wanaosoma China kupitia makundi ya WhatsApp.

AINA MBALIMBALI ZA SCHOLARSHIP nchini CHINA zinazoweza kuombwa na Watanzania:

1. Chinese Government Scholarships-

Imegawanyika sehemu kuu mbili-

•Unaweza kuomba hiyo scholarship directly vyuoni kupitia katika website za vyuo husika
(Vyuo husika hutumika kama agency katika kuku recomend kwa CSC/CGS ili upate scholarship.
Hii huwa nzuri maana Chuo kikisha kukubali, CSC wanapitisha moja kwa moja.

Katika kuomba hii utatumia Agency number- ya chuo husika wakati unajaza online.

List ya universities agency numbers zipo kwenye website ya CSC
Njia hii huusisha kutuma documents zako moja kwa moja Chuoni either Online au Posta,

au njia zozote za usafirishaji kulingana ma maelezo yanayokuwa yametolewa katika website ya chuo husika.
Njia ya pili unaweza kuomba kupitia nchini kwetu ambapo jukumu hili limekabidhiwa katika Wizara ya Elimu na huratibiwa chini ya TCU

Tangazo hutolewa wizara ya elimu na TCU.

Tangazo hili huwa na vigezo vya ziada pia vinavyo ongezwa kwa utaratibu wa nchi yetu.
Ujazaji ni uleule kama mwanzo ila hapa tofauti ni Agency number ipo ya Wizara hutolewa kwenye Tangazo.

Hapa ukishajaza documents zako unazituma TCU na zitafanyiwa kazi na majibu yatatolewa na wizara ya Elimu.
2. Chinese universities Scholarships

Vyuo pia vina aina zao za scholarships.
Hii unaimba chuoni na taarifa zake hupatikana kadri unavyo fungua website za chuo husika

Nyingi sana sio FULL scholarships bali Partial scholarships.

3. Confucius Institute Scholarships

Hii number tatu nayo mfumo wake wa kuiomba ni kama wa number 2.

Ila tu tofauti yake ni kuwa hii hutolewa mara nyingi kwa wanao soma lugha ya KICHINA na mambo ya Utamaduni wa Kichina (Masuala ya Kiasili ya China)

4. Local Government Scholarships

Hizi ni Scholarship za Serikali za majimbo China

Anaweza kuomba mtu yeyote na utaratibu ni kuingia website za vyuo ulivochagua na kusoma details vizuri.

Nazo zinaweza kuwa PARTIAL au FULL katika ufadhili wake.

5.Presidential Scholarship

Hii ya mwisho kwa karatasi hii. Inajielezea kama jina lake hutolewa na Rais wa Jamhuri ya watu wa China (kupitia Ofisi ya Rais wa China)

Nayo huombwa na mtu yeyote unaweza pia pata ikiwa FULL au PARTIAL.
6. MOFCOM SCHOLARSHIP:

Hii ni aina ya scholarship ambayo Watanzania tunaweza kunufaika nayo.
Huombwa kupitia Ubalozi wa China, Tanzania. Huwa na vigezo vya ziada na limit ya waombaji.

Hii inafaida nyingi ila Wanufaika wake kwa asilimia Kubwa ni WATUMISHI WA UMMA
Kuna aina nyingi sana za Scholarship nchini China-
Zikiwemo;

•OIL AND GAS SCHOLARSHIP- Hii utangazwa ndani ya wizara ya nishati kwa ajili tu ya kusoma mambo ya OIL and Gas
•BELT AND ROAD SCHOLARSHIPS

Pamoja na Scholarship nyinginezo zinazotolewa makhsusi kwa fani mbalimbali

UTANGAZWAJI & UPATIKANAJI:

Kuna Scholarship zinatangazwa na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-
kupitia Wizara mbalimbali;
(hapa kuna umuhimu wa kufuatilia Matangazo ya Wizara za Nchi yetu)

Njia Kuu ni kupitia Tovuti za Scholarships za China.






 
Unaweza kurecommend Vyuo vizuri vya Afya kwa Undergraduate ?

- Je, ni kweli international students ( MBBS ) China hawaruhusiwi kugusa mgonjwa na badala yake hutumia midoli ?

- Je, kuna uwezekanao wa kupata scholarships za afya ?

- Je, kama mtu anataka kusoma MBBS China bila scholarships yoyote gharama za ada zikoje ?
 
Pia kuna Kampuni kama Global Education Link (CEO: Mr Mollel) na Universities Abroad Link (CEO Mr T. Kabetha) hawa wanaonekana wana uzoefu kutafuta shule na scholarship China na nchi nyingine. Uzuri hawa wamesajiliwa TCU kwa hiyo wanakusaidia upate kitu chenye mashiko kwa Tanzania. Sijajua kama wanatoza gharama kiasi gani kwa service hiyo.
 
Pia kuna Kampuni kama Global Education Link (CEO: Mr Mollel) na Universities Abroad Link (CEO Mr T. Kabetha) hawa wanaonekana wana uzoefu kutafuta shule na scholarship China na nchi nyingine. Uzuri hawa wamesajiliwa TCU kwa hiyo wanakusaidia upate kitu chenye mashiko kwa Tanzania. Sijajua kama wanatoza gharama kiasi gani kwa service hiyo.
GEL nime wa email kutaka kujua gharama ambazo wanachaji kwa kumsaidia mtu kufanya Application lakini naona kimyaa hawajanijibu

Binafsi naona kupitia hawa kuna uwezekano ukafanikisha kuliko wizarani naskiaga kuna ubaguzi kwenye Scholarship

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GEL nime wa email kutaka kujua gharama ambazo wanachaji kwa kumsaidia mtu kufanya Application lakini naona kimyaa hawajanijibu

Binafsi naona kupitia hawa kuna uwezekano ukafanikisha kuliko wizarani naskiaga kuna ubaguzi kwenye Scholarship

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza ukawapigia simu pia. Nafikiri uki-google utapata namba zao. Institutions zetu nyingi sijui kwa nini ni wazito wa kujibu -email.

Serikali huwa wanapenda watumishi wao kwanza halafu ndio wewe na mimi na kama huna ajira inaweza kuwa kazi sana. Lakini usikate tamaa-keep on trying.
 
Unaweza ukawapigia simu pia. Nafikiri uki-google utapata namba zao. Institutions zetu nyingi sijui kwa nini ni wazito wa kujibu -email.

Serikali huwa wanapenda watumishi wao kwanza halafu ndio wewe na mimi na kama huna ajira inaweza kuwa kazi sana. Lakini usikate tamaa-keep on trying.
Nilitaka nipate tu details za kutosha alafu nipime maana ukipata full scholarship kwa baadhi ya vyuo vya China inakuwa safi sana hata shughuli zako unaweza kuzisitisha na kumwachia ndugu yako anendelee alafu we unaenda kuongeza CV

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom