Namna ya kuokoa CHADEMA isife...

Uzuri mmoja ninao upendea kwenye hiki "kifo" cha Chadema ni hu; uchaguzi wa wabunge popote ambapo Chadema "mfu" imeshiriki, ccm wametangazwa kwa msaada wa police, najiuliza tu, "sijui kwanini police wanahangaika na WAFU" maanake maiti wala hua hazisemi!
Nimepiga kura chaguzi zote ambazo umezitolea mfano, CUF umeipa tu sifa isizo stahiri, CUF haijwahi kuwa tishio bara kama Chadema na in fact hata nusu tu haijafikia, NCCR-Mageuzi labda but nayo ni kwa mwaka mmoja tu; again umaarufu wa NCCR-Mageuzi mwaka ule sio wa Mrema pekee yake (sina maana Mrema hakuchangia, but him sio pekee aliyeleta msisimko) Uchaguzi wa Zambia mwaka 1992 na Malawi vilichangia sana kuona pia hata Tanzania tunaweza kukiondoa chama tawala madarakani, washukuru Nyerere alifanya yake.
 
25-27 October 2020..tusije kulaumiana maana Kimbunga Cha JPM kitasomba madudu yote..na hawataonekana Tena katika taswira ya siasa za nchi yetu.mjiandae kisaikolijia kupokea maamuzi ya wenye nchi
 
Naomba ulete hapa tofauti ya NCCR ile ya akina Lamwai,Marando, Tundu Lissu, Antony Komu, Mrema, Mbatia na Chadema hii kitaasisi.
 
Hili ni andiko la George Kahangwa nafikiri unamfahamu vizuri ....soma katikati ya mstari ...

Muuliza swali nashawishika kuamini kwamba ulitaka kujua kweli. Kama ni utafiti naomba uzingatie taarifa hizi

1. Vuguvugu la wanamageuzi lilianza miaka ya 80 wakati wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam walipoanza kuhoji uwepo wa mfumo wa chama kimoja. Ni katika kipindi hicho Ndg. Mabere Nyaucho Marando (Katibu Mkuu wa kwanza wa NCCR) alifanya presentetion hapo chuoni kuhusu suala hilo. (Kama nakala ya presentation yake inaweza kupatikana basi siku moja tutaiweka hapa, kwa ajili ya kuweka kumbukumbu vizuri)
2. Mnamo mwaka 1984, Ndg.James Mapalala (makamu mwenyekiti wa kwanza wa NCCR) alimwandikia Mwalimu Nyerere barua ya wazi akitaka mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini (kumbuka ulikuwepo awali Mwalimu akaufuta)

3.Miaka saba baadaye (1990) Mwalimu akaanza kuelewa (wakati huo alishaacha urais) akaanza kusema si vibaya mfumo wa vyama vingi ukirejeshwa nchini
4. Mnamo mwaka 1991 wasomi wa UDSM, pamoja na wanaharakati wakaianzisha NCCR. Ikawa chini ya Uenyekiti wa Marehemu Chifu Abdallah Fundikira (waziri wa zamani wa Mwalimu), Makamu; Mapalala, Katibu Mkuu; Marando.
5. Mwaka huo huo 91 Rais Ali Hassan Mwinyi akaunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi kama vyama vingi viruhusiwe au visiruhusiwe. Watanzania wengi hawakuvitaka, lakini wapo waliosema virudi.
6. Mzee Mwinyi akaheshimu mawazo ya wachache, mwaka 1992 akaruhusu virudishwe.
7. Mwaka huo 1992 (hapa ndipo sura ya sasa ilipotoka) waliokuwemo ndani ya NCCR wakagawanyika. Fundikira Mwenyekiti akaunda chama; UMD (japo kabla hajafa alirejea CCM), Mapalala huyo naye akaunda CCW ambayo kwa kushirikiana na Shaban Mloo wa KAMAHURU ya Zanzibar wakaunda CUF (sasa Mapalala yuko CHAUSTA). Marando akaendelea kuiongoza NCCR kwa kuiboresha na neno Mageuzi (sasa naye yuko CHADEMA), baadhi ya wajumbe wengine wa NCCR wakashiriki kuiunda CHADEMA wakitumia kaulimbiu ya NCCR 'demokrasia na maendeleo'. Na wengine wakaendelea kuunda vingine, matharani hata Mziray wa APPT-Maendeleo anatokea NCCR.

Kwa ufupi NCCR ilisambaa kabla ya ujio wa Mrema. 'ikawa kama maandiko; nitampiga mchungaji wa kondoo, na kondoo wa kundi lake watatawanyika)
8. Ndio sinema ya 1995 ikaanza (Hii sasa usome Kitabu cha Ndimara Tegambwage)
 
Ni tabia ya kawaida kwa fisi kuwatakiwa viumbe vingine vife ili afaidi mzoga.......
 
Nimekuelewa, binafsi sina muongo wa kisiasa wa Chama fulani, ila Chadema hawana budi kujitafakari kwani ni dhahiri kuna baadhi ya mambo hayako sawa kwa sasa ingawaje yawezekana ni matokeo ya visababishi vya ndani ama nje ya Chama chao, hekima si kutaka kusikia linalokufurahisha pekee! Kubali kusikia madhaifu pia ili ktk kuyatatua ni dhahiri hukufanya kuwa bora zaidi.
 
Huo ni mtazamo wako. Na hivyo vyama NCCR, TLP na CUF havijafa. Vinaonekana dhaifu sababu ya uimara wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA. Na ndio maana mashambulizi mengi yanaelekezwa CHADEMA kuliko sehemu nyingine. Hutosikia mwenyekiti wa TLP anashambuliwa, wala wa NCCR ndio maana kila siku ni CHADEMA hivi, CHADEMA vile. Mara CHADEMA kahujumu elimu, mara sijui wanajifunza ujasusi Libya. Hii yote ni kudhoofisha nguvu aliyonayo CHADEMA katika siasa za Tanzania.
Wewe kama unaishi kwa historia, endelea tuu kuishi hivyo.
 
Upinzani utaendelea tu, Tanzania ni nchi ya vyama vingi na CHADEMA inazidi kuimarika. Peoples[emoji1479]
Huwa napenda sanakusikia hicho kiitikio cha "chadema inazidi kuimarika"
Inanikumbusha maneno ya kujitapa na kejeli za yule waziri wa Iraqi. Majeshi ya UN yakikaribia kuuteka mji mkuu Baghdad, yeye alikuwa akijitapa kuwa majeshi yao yanatoa kipigo kwa majeshi ya un.
 
Kwa nini unafurahia kifo cha Chadema?
Nipe sababu tano zenye mashiko kwa mustakabali wa taifa.
 
Hujiulizi ni kwanini viongozi wa CHADEMA wanatekwa,wanatengenezewa kesi, wanauawa na wengine kujeruhiwa huku SERIKALI IKIFURAHIA hiyo hali????.
Haujiulizi ni kwa nini mkuu wa nchi yuko kimya juu ya haya yanyoendelea nchini???.
Kipara kipya kaa kimya Ndugu kwa sababu haujui na huajui kuwa haujui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…