mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,714
Chadema haifi mamluki wanajiondoa wenyeweChadema ndio bye bye hakuna dawa wala uganga inakufa kifo cha Nccr mageuzi,Cuf hivi vyama viwili vilipita katika njia wanazopitia chadema kwa hivi sasa,
Nccr baada ya kutamba uchaguzi wa 95 kwa kumpokea kada mkuu wa CCM Lyatonga mrema baada ya hapo ikawa ni mtifuano na kufifisha chama machoni mwa watu mpaka leo hii Nccr haipo labda ukisikia mbatia ndio unakumbuka kuna kitu kinaitwa Nccr mageuzi
Cuf ilipita njia hizi hizi za Chadema baada ya kutamba uchaguzi wa 2000 Cuf rasmi iliingia kwenye mitifuano isiyo kwisha mpaka kilizaliwa chama cha kingine kupitia aliyekuwa kada wao maarufu Hamadi Rashidi leo hii kama tunavyoisikia Cuf inapumulia mashine kuna ya zanzibar na ya bara
Historia inatuonyesha Chadema baada ya kumchukua kada wa Ccm maarufu Lowassa leo hii Chadema ipo kwenye minyukano ya chini kwa chini japo wenyewe wanajaribu kuifunika lakini kwa muonekano tu Chadema inayumba na imepoteza muelekeo watu kila kukicha wanaikimbia Chama na wameanza kutuhumiana tuhuma za usaliti wao kwa wao!
Swali kwanini kila kada mkuu wa CCM akihamia chama cha upinzani hukumbwa na dhoruba!
Hizo ramli hazijaanza leo. Nyie wapiga ramli wa sasa ni sisimizi tu.
Alianza yule chimpanzee wa Bunda. Sijui yuko wapi sasa.
Chadema ishakufa tokea wamchukue fisadi
Upinzani hautakufa lakini si chadema. Wameshupaza shingo kufanya mabadiliko. Chadema inafutika kwa staili ile ile ya NCCR kwa tuliokuwa tunafatilia siasa tunakumbuka vyema.na kila anayekufa anaona hafi, mpaka anakufa na kukosa muda wa kujiuliza why
wanachama wote ni nyumbu
kikifa nyumbu wanahamia jengo lingine
Mtapata tabu sana na Chadema, eti sio kufa kama binadamu ruksa kubadilika kama kinyonga.Wana Ufipa ukiwaambia Chadema utakufa wanadhan tunamaanisha kufa Kama kifo Cha binadamu
Tunamaanisha kifakufa Kwa maana kitakuwa Kama NCCR Au CUF
Hata akiondolewa Kubenea ataibuka mwingine tu Halafu Mara nyingi wale watu wa karibu Na Mbowe anaewaamini Sana ndio huja kum challenge
Alianza Chacha Wangwe, akaja Zitto Kabwe, akaja Dr Slaa Na Sasa Mwandani Na maiti wa Mbowe Ndugu Kubenea Na Komu nao wamechoka
Hata Hawa kina YericKo nao watakuja kumzingua Na kumchoka Mbowe
Mtapata tabu sana na Chadema, eti sio kufa kama binadamu ruksa kubadilika kama kinyonga.
Kwani wakati wa NCCR ulikuwepo peke yako ina maana wengine hatukuwepo, enzi za Mrema upinzani ulikuwa mchanga haukuwa na mbinu madhubuti wala resources za kupambana figisu za CCM, mihemuko ilizidi uhalisia.Upinzani hautakufa lakini si chadema. Wameshupaza shingo kufanya mabadiliko. Chadema inafutika kwa staili ile ile ya NCCR kwa tuliokuwa tunafatilia siasa tunakumbuka vyema.
Politics is not static is dynamic, kila wakati na siasa zake, siasa za ustaarabu ni tofauti na siasa za kidikteta.Siku hizi Mbona mmekuwa Wapole sio Kama enzi Za Mkwere?
Mkwere angewaambia Marufuku Mikutano ya Kisiasa mngetii Kama mnavyomtii Mwenye heri John Magufuli?
Kwa hiyo kwenye Siasa Za kistaarabu ndio mnapiga mikwara kwenye Siasa Za kidikteta mnaufuataPolitics is not static is dynamic, kila wakati na siasa zake, siasa za ustaarabu ni tofauti na siasa za udikteta.
ccm ilishakufa na nyerere. kilichobaki sasa ni kivuli chake kinacholindwa na polisccm,nec na hata dola kiujumla....na CCM inafuata itakufa kama wale walio zama maji ukerewe
TLP,NCCR,UDP bado vipo havijakufa mkuu !Siku CHADEMA ikiisha/ikifa tena kifo cha Mende, mniamshe nisherehekee nipo ndani ya shuka gubigubi hapa
Hayo sasa ni malumbano yasiyokuwa na hoja ndani yake tafuta swali au hoja nyingine nikujibu.Kwa hiyo kwenye Siasa Za kistaarabu ndio mnapiga mikwara kwenye Siasa Za kidikteta mnaufuata
Imani huleta upumbavu muda mwingine kuamini aliyekufa ataamka!Chadema ni imani, kama unajua nini maana ya imani utakuwa hujisumbui na huo ujinga uliopost
Inawezekana utabiri wake ukawa na ukweli maana yanayoendelea huko ni siri y baina ya kubenea na komu!Ramli hizo hazijaanza leo alitabiri mzee Wasira miaka ya 2010 kafa yeye instead.
View attachment 900706
Ndio maana nami nimeuliza kwanini kila kada wa CCM akichukuliwa upinzani kunazuka balaa!Sawa sababu kuu ya haya yote mkuu chanzo nini!
Hakiwezi kufa ndio maana tuna utitiri wa vyama baada ya kuzaa vyama watoto hivyo vyama mama vinadhohofika!Wassira ambaye alikuwa na nguvu ndani ya ccm kuliko huyu jiwe anashangaa Chadema haifi ila yeye ndio anajifia na sasa amekuwa mfuga mbuzi tuu. Gademit!!
Résultats Google Recherche d'images correspondant à https://1.bp.blogspot.com/-JUEiSQ3ROAw/UpmOTi4cZVI/AAAAAAAAbnw/0QgkXCOAgIo/s1600/1476615_550118435076927_368953879_n.jpg