Namna ya kumkamata mwanaume!!

Namna ya kumkamata mwanaume!!

Kweli kabisaaa, na no. 2, nimeipenda sana, watu wanakurupuka mno, eti utanioa lini, or sijui nataka kuja kwenu kutoa posa, eeeh, wakati ndio una wiki 3 tangu ufahamiane naye, naogopa such people, kuoana si mchezo, ukikurupuka baadae unaweza ukajuta sana, ukajikuta uko na mtu asiyekufaa kabisaaa kimatendo
 
Kwa kweli siku msichana akinifanyia haya lazima nimtangazie ndoa. Maana kama umejua vigezo
 
I was single once, but now i'm a wife and a mother. Nimekaa nikaona sio vibaya iwapo nta-share tips kadhaa zilizonisaidia kumuweka baba Ashrat sawa na mpaka leo hii sijawahi kuhisi wala kugundua kwamba anatoka nje ya ndoa yetu, japo matatizo ya hapa na pale hayakosekani ila tumedumu na bado tunaendelea na safari.

Unapokutana na mwanaume akakutongoza/mwanamke akakukubalia kuna uwezekano mkubwa kuwa amevutiwa na wewe kweli au kakutamani tu. Kitu ambacho watu hua wanasahau ni kwamba hata mtu aliyekutamani tu unaweza ukampa mwongozo/sababu mpaka mwenyewe akajikuta anakupenda kuliko ambavyo angeweza kutarajia kwamba angewahi kupenda. Ndio maana hata wale waitwao 'bad girls/boys' hua wanajikuta wamenaswa na kunasika at some point.

1. Usiigize.
Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/mazoea n.k

2. Don't move too fast/act desperate.
Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa wa mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo gani na mie?" "utanioa?" "Kanitambulishe/nataka nikakutambulishe." n.k Mpe nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa aina gani, je unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho hicho.

3.Don't be too demanding.
Huyo sio baba yako wala sio mume just yet, hivyo chochote atakachokufanyia kinatokana na yeye kutaka/kupenda kufanya hivyo na sio kwakulazimika. Haki hiyo hauna.

4. Kuwa na shukurani.
Learn to appreciate all that he does for you, that way ataona umuhimu wa hayo anayokufanyia, yawe makubwa au madogo.

5. Be real.
Badala ya kufika kwake na kuanza kushangaa anaishije bila ya mfanyakazi wa ndani huku ukitamba kuwa wewe huwezi, shangaa anawezaje weka nyumba yake katika hali nzuri mwenyewe bila ya msaada. Hii itaonyesha fika wewe utakua mke wa aina gani hapo baadae, kama ni wale wakukaa miguu juu huku wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au la.

6. Learn to cook if you don't know how to.
Waliosema "the way to a man's heart is through his stomach" hawakukosea. Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili kushiba wengi hua wanajali ladha. Hiyo ndio hua inawaongezea hamu ya kula na kuwarudisha nyumbani mapema pia kuwafanya wakumiss pale inaposhindikana kula chakula chako . Kwakumwonyesha mwanaume kwamba hata tumbo lake unaweza kuliridhisha unamwongezea sababu za kukuweka kwenye maisha yake.

7. Mheshimu.
Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba haheshimiki.

8. Kuwa ngao yake.
Inapotokea anakumbwa na matatizo yoyote yale onyesha utayari wa wewe kuwa pamoja naye kwa hali na mali mpaka yatakapoisha. Pia usikose kumjali kumpa moyo pale unapoona inahitajika.

9. Kuwa muwazi.
Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa moja yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema ili aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la.

10. Usiwe na chuki.
Kikifika kipindi cha yeye kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake onyesha ushirikiano. Usionyeshe chuki wala kujiona kana kwamba wewe ndio wewe.

11. Give your all.
Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na usiwe mvivu.

12.Pendeza.
Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje hata ndani pia. Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu mavazi yako.

13. Onyesha interest kwa yale ayapendayo yeye.
Usiwe mbinafsi kila siku unataka kusikilizwa wewe tu na story/mambo utakayo wewe. Uliza/jua kuhusu yale anayopenda yeye mf. mpira/siasa.

14.Kuwa mtulivu.
Usiwe mtu ambae kila saa simu yako inapigwa pigwa na wanaume wasio ndugu wala marafiki wakaribu na wanaoeleweka. Discpline ni muhimu sana.

15.Usimzonge.
Usiwe mmoja wa wale watu wanaofuatilia wenzi wao masaa yote wanapokuwa hawapo pamoja. Mpe nafasi ya kuwa na marafiki zake bila kuhitaji kuzima simu ama ku-ignore simu/text zako.

16. Mfurahishe/chekeshe.
Joke around sio muda wote yeye ndio awe wakukufurahisha wewe.

17. Jifunze kusamehe.
Mambo madogo madogo yanapoombewa msamaha samehe na uache yapite.

18. Mshirikishe Mungu wako.
Ukishaona kwamba huyo ndie basi mshirikishe yule unayemwamini ili upate mwongozo wa kiroho.

Mama Ashrat.
Mwanamke akiyafuata na kuyatekeleza yoote hayo ulioyasema, basi najua sichomoki. Atanipata tu
 
Ni kweli kabisa hata mie zipo nilizozitumia hapo na nilipata BIG results,
wasichana msione hayo ni maigizo punguzeni kuiga mambo wanayoita ya mjini mengine hayana faida kwenye maisha..
Women lets be independent kifikra na kimatendo pia.
 
Ni kweli kabisa hata mie zipo nilizozitumia hapo na nilipata BIG results,
wasichana msione hayo ni maigizo punguzeni kuiga mambo wanayoita ya mjini mengine hayana faida kwenye maisha..
Women lets be independent kifikra na kimatendo pia.

so truee dr
 
Nimekukubali. Problem yetu ni desperado! Nna dadangu akiambiwa na mkaka ntakutoa jioni, anaulizia pa kupata gauni la harusi!
Kila la kheri mama

Ahahaha King'asti bana ahahaha!

I cant wait to see you@ JF party this saturday!I'll give you some MATABORWA as my precious gift from Kyela!

CC DEMBA
 
Last edited by a moderator:
hehehee, i am invisible aisee, ntakuwepo kwa party ila hutoniona wala kunitambua.
ngoja kwanza, matobolwa ya kyela ni ya kichina ama yako kama yale ya tabora?
Ahahaha King'asti bana ahahaha!

I cant wait to see you@ JF party this saturday!I'll give you some MATABORWA as my precious gift from Kyela!

CC DEMBA
 
kakangu tembea ujionee. afu lina akili za shule na madigirii. akili za wanaume hana kabisaaaaa!
tena anapanga na tarehe ya harusi, muulize huyu kaka kabila gani, sijamuuliza! anaishi wapi? nadhani kinondoni manake kuna siku nilimsikia akimuambia mtu tukutane kndoni.

Dadake 'fixed point na "snowhite huyo, wanamjua 😛ray:
hahahaha hii kali King'asti
 
na wewe hebu acha ubahili. sasa makange rose garden, bajaj to akudo and bajaj home ni sh ngapi? ndo maana hamuwowi. relationship zetu zamani paw anakungoja kisimani na anakubebea maji hadi home. au mnaenda kukata kuni unachangia stori tu. :bump:
Lzm kwanza weekend mkale Makange Rose Garden na jioni mkaserebuke Akudo!

Relationship za siku hizi gharama sana
 
kakangu tembea ujionee. afu lina akili za shule na madigirii. akili za wanaume hana kabisaaaaa!
tena anapanga na tarehe ya harusi, muulize huyu kaka kabila gani, sijamuuliza! anaishi wapi? nadhani kinondoni manake kuna siku nilimsikia akimuambia mtu tukutane kndoni.

Dadake 'fixed point na "snowhite huyo, wanamjua 😛ray:

Aisee......kumbe eeh...haya.

CC Fixed Point snowhite
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli siku msichana akinifanyia haya lazima nimtangazie ndoa. Maana kama umejua vigezo

Umeonaa mkuu eh? Mi akinifanyia hayo yote hata baadhi tu hakika natangaza ndoa. Unajua wanawake hawajajua kitu kimoja; MEN ARE DRIVEN BY WOMEN namaanisha nini jinsi yeye atakavyokuwa anajichukulia ndivyo nami ntakavyokuwa namchukulia. Akijijali, akijiheshimu, akionesha hali ya kunithamini nami automatically najengeka katika hayo juu yake.
Asante sana Mama Ashrat kwa hili somo, hakika unawatakia baraka njema wanawake wenzako kutokana na hali ya maisha ilivyosasa. Big thanks to you, I know some of women will be caught up by this n get something to practise.
 
Kama hakupendi hata ungemfanyiaa nin hakupendii tu
Wewe ndio huelewi, hamna mtu huwa anapenda mnapoonana mara kwanza, ile huwa ni kutamani tu.
Atakupenda baada ya kuwa pamoja na kuzoeana, na inawezekana baada ya kumfanyia aliyoeleza Mama Ashrat.
 
Back
Top Bottom