Namna ya kudhibiti Nguruwe Pori kwa uharibifu shamba la Mihogo

pamoja na njia zilizoshauriwa hapo juu, vile vile wakati unapanda basi unaweza kuzungushia pembeni kama mistari minne ya mihogo michungu, wakiingia wakaonja wakakuta ni michungu wanadhani shamba zima liko hivyo hawafanyi uharibufu mkubwa... lakini pia ni vizuri ukapanda sehemu ambayo kuna mashamba mengine ya mihogo..ukikuta umepanda mwenyewe lazma uumie
 
Utajiri huo ndugu, tafuta kibali maliasili uweke mitego ukamate uuze nyama. Hiyo mboga ni tamu kuku atasubiri mno...
Yani hadi nimekuonea wivu, aliyesema kwenye miti hakuna wajenzi hakukosea
 
Ha ha ha anawarogaje sasa umenichekesha mkuu
 
Wadau,

Kama mada husika hapo nina shamba kubwa la mihogo changamoto kubwa niliyonayo ni nguruwe usiku wanafanya uharibufu.

Naomba mawazo na maarifa ya kuwadhibiti

Ahsanteni
Aisee kuna post moja nimeifumania. Jamaa amesema aliwadhiti hao wadudu kwa kuweka taa kadhaa (katika kila pande) shambani. Kwakuwa wale jamaa hawafanyi shughuli zao mchana/kwenye mwanga, kwahiyo ukiweka taa hawatafanya yao.
 
Hiyo avatar yako na hayo maneno uliyoyaandika kwenye bold yanatia shaka na ukakasi.
Allah hawezi kunihukumu kwa Kula nyama labda kama sikumshukuru kwa neema hiyo aliyo kuruzukia waja wake! Labda Mwenzangu mjuzi niwekee ushahidi ilipopigwa ban..
 
Allah hawezi kunihukumu kwa Kula nyama labda kama sikumshukuru kwa neema hiyo aliyo kuruzukia waja wake! Labda Mwenzangu mjuzi niwekee ushahidi ilipopigwa ban..

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللّهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلاَ عَادٍ فَلا إِثْمَ عَلَيْهِ إِنَّ اللّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
 

Wee mbona unachekesha
unaelewa dharula bro? sasa ikikufika uteme au ule? mbona hujaambiwa ukishikwa na dharula uikurubie zina? Na ukila kupitia kiasi wee ni mlafi...Kula tu bro chaumbile Imulungu ni cha kumemena
 
Mkuu kama bado unahitaji njia rahisi ya kuzuia Nguruwe ni kuchimba Msingi wa upana kama Futi moja kwenye upande ule wanaoingilia au kuzunguka Shamba hapo hawawezi kupita tena coz Miguu yao ya mbele ni mifupi na hawawezi kuikunja hivyo utamkuta asubuh akihangaika hapo. Aidha kwa Nyani ni kuripua baruti iwe kwenye Gobole etc hapo hawawezi kurudi tena mana wanaogopa Bunduki sana.., ikishindikana nunua redio halafu uwe unaiwasha muda wao ule wanaokuja, iwashe sauti ya juu basi watajuwa mwenyewe yupo hivyo hawata ingia shambani.
Nb:
Hii ya Redio inabidi ujiridhishe na aina ya Nyani unayodeal nao kama ni wa Porini haswa itafanikiwa, ila wakiwa hawa wanaokula Mikate kama huyo kwenye avator yangu, ndugu yangu utawakuta wamemaliza Shamba lote huku wamebadili na stesheni wameweka Bongofleva wanaserebuka kwa furaha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…