Namna ya kuandaa ubuyu wa Zanzibar

Doncy monco

Member
Jul 26, 2019
38
101
Mahitaji
1. Sukari vikombe 2
2. Maji vikombe 2
3. Nusu kikombe unga wa ubuyu
4. Vikombe 4 ubuyu wenyewe
5. 1/4 pili pili ya unga
6. 1/4 tsp chumvi
7. 1/4 tsp iliki ya unga
8. Rangi nyekundu au yeyote ile utakavyopenda. 9.vanilla(kama utapenda)

MATAYARISHO
1. Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.

2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.

3. Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi Ttu
4. baada ya mchanganyiko wako kuiva ipua hayo maji sasa Chukua beseni au sufuria chini weka ubuyu wako ndani ya beseni Anza kumimina hiyo juice yako kidogo kidogo huku ukiuchanganya kwa mikono safi.Ila hakikisha pembeni una Unga wa ubuyu ulio changanywa na mchanganyiko huo huo.

5.Baada ya ubuyu wako kuchanganyika vizuri (usiwe rojo) Anza kumiminia ule unga kwa juu ili uwe mkavu mkavu na kutoa ule ubichi alafu uanike ukishapoa ubuyu tayari kuliwa.

Angalizo: Hatua ya 4 ni muhimu sana hakikisha mchanganyiko unamimina kwenye ubuyu mkavu na sio kuchukua ubuyu mkavu na kuupikia.Tunafanya hivyo ilikufanya ubuyu uwe mlaini na usiwe mgumu wakati wakula.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom