Namna wafanyabiashara wanavyopata tabu Tabata Kinyerezi

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,607
1,596
Tabata Kinyerezi ni eneo lililopo Jijini Dar es salaam wilaya ya Ilala,

Kulikuwa na soko eneo la Tabata Kinyerezi, soko hilo lilivunjwa na uongozi wa wilaya ya Ilala mwaka 2004 kwa lengo la kupanua soko hilo ili liwe la kisasa na kuweza kuhudumia wananchi wengi wa Kinyerezi na jiji la DSM kwa ujumla.

Lengo la mpango huo pia ni kuweza kupunguza msongamano katika soko la kariakoo kwa kusaidia wafanyabiashara wengine kuhamia soko la kisasa la kinyerezi.

Wananchi wengi walipata hasara baada ya kuhamishwa sokoni hapo ili kupisha maboresho lakini wakiwa na imani baada ya mda mfupi watanufaika na uboreshaji huo.

Ni miaka kumi na tatu sasa imepita, eneo hilo hilo lililotengwa kwa ajili ya soko sasa limeshavamiwa na watu wamejenga magorofa yao na wengine wanaendelea na shughuli zingine kinyume na malengo ya soko hilo.

Eneo lililobakia sokoni hapo likawa dogo, hivyo serikali ya uongozi wa ilala ikalazimisha kujenga kasoko kadogo kasiko na viwango tena kwa gharama kubwa kuliko kawaida.

Wafanyabiashara baada ya kuvunjiwa biashara zao sokoni hapo mwaka 2004 iliwalazimu kuamia eneo lisilo rasmi la kinyerezi mwisho,
eneo la kinyerezi mwisho ni hatari kwa usalama wa wafanyabiashara hao sababu wapo karibu na nguzo za mitambo mikubwa ya kufua umeme Kinyerezi.
Viongozi wa wilaya ya Ilala fanyieni kazi kuweza kumalizia haraka iwezekanavyo kumalizia soko rasmi la kinyerezi kwani wafanyabiashara wanaangaika sababu hadi sasa hakuna sehemu rasmi ya soko eneo la kinyerezi na hii inapelekea mitaji ya wafanyabiashara kufa.

Tarehe 29/05/2017 Mwenge wa uhuru ulifika sokoni hapo ili kuweka jiwe la msingi,
Sasa hii ina mashaka kwamba kwanini tangu mwaka 2004, mwenge wa uhuru unakuja kuweka jiwe la msingi 2017,

pia kuna siku mkuu wa mkoa wa DSM ndugu Paul Makonda aliendaa kimya kimya sokoni hapo kuangalia kinachoendelea sokoni hapo ila hadi leo hakuna kinachoendelea sokoni hapo.

Wafanyabiashara tunauliza inakuwaje mwenge wa uhuru unaweka jiwe la msingi kwenye soko ambalo tayari limehujumiwa kwa kujengwa magorofa ya watu binafsi na vitu vingine kinyume na mpango wa soko?
Pili nini tatizo hadi sasa soko hili limeshindwa kukamilika kwa kipindi cha miaka 13?
Hivyo tunawaomba uongozi wa wilaya uboreshe na kufungua soko la kinyerezi mapema ili kuweza kunusuru mitaji ya wafanyabiashara na pia kuongeza mapato kwa halmashauri ya wilaya ya ilala, mkoa wa Dsm na nchi kwa ujumla.

Pia tunamuomba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda aweze kufatilia hili hili tatizo sokoni hapo kwa ukaribu hadi liishe sababu alishawahi fika kimya kimya na anajua matatizo ya eneo hilo Sokoni Tabata Kinyerezi.
Wafanyabiashara wa kinyerezi wamekuwa katika tabu kubwa tangu mwaka 2004 soko hilo lilipo vunjwa na wamekuwa wanaingia hasara kwa kuwa hakuna eneo rasmi la biashara eneo la Tabata Kinyerezi bali wanachoambulia ni tabu ya kudaiwa kodi kwa wenye nyumba na mamlaka mbalimbali za serikali kama TRA, TFDA n.k
 
Aisee poleni sana kwa kadhia mnayopata miaka 13 yote hiyo...Lazima kuna masuala hayajakaa sawa hapo Either utendaji mbovu au ufatiliaji usio wa kuridhisha katika kuendesha soko lenu
 
Aisee poleni sana kwa kadhia mnayopata miaka 13 yote hiyo...Lazima kuna masuala hayajakaa sawa hapo Either utendaji mbovu au ufatiliaji usio wa kuridhisha katika kuendesha soko lenu
Ni shida kubwa sana tunayo ndugu Joseverest,
kila mwaka zinatolewa ahadi kwamba soko la Tabata Kinyerezi litafunguliwa, imepita miaka 13 sasa na tayari watendaji wameshauza maeneo kwa watu binafsi waliojenga magorofa yao binafsi pia kuendesha shughuli zingine kama gereji, viwanda vya matofali n.k kinyume na malengo ya soko,
eneo lilibaki pale ni dogo sana ila napo wanashindwa kumalizia na kufungua soko hilo kilichobaki ni hasara kubwa kwa wafanyabiashara
 
Yaani hao watendaji ndio wana makosa sana hawana huruma na wafanyabiashara wako hapo kujinufaisha tu, wanawapa ahadi za uongo tu..embu ona sasa eneo lilibaki ni kidogo...inasikitisha kwa kweli ndugu
 
Yaani hao watendaji ndio wana makosa sana hawana huruma na wafanyabiashara wako hapo kujinufaisha tu, wanawapa ahadi za uongo tu..embu ona sasa eneo lilibaki ni kidogo...inasikitisha kwa kweli ndugu
Una ushauri gani katika hili jambo ndugu?
 
Mjitahidi tu kufikisha hoja zenu kwa viongozi husika kwa msistizo tu hadi wazitimize
 
yaani miaka 13 ni hatua ya upembuzi yakinifu na kuweka jiwe la msingi........ hapo inaonesha baadhi ya wataalam/ wasomi na viongozi wetu akili zao zinafikiria taratibu.....
 
yaani miaka 13 ni hatua ya upembuzi yakinifu na kuweka jiwe la msingi........ hapo inaonesha baadhi ya wataalam/ wasomi na viongozi wetu akili zao zinafikiria taratibu.....
Uko sahihi kabisa ndugu, tabata kinyerezi lile soko limekuwa kama kichaka maana ahadi za kufunguliwa zimeanza kutolewa ni miaka mingi imepita sasa, cha ajabu ni kwamba pembeni kuna ofisi ya mtendaji, kuna mahakama ina maliziwa ujenzi na pia kituo cha polisi kimeanza kufanya kazi, ila soko ndio limepigwa zengwe na watendaji pale
 
Ushauri mzuri.
Au nendeni kwa mkuu wa wilaya mpeleke kilio chenu. Nakala kwa Mkuu wa mkoa makonda.
Wadau tumekubaliana tuanzie ngazi ya chini kwa mtendaji wa kata pamoja na diwani halafu kama hatujalizishwa na maelezo yao juu ya ufunguzi wa soko la kinyerezi tutaenda ngazi za juu zaidi.
Una ushauri gani juu ya huu uamuzi wetu ndugu?
 
Back
Top Bottom