Kutokana na report ya CAG ya mwaka 2025 hivi ndivyo mashirika ya Uma yanavyonufaika na 4R za Mh Rais wetu mpendwa.
1.TTCL wao wameona namna nzuri ya kunufaika na 4R za Mh Rais ni kupandisha hasara kutoka billion 4.32 mwaka 2022 hadi billion 27.7 mwaka 2023.
2.TRC wao wameupiga mwingi zaidi na kuitumia vizuri hii fursa ya 4R za Mh Rais Samia na kupandisha hasara kutoka billion 102 mwaka 2022 hadi billion 224 mwaka 2023
3.ATCL Hawa licha ya kununuliwa ndege , kupewa ruzuku na kupewa mazingira mazuri ya kufanya biashara lakini wakaona haitoshi ngoja na wao wasibaki nyuma kwenye fursa ya 4R za Mh Rais wetu, kwa hiyo wakapandisha hasara ya shirika kutoka billion 56.6 ya mwaka 2022 hadi kufikia bilioni 91.8 mwaka 2023
Kuna kitu hakiko sawa mahali,ninavyojua Mimi,cost ya service ikiwa kubwa basi na demand iwe top maximum,demand inapokuwa top maximum lazima kutakuwa na super normal profit,Mazingira ya Biashara Tanzania ni ya kkma sana,yaani watumiaji wa luxury good ni Wana siasa pekee sababu ndo kundi liko huru kutumia asali ya nchi hii sababu ya super incentive wanazopata,ukija kwa mtumishi wa kawaida hana pesa ya likizo sababu ya utapeli wa serikali ya Tanzania kisa Miradi ya kimkakati.Shbiby ameenda kuwekeza pale Morogoro lakini amekaba mnyororo wote wa thamani kwa majirani zake sababu yeye ni mwanasiasa,sasa kwa mtumishi wa kawaida bila annual bonus ya maana hawezi kukata tiketi ya ndege ili uende bukoba kupeleka watoto kwa bibi,hii hapa inaleta ukakasi mkubwa na kusababaisha mkanganyiko mkubwa kwa Miradi pendwa ya ATCL.
Ujinga huu huwezi kuta nchi zilizoendelea,unakuta nchi ni maskini na akili nayo ni ya kimaskini,inakuwaje watu nchi nzima tunahangaika kufanya kazi kwa bidii wakati hata masoko ya hizo bidhaa sii ya uhakika?
Tujitahidi sana kuongeza thamani ya bidhaa hapa nyumbani ili Kodi ikusanywe na hili toto jinga Znzbr tunalolipa asilimia kumi ya mapato ni wakati sasa lianze kujitegemea limeshaota mvua za ukoo hili toto.
Tokea nimejua kuwa soko la bidhaa za mashamba halina uhakika nimekuwa na hofu ya kubwa kwanini Miaka lukuki tunakopa na wakati mazao ya wakulima yako mengi ila soko hakuna,tunashindwa vipi kuchukua pesa za psssf na kufungua Kampuni kubwa ya uwindaji na kununua mitambo ya kuchakata na kuchimaba madini.
Tunakuwa na akili gani kukosa boti Kali za safari ya kifahari kati ya miji ya Msumbiji,Mtwara na Tanga kuwatembeza watalii wanaojitambua.Hebu tuwe wawazi tunafeli sana kutowekeza kwa nguvu kwenye uvuvi,huwezi amini kwa sasa hakuna samaki mikoani yate wa baharini kwa wingi kama mahitaji yalivyo,ukienda hoteli zote utakula tilapia lakini huwezi kula blue fish 🐟 sababu mkiwa miasaba tuu kwenye kazi samaki wa bahari hawatapatikana kukidhi haja hiyo.
Ukija kwenye siasa Kuna dude Moja limetukaba toka uhuru lakini hawana nia ya dhati kifuta bomu la ajira kwa vijana hapa nchini,ilianzishwa BBT imetelekezwa imebakia kiasi kidogo tuu na kwa watoto wa wakubwa tuu,tunaomba Miradi hii iwafikie wote wenye uhitaji.Dude hili liko pale kama mkoloni wa ndani,huwezi achia bidhaa za gesi zitoke nje mfano mbolea wakati Traole kaonyesha mfano na sasa watu wanaiona Burkina Faso kama malaika sababu siasa chafu zimewekwa kando na mwamba wa Afrika huyo aliona fursa na kuifanyia kazi.
Tafadhali sana,tunakusanya Kodi kubwa sana lakini hizi mambo za kutembea nchi nzima na highway zenye single lane ni aibu kubwa tunaomba Barabara pana na ziwe njia nane au sita,Mbona kutoka Toronto kuelekea america wameweza kwani mnafikiri dhurma ikiwekwa kando sisis hatuwezi,kila mtu afanya kazi na apate haki yake,mnamuaona Traole alivyoweza mnafikiri ni ndoto Tafadhali sana tunaomba nchi isonge mbele,kama ccm wamaeshinda na hawafanyi jambo la maana piga chini,ni aibu Jiji la daresalamu watu Wanafanya kazi lakini Jiji zima ni chafu na hakuna maisha yanayofanana na hardworking ya watanzania,kila mtu afaidi matunda ya uhuru au laa basi sisi ni maskini wa kwanza hapa afrika wenye resources zote,tunaomba masoko ya bidhaa za kilimo yawe ya uhakika na thamani iongezwe hapa Tanzania.Na sio kidumu kile kidude cha nyani na fikra zake wakati njaa Iko kila Kona.