Namna hirizi ilivyookoa penzi langu

Mnyenz

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
1,413
4,289
Habari zenu wakuu!
Nimekutana na thread humu ikizungumzia namna mganga alivyomtapeli baba ya mtoa mada m20+, lakini kilichonivutia kuanzisha sired yangu ni comment ya memba mmoja ambae anasema hakuna uchawi, mtu unaweza fanya ujanja tu na mambo yakajipa.

Niseme tu na mie nilifanya ujanja ujanja nikaokoa penzi langu lililoingiliwa na mtu mzima hovyo.

TWENDE PAMOJA:

Ukitaka kucheza na akili ya mtu ni kitu simpo tu.

Nakumbuka miaka flani nyuma kuna mzee mmoja mkuda mtaani alikua hapendi mahusiano yangu na demu flani hivi. yaani yule mshua alikua mkuda to the maximum, akawa anasambaza maneno ya hovyo sana mtaani kunihusu.

Mwanzoni nilimdharau tu ila baadae nikaona hii ishu inakua siriaz, nikaamua kumuuliza demu akasema yule mzee alishamtaka akamtolea nje, nikaona ok kumbe ni wivu tu(in gwajima voice)

Basi nikakaa chini nikaona iweje huyu mume mwenzangu anipande kichwani? Nikapanga mipango ya kibedui kumuhusu, baada ya mipango yangu kukamilika nikatengeneza mazingira ya kumjaza na kweli mzee wa watu bila kujua akajaa.

Siku aliyojaa kwenye rada nikamchana ile mbaya, katika majibizano(kufokeana) nikawa narudia sana maneno haya "WEWE MZEE DAWA YAKO IPO JIKONI, LAZIMA UKOME KUNIFUATILIA" kumbe mie ninamwekea mtego tu, baada ya kuhakikisha ujumbe umefika nikaondoka zangu pasi na yeye kujua mimi nina mpango kabambe.

Baada ya siku tatu mie nikaenda bondeni, nikamkamata chura, nikachukua vitambaa viwili(chekundu na cheusi) nikaviShona kwa sindano kisha nikamtumbukiza yule chura halafu nikashona pooote pasi na kuacha tundu.

Alfajiri tu Mie huyooo nikabeba ki paseli changu cha chura na unga wa sembe mpaka mlangoni kwa yule mzee, nikaweka kale ka mzigo kangu ka chura kimya kimya(kama wafanyavyo wale jamaa wanaopeleka bahasha kwa wahusika/ ref video ya mbosso Nadekezwa) halafu nikachora na duara kwa kutumia ule unga(chura akawa katikati) mie huyooo nikasepa kimya kimya.

Oyaaa unaweza kufanya kitu kwa nia ndogo lakini madhara yakaja makubwa, yaani mtaa mzima ulijaa pale kwa mzee, stori ni hirizi imeonekana inapumua, hakuna aliyetaka kuigusa wala kusogelea.(yaani nilifanya simple tu ila nikawa full mchawi hahahhaaha)

Ile habari ilivuta watu mpaka mitaa ya jirani, tukajikuta tumepata watalii wa kutosha mtaani. Hhahahaaaaa!

Yule mzee aliteseka sana na lile tukio mpaka akawa anaenda kwa waganga.

Baada ya kama wiki ndo nilikuja kuonana nae, nikamsalimia akasonya tu, mie hapo kimoyomoyo nasema dawa imekuingia.

Akawa analeta waganga mpaka pale kwake kuja kuagua, mie namcheki tu halafu nasema hiiiiiiiii bagoooshaaa!, heshima ikafuata mkondo wake na nikawa dizain naogopwa mtaani.
 
Baada ya kama wiki ndo nilikuja kuonana nae, nikamsalimia akasonya tu, mie hapo kimoyomoyo nasema dawa imekuingia.

Akawa analeta waganga mpaka pale kwake kuja kuagua, mie namcheki tu halafu nasema hiiiiiiiii bagoooshaaa!, heshima ikafuata mkondo wake na nikawa dizain naogopwa mtaani.
hahahaha uwiiii umechekesha mkuuu yani hapa nilipo sina mbav, sasa baada ya mzee kuleta waganga hakugundua kuwa ulikuwa unamtisha? na je watu wote mtaani walijuwa kuwa ww ndo ulipeleka ile chura?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom