Namna chandarua kinavyoua nguvu za kiume

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Kuna watu wengi ambao hawapendi kutumia vyandarua kwa dhana kuwa huwa vinamaliza nguvu za kiume, dhana hii ni kweli lakini kwa namna kama ifuatavyo: Tendo la ndoa hasa kwa wanafamilia (couple) waliyodumu kwa muda mrefu pamoja huwa linahitaji mazingira tulivu yasio na vurugu, maudhi, uchovu, msongo wa mawazo, mikwaruzo/kuguswa na kitu chochote, harufu chafu wala kelele za vitu vingine ambazo zinaweza kuhamisha concentration/focus ya wanandoa kwenye tendo la ndoa.

Zoezi la utumiaji vyandarua hasa vijijini huwa linakumbwa na changamoto zituatazo:

1. Vyandarua vya misaada kutengenezwa kwa nyuzi nzito za nailoni ambazo zinakwaruza zinapogusa ngozi ya mtumiaji
2. Vitanda vyembamba vya kuanzia upana wa futi 1.5 hadi 2.5 na vya kamba vinavyotumiwa na wanavijiji wengi.
3. Idadi kubwa ya watu wanaolala kwenye kitanda kimoja (mama, baba na mtoto mdogo)
4. Hafuru ya dawa iliyopakwa kwenye chandarua.

Hali kama hii hapo juu inasababisha chandurua kigusane na ngozi ya mtumiaji kutokana na udogo wa kitanda, ukosefu wa godoro la kuchomeka chandarua na idadi kubwa ya wanaolala kwenye hiki kitanda kidogo. Chandarua kugusa na kusugua ngozi ya mgongo wa baba kunaongezeka wakati baba anapokuwa kwenye tendo la ndoa (up and down) kiasi cha kusababisha ghasia itakayosababisha kuhamisha hisia za baba kuendelea kufanya tendo la ndoa. Harufu kali ya dawa ya chandarua inayogusa pua za wanandoa inabadilisha kabisa mandhari ya kitandani na kuwafanya wanandoa waanze kupiga chafya na harufu ya manukato yao kupotea kabisa na kuhamisha kabisa fikira za tendo la ndoa kwenye mawazo yao. Hali hii inamaliza kabisa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa wanandoa hasa wanaume ambao ni rahisi sana kuathirika kwa ghasia na vurugu za aina hii.

Tunapowapa wananchi wa vijijini vyandarua vya misaada tusisahau pia kuwapa elimu ya kutosha na kuwasaidia pia vitanda na magodoro ya kufunga vyandarua hivyo. Tuangalie material yanayotumika kutengenezea vyandarua hivi ambavyo sio rafiki vinapogusa ngozi ya mtumiaji (inachoma). Ama kweli rahisi ni ghari sana kwa wanandoa, ndio maana wanavibadilishia matumizi.
 
010fb8f1a1134d25103feeac898b249a.jpg
 
Nilivosoma heading nikakimbilia chandarua changu na kukiwasha moto
Wakati moto unaunguza Hilo takataka nikawa nasoma hii kitu
Hata cjamaliza kusoma niko kuzma moto sasa
 
Then you choose! Malaria vs heavy sexual enter-course
Malaria itaendelea kusumbua mkuu, maana chandarua inapogusana na ngozi ya mtuamiji (kitanda futi 2 watu 2 na mtoto) ina maana kuwa mdomo wa mbu (proboscis) wanaifikia damu ya wanafamilia na kufanya vitu vyao kiulaini kabisa.
 
Back
Top Bottom