Namna bora ya kukata roho

Namna bora ya kukata roho

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,102
Reaction score
828,984
Kifo ni mwanzo sio mchakato. Once roho inapoachana na mwili husafiri mamilioni ya kilometers kwenye utupu wa dunia. Ni kama imetoka kifungoni na sasa iko huru. Roho ndani ya mwili uwezo wake huwa wa mipaka mno. Ni mpaka mtu afanye juhudi za kufungua jicho la tatu ndio kidogo unaweza kuona zaidi ya kuona.

Kiingereza tunasema seeing beyond. Bila kujali roho itasafiri kwenda wapi mautini ama katika uhai bado kuna muunganiko usiokoma na mwili husika, hivyo daima hurejea. Watu wale walionusurika vifo, yani wale waliofika hatua ya umahututi. Katikati ya kifo na uzima, wakizinduka hukwambia kwamba wameota ama waliona wanaenda mbali sana. Mbali kabisa angani ama chini ya dunia kusiko na mwisho ama tambarare isiyo na ukomo.

Wanaenda tu lakini hawafiki na walikuwa wanasikia sauti kwa mbali zikiwaita warudi. Kifo ni mwanzo sio mchakato. Death is the state not the process.
journey.jpg

Kila roho ina asili. Ina makazi asili na makazi mbadala, makazi ya muda ama makazi ya kupita
Mwezi uliopita mwishoni tulipoteza kijana wetu ofisini alianguka umbali wa mita tano toka juu na akatua kwenye zege. Nilikuwa naye mpaka anakata roho. Tulifanya juhudi mbalimbali za kuokoa maisha yake. Tukamkimbiza hospital ya mkoa na baadae Muhimbili kwa ambulance

Muda wote huo niliona alivyokuwa akipambana roho isimuache. Niliingia ulimwengu wa roho kimyakimya kumsaidia uhai, mapambano. Ni kupitia huko nilimuona akielea mbali kabisa na mimi. Alikuwa mwepesi na mwenye kasi ya ajabu. Nilirudi kimwili na kumuona akijaribu kupepesa macho huku madaktari kwa juhudi kubwa wakifanya hand pumping, mashine ilikuwa imeshashindwa kazi.

Nilianza kuchant mantras za mwisho mwema. Nkachant Krishna, nikachant kuan ing pussa. Dakika kumi baadae akapumzika kwa amani. Hana mateso tena. Tunafanya makosa mengi na kushindwa kuwasidia wapendwa wetu kukata roho salama. Kumbuka hata sekunde zile za mwisho unaweza kumsaidia marehemu akawa na mwisho mwema. Kuna vita ya kiroho muda ule, kuna uvutano wa hasi na chanya, kuzimu na mbingu.

Ukiwa mtulivu unaweza kumsaidia asiende upande mbaya I mean roho yake. Sanasana ni roho kutoka na kwenda kuripoti kwenye makazi yake asilia kisha kurudi kwenye makazi yake duniani. Tunaita blissful state. Ukikosea kidogo ana hata yeye mwenyewe basi roho yake huwa ya kutangatanga bila ya kuwa na kikao maalum na kuleta shida kubwa.

Ibada za mwisho kabla ya kukata roho ndio tunazozifahamu zaidi, lakini tukumbuke kuna ibada nyingi tofauti ambazo huwa msaada mkubwa kwa marehemu. Sehemu nyingi za ajali na majanga, tunapoona watu wakikata roho ni sehemu sahihi za kufanya ibada za binafsi sirini, ibada za kuingia ulimwengu wa roho kimyakimya kwenda kutoa msaada wa kuomba njia sahihi kwa wale wafao.

Najua sijaeleweka ngoja jukwaa letu lianzishwe tutaeleweshana zaidi

Jr
 
Si kweli huu ni upotoshaji wa shetani ili watu wengi wapotee na wasiende mbinguni na wasimtumainie Mungu

Duniani kuna nguvu mbili tu ya Mungu na ya shetani yaani ya wema au ubaya

Ili kwenda mbinguni inakubidi uwe chini ya nguvu ya Mungu na hakuna yeyote anaeweza kwenda kwa Mungu bila kujitoa kikamilifu kwake na haikuhitaji kufanya chochote cha ziada ili kuwa kwake ila kila kitu kimeshaandaliwa kwa wote wanaokubali kumtii

Hayo mengine ni mbinu za shetani kuwapa watu matumaini ya uongo ili waweze kujitumainia wenyewe na mwisho wafe ktk dhambi zao na kuangamia ktk moto siku ya hukumu

Kwa mujibu wa biblia mtu anapokufa anarudi ktk hali aliyokuwa nayo ya kutojifahamu kabla hajazaliwa hadi atakapofufuliwa tena kwa ajili ya hukumu ndipo atakapopata tena fahamu na kwenda motoni au mbinguni kupo chini ya Mungu yaani siku ya hukumu tambua hakuna binadamu ama roho yoyote inayoweza isaidia roho nyingine kwenda popote pale mbinguni ama motoni hizo ni porojo za shetani
 
Kwa muktadha wa Bible takatifu uko sahihi kabisa na nakubaliana nawe kwa asilimia mia moja lakini dunia hii ni zaidi ya uijuavyo
Kuna imani nyingi kuna dini nyingi na nyingine ni za ajabu hasa.... Nakushauri jifunze tu ujue lakini si lazima uamini au u practice... Mungu akurehemu

Jr
 
Back
Top Bottom