Namibia yakataa fidia ya mauaji ya kimbari iliyotolewa na Ujerumani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Namibia Hage Geingob amekataa kupokea fidia iliyotolewa na Ujerumani kwa ajili ya mauaji ya kimbari wakati wa ukoloni.

Jeshi la Ujerumani liliuwa mamia ya maelfu ya watu wa jamii ya Herero na jamii ya Nama kati ya mwaka 1904 na mwaka 1908, wakati wa ghasia za kupinga ukoloni.

Inadaiwa pia kuwa asilimia sabini na tano (75%) ya idadi ya watu wa Herero na nusu ya idadi watu wa Nama waliuawa.

Nchi hizo mbili zilianza majadiliano juu ya fidia ya kimbari tangu mwaka 2015 na tayari wamekuwa na mazungumzo mara nane hadi sasa.Rais Geingob alikuwa anatoa muktasari wa majadiliano hayo kati ya timu ya majadiliano ya Namibia na wawakilishi kutoka Zed Ngavirue.

"Fidia iliyotolewa sasa na serikali ya Ujerumani bado haijakubaliwa na serikali ya Namibian," taarifa kutoka kwa Rais ilieleza . Aidha hakukuwa na maelezo zaidi yaliyotolewa kufafanua uamuzi huo.

"Ujerumani imekubali kuomba radhi lakini imekataa kufikia maafikiano kati yao ya kuuguza majeraha waliyoyaacha”, taarifa hiyo iliongeza.

Ukurasa wa Twitter wa ofisi ya rais wa Namibia uliweka picha ya rais Geingob na Ngavirue .

BBC Swahili
 
Ila wajerumani ni kama Wana vinasaba vya kutekeleza mauwaji ya kimbari....kwanzia kwa waafrika hadi kwa wayahudi.

Hata huku Tanganyika walifanya maasi makubwa mno....afadhali walivyopoteza vita zote za Dunia.
 
Hata huku Tanganyika inabidi watulipe fidia kwa utawala wao wa kikatili enzi za ukoloni bila kusahau Vita vya maji maji.
 
Sasa hata ukizikataa, hizo pesa unapata faida gani, kwani kama ni kuteswa ulisha teswa tu!!! Bora uchukue tu mjengee hata mahospitali, mashule potelea pote
Hapo ni zaidi ya mali. Unaweza kukataa kwa sababu za kitaifa. Unaweza kukubai fedha kumbe ikawa kujidhalilisha tu. Hii ndo ukisikia masikini jeuri.
 
Namibia rejected German colonial Compensation offer. Deutschland was prepared to give ten million euros as reparation. The proposal for crimes in the colonial Era was turned down as unacceptable by the Namibian government. The reason is obviously not the money alone.

Namibia was categorical in their dismisal of an offer of compensation from Germany in the negotiations to come to bring closure to the colonial era. For President Hage Geingob, paying ten million euros in reparation is still “unacceptable,” the newspaper “The Namibian” quoted the president’s advisor, Alfredo Hungary.

Geingob himself tweeted that he had been made aware of the status of the discussions and had proposed that the negotiations continue. “We remain determined in completing this key mission,” he wrote.

Among other things, the designation of the compensation as reparations is controversial. Geingob stated that the federal government opposes the use of the term because it had also been avoided in Berlin’s negotiations with the Israeli government on reparations for Holocaust victims.

Geingob rejected an alternative term suggested by the federal government. The terminology will therefore remain the subject of the negotiations, declared Namibia’s head of state.

Berlin and Windhoek have been negotiating an agreement since 2015 which, in addition to an official German apology for the colonial crimes, should also contain commitments for development aid.

Between 1900 and 1910, thousands of members of the Nama and Herero ethnic groups were massacred by German troops under German colonial rule in what is now Namibia. Historians rate the massacre as the first genocide of the 20th century.

Germany has acknowledged that there were atrocities during colonial rule. So far, there is no official apology or compensation for it.


Namibia rejects German colonial Compensation offer | Lion Net News
 
Back
Top Bottom