salthanks
JF-Expert Member
- Aug 5, 2016
- 3,284
- 6,845
Umeongea sahihi mkuuSoma historia ya Dubai. Ilikuwa na hali mbaya kuliko ya kwetu lakini mabadiliko makubwa sana yalitokea ndani ya miaka 15. Na katika hiyo miaka 15, kila mwaka, kuanzia mwaka wa kwanza kulikuwa na miradi mikubwa yenye impact kubwa iliyofanyika.
Uchumi wa Tanzania bado ni mdogo sana. Hata ukizuia wizi kwa 100%, mapato yote yakusanywe kwa usahihi, bado itaendelea kuwa maskini. Mkazo mkubwa ungeelekezwa kwenye uwekezaji na uzalishaji. Hakuna nchi ambayo hakuna wizi. JPM hata afanye nini hawezi kuufuta wizi moja kwa moja. Hilo ni zoezi endelevu, huwezi kusema nimalize kwanza wizi ndiyo nianze kushugulika na sera za sustainable development. Vitu vingi anavyoshughulika navyo vinahitaji process endelevu lakini yeye anafanya kama vile vinahitaji jitihada zenye ukomo.
JPM hawezi kuifanya Tanzania iwe imeendelea kwa kulala na kuamka bali tunatakiwa tuone kila mwaka tunapiga hatua toka wapi kwenda wapi.
Uwekezaji umeongezeka toka kiasi gani mpaka kiasi gani? Lakini chini ya utawala wake uwekezaji umeanguka toka 26.8% mpaka kufikia 3.8%.
Unemployment imepungua toka ngapi mpaka ngapi? Taarifa zilizopo ni kuwa unemployment imeongezeka.
Exports zimeongezeka toka ngapi hadi ngapi? Nazo kwa taarifa za BOT zimeshuka.
Performance ya sekta moja moja za uchumi na huduma, zimekua kutoka wapi mpaka wapi? Taarifa za BOT zinaonesha kila sekta imedondoka katika volume au katika ukuaji.
Kama katika vigezo vyote vya upimaji wa maendeleo, tunaenda chini, ni muujiza gani utakaotokea ili baada ya miaka 5 au 10 ya JPM tushtukie tuna maendeleo? JPM kama anataka kutoa mchango wa maendeleo kwa Taifa hili aache siasa za umaarufu, afanye kazi kwa kiwango kikubwa cha kutumia akili. Dunia ya leo, maendeleo hupatikana kwa werevu, siyo kwenye majukwaa ya mikutano, hizo ni siasa za zamani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app