Namhurumia yeyote atakayesimama kugombea urais na Magufuli 2020

Naomba kuuliza swali....na nnaomba majib yenye akil,sio bla blaa,...."kwanin watu wasimchague magufuli 2020"..ni ubaya gan haswa aliofanya asistahili kuchaguliwa.
 
Kwa jinsi anavyopiga kazi lazima mtu aambulie aibu. Mwaka mmoja na nusu wa utawala ameishangaza dunia utadhani ametawala miaka 20. Hongera sana rais wetu. Tulitaka rais wa aina hii.
huna haya unajitekenya na kucheka mwenyewe,kwa taarifa hata saa 3 asubuhi hafiki atakanyagwa mbali
 
Naomba kuuliza swali......,kwanin watu wasimchague jpm?..naomba majibu
Hakuna matokeo chanya ya anachokifanya kwa maisha ya wananchi wa kawaida. Ana dhamira nzuri lakini hana mbinu sahihi. Wakati wote kinachotazamwa ni matokeo, siyo unachokifanya.

Uchumi ni sayansi ambayo wale tu walio werevu hufanikiwa. Uchumi haujengwi kwa kuongea sana kwenye majukwaa au kwenye TV bali hutegemea zaidi mipango na mbinu sahihi ambazo huwezi kuzipata kwenye majukwaa ya mikutano.

JPM ni Rais, anatakiwa kuleta matokeo lakini anafanya kazi kama mtu anayezunguka kutafuta kura. Anatafuta short term simple popularity badala ya kutafuta sustainable popularity.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko wrong bro,..nchii hii ilikua imeoza,ilikua haitekelezek,budget kubwa makusanyo hafifu,ufisad kila kona,kuanzia mwalim wa shule ya msingi had raisi..for 50yrs,.hiv unabadilishaje mambo mazito ambayo yatamfikia had mtu wa kijijin maskin in a short period?

ulitaka awajaze watu pesa mifukon kwa kaz gan hasa tunazofanya wa tz?production ni poor,no export,utalii poor,madini sheria za hovyo kabsa,siasa ni vijembe,matusi etc,maofisin ni business as usual,watu hawafany kaz ni mazoea tuu,.labda kidogo sekta binafsi inajitahid.

sasa pesa extra unaitoa wap ya kuwajaza watu mifukon,akat nchi yako kikubwa inachofanya ni shugul za kutoa service tuu na hakuna production wala exportation ya goods,bandari uozo mtup,ufisad kila siku tunaona,umeme huko ma escrow,na bdo nchi haina afya nzur,dawa hakuna etc,maisha duni,hiv unarekebishaje nchi kwa mda mfup haya yote,tusiongee tuu kwa jazba tuseme ukwel
 
Yaani hata miaka 5 haijaisha mshaanza kuwaza uchaguzi, ni sawa na mtoto anayekula chakula, sahani hata haijafika nusu anaanza kuwaza chakula cha jioni... Ulafi na uchu wa madaraka! Wekeni tume huru tuone.
 
Kwa jinsi anavyopiga kazi lazima mtu aambulie aibu. Mwaka mmoja na nusu wa utawala ameishangaza dunia utadhani ametawala miaka 20. Hongera sana rais wetu. Tulitaka rais wa aina hii.
Ni kweli tunaona alivyoshughulikia sukari hadi saivi tunanunua kwa bei nafuu kabisa, vijijini kwetu ameshamwaga milioni hamsini alizoahidi pia tusisahau alivyofuta kodi na maushuru mbalimbali kama alivyoahidi wakati wa kampeni. Itakumbukwa pia ameimarisha demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari, deni la taifa ni kama limeisha kabisa huku wananchi wakiwa na unafuu mkubwa wa maisha. Tumpongeze!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko wrong bro,..nchii hii ilikua imeoza,ilikua haitekelezek,budget kubwa makusanyo hafifu,ufisad kila kona,kuanzia mwalim wa shule ya msingi had raisi..for 50yrs,.hiv unabadilishaje mambo mazito ambayo yatamfikia had mtu wa kijijin maskin in a short period?

ulitaka awajaze watu pesa mifukon kwa kaz gan hasa tunazofanya wa tz?production ni poor,no export,utalii poor,madini sheria za hovyo kabsa,siasa ni vijembe,matusi etc,maofisin ni business as usual,watu hawafany kaz ni mazoea tuu,.labda kidogo sekta binafsi inajitahid.

sasa pesa extra unaitoa wap ya kuwajaza watu mifukon,akat nchi yako kikubwa inachofanya ni shugul za kutoa service tuu na hakuna production wala exportation ya goods,bandari uozo mtup,ufisad kila siku tunaona,umeme huko ma escrow,na bdo nchi haina afya nzur,dawa hakuna etc,maisha duni,hiv unarekebishaje nchi kwa mda mfup haya yote,tusiongee tuu kwa jazba tuseme ukwel
Soma historia ya Dubai. Ilikuwa na hali mbaya kuliko ya kwetu lakini mabadiliko makubwa sana yalitokea ndani ya miaka 15. Na katika hiyo miaka 15, kila mwaka, kuanzia mwaka wa kwanza kulikuwa na miradi mikubwa yenye impact kubwa iliyofanyika.

Uchumi wa Tanzania bado ni mdogo sana. Hata ukizuia wizi kwa 100%, mapato yote yakusanywe kwa usahihi, bado itaendelea kuwa maskini. Mkazo mkubwa ungeelekezwa kwenye uwekezaji na uzalishaji. Hakuna nchi ambayo hakuna wizi. JPM hata afanye nini hawezi kuufuta wizi moja kwa moja. Hilo ni zoezi endelevu, huwezi kusema nimalize kwanza wizi ndiyo nianze kushugulika na sera za sustainable development. Vitu vingi anavyoshughulika navyo vinahitaji process endelevu lakini yeye anafanya kama vile vinahitaji jitihada zenye ukomo.

JPM hawezi kuifanya Tanzania iwe imeendelea kwa kulala na kuamka bali tunatakiwa tuone kila mwaka tunapiga hatua toka wapi kwenda wapi.

Uwekezaji umeongezeka toka kiasi gani mpaka kiasi gani? Lakini chini ya utawala wake uwekezaji umeanguka toka 26.8% mpaka kufikia 3.8%.

Unemployment imepungua toka ngapi mpaka ngapi? Taarifa zilizopo ni kuwa unemployment imeongezeka.

Exports zimeongezeka toka ngapi hadi ngapi? Nazo kwa taarifa za BOT zimeshuka.

Performance ya sekta moja moja za uchumi na huduma, zimekua kutoka wapi mpaka wapi? Taarifa za BOT zinaonesha kila sekta imedondoka katika volume au katika ukuaji.

Kama katika vigezo vyote vya upimaji wa maendeleo, tunaenda chini, ni muujiza gani utakaotokea ili baada ya miaka 5 au 10 ya JPM tushtukie tuna maendeleo? JPM kama anataka kutoa mchango wa maendeleo kwa Taifa hili aache siasa za umaarufu, afanye kazi kwa kiwango kikubwa cha kutumia akili. Dunia ya leo, maendeleo hupatikana kwa werevu, siyo kwenye majukwaa ya mikutano, hizo ni siasa za zamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom