Namchukia Jakaya Kikwete

jamani mimi nilimchukia tangu alipofanya mkutano na wazee na kusema "Lowasa kujiuzulu ni sawa na ajali kazini" mpaka leo simpendi kabisa; akanizidishia uchungu alipowakampenia ubunge mafisadi; ... hapo alinimaliza kabisa. Sasa tegemea waziri mkuu kuwa Lowasa au atapewa wizara nyeti....... ndipo utakapojua mkwere hamnazo!!!!!!!!!!!!!!!!!...
 
:caked: mimi nikisikia jina hilo napata kiungulia ghafla sijui kwanini ,sisi tumetimiza haki yetu ya kupiga kura,alicho fanya yeye anakielewa na Mungu wake,yeye sio malaika,wako wapi Kamuzu banda wa malawi? ( The life president) alijiita rais wa maisha,kila chenye mwanzo kina mwisho wake,Tanzania sio shamba la mjomba au chuma ulete ipo siku ya hao mafisadi ambayo mungu amepanga ya kuwang'oa
 
Kipindi cha Mkapa ilikuwa balaa wana CCM wote walikuwa wanakaa kimya.

What about SIMU 2000? Kiwira huko?

Well lakini Mkapa atleast alituachia barabara tunamshukuru kwa kuiunganisha nchi kwa mtandao mpana wa barabara na kutuletea wawekezaji kwenye madini kama vile Barrick na wengine ambao wamesaidia kuongeza makusanyo ya kodi.

KIla kiongozi ana mabaya na mazuri yake!
 
Lakini wapo wanaompenda!
Ni kweli na hao ni, "Wezi wa mali ya umma, wabadhirifu wa mali ya umma, wavivu, wapenda anasa, walanguzi, wakwepa kodi, majambazi, ombaomba, wapenda matanuzi ughaibuni, wanaojilimbikizia mali ya haramu, wadini, wabaguzi, na kundi kuuubwa la majuha."
 
NAJUA ANAJUA KWAMBA namchukia big time.
nina sababu nyingi sana za kutopenda style yake ya utawala. naona mengi mmeyapost hapa
 
I hate him so much. I do no how much i hate him. Please God be with me . forgive me for hating him.
 
Labda hujui chuki yako inasababishwa na nini!!!!!! lakini jiulize vizuri moyoni na utagundua ni DHAMBI ya udini ndio inayokutesa. hakika wale wote waliopandikiza dhambi hii kupitia madhabahu wanatakiwa kuteketezwa kimyakimya kwani mbegu walioipanda haitakiwi kuota na kutokeza juu ya ardhi ya watanzania... kama unadhani nakuonea,,,,,, naomba nikosoe kwa huu ushahidi hapa chini.....
NANI ADUI YETU??? MKAPA au KIKWETE????
1.Maliasili(misitu, madini, samaki na wanyamapori) vilianza rasmi kuvunwa chini ya serikali ya MKAPA kupitia mikataba isiyo na tija kwa taifa ambayo tunailalamikia hadi leo.kabla ya hapo hapakuwa na uvunaji wa kiwango hicho.

2.ELIMU nayo ilisambaratika katika utawala wa MKAPA(Kumbuka sakata la ubadilishaji wa mitaala),matumizi ya vitabu tofauti katika mashule,ufutaji wa michezo shuleni, kuzipigia chapuo shule binafsi na kuzinyima ruzuku shule za serikali.

3.USAFIRISHAJI nao ulisambaratishwa kwa makusudi kipindi cha MKAPA kwani ATC,TRC,THA,TTBSLTD, KAMATA na UDA Vilimalizwa na vimeshindwa kurudi hadi leo.

4.MWASILIANO JE???? Kila mtanzania ni shahidi wa jinsi MKAPA na serikali yake walivyolifilisi shirika la simu TTCL na jinsi ambavyo wametumia ghilba kuiondoa CELTEL-(SASA ZAIN) kutoka mikononi mwa TTCL na kuwa mali ya kikundi kidogo cha watu.

5.NISHATI NAKO VIPI????? mnakumbuka IPTL?? Ni kipindi cha uongozi wa MKAPA ambapo TANESCO WALIINGIA MIKATABA YA KIFISADI iliyochangia kuyumba kwa kiasi kikubwa sana kwa TANESCO mpaka kupelekea kashfa nyingine kama za Richmond.

6. KUHUSU MAJI???? NI edward lowwasa aliyefuta mikataba ya kifisadi kati ya wadau na wawekezaji(kumbuka kasheshe la DAWASA kuvununja mkataba na wawekezaji)lakini upuuzi wote ulifanyika chini ya MKAPA.

7.MAADILI ya watanzania kama taifa yaliingia kwenye majaribu kusamabaratika kipindi cha MKAPA
8.Kuhusu UFISADI ndio usiseme kabisaaaaaa,,,,, kwani DEEP GREEN,MEREMETA,EPA,KAGODA NA UUZAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI uliratibiwa na kutekelezwa chini ya serikali ya MKAPA.
9. KUHUSU ULINZI NA USALAMA,,,, ni kipindi cha mkapa ambapo polisi na wahalifu walikuwa wakisaidiana katika kazi zao kiasi cha askari kuwa walinzi wa wanyan'anyi na wananchi wakibaki hawana usalama,
nahitimisha kwa kusema!!!!!! mwindaji akienda porini na mbwa wake kwa ajili ya kuwinda, ni mbwa anayefanya kazi ya kunusa ,kumkimbiza ,mpaka kumkamata mnyama, mwindaji atakachofanya ni kuchinja mnyama na kubeba nyama kwenda nyumbani ambapo pamoja na rafiki zake na wanafamilia watakula nyama yote na kubakiza mifupa na makombo kisha humtupia mbwa. naye mbwa ataona amethaminiwa na ataonyesha furaha yake kwa kutingisha mkia kwa shukrani.
mkapa amewaachia uwanja wa mpira na daraja la mto rufiji kama makombo ili wale wenye silka za mbwa watingishe mikia kwa furaha wakati minofu yote(nishati,madini,maliasili, misitu,viwanda,mawasiliano) amekula yeye,familia yake na marafiki zake,

sikukatazi kumchukia KIKWETE,,, ila nawe tuambie ukiambatanisha na ushahidi juu ya nini kibaya alichoifanyia hii nchi zaidi ya mema na jitihada za kurekebisha yale aliyoharibu MKAPA.
Kama utaruhusu imani(imani za mapokeo ya kikoloni) ziuathiri ubongo wako kiasi cha kushindwa kuona ubaya wa MKAPA kwa sababu tu muumini mwenzako na kumchukia KIKWETE eti kwa sababu ya tofauti ya imani,, basi wewe utakuwa mtumwa wa kifikra wewe na kizazi chako chote.


Ni Sawa na kulinganisha Mafuta na Maji!!
 
Kwa hilo mkuu mimi kama ningekuwa na mshiko wa kutosha ningahamia hata nchi nyingine. Sielewi kwanini hawa jamaa wameamua kututawala kwa nguvu wakati siye hatuwaependi. mungu sikia kilio chetu, sisi wanao tunateseka katika nchi yetu. JK na wazee wenzake akina Kiravu na lewisi makame wamechakachua kura zetu ili waendelee kupata umaarufu. Wakati viwanda vyetu wameiba
 
Boby umezungumza vema, mie nadhani hawa jamaa wanaowachukulia hatua viongozi wa nchi wanaohimiza mauaji kama walivyofanya kwa Sadam nadhani ni wakati muafaka wa kuangalia marais wanaofanya makusudi kuua watu wasiokua na hatia. Kuua sio lazima apeleke jeshi likawapige risasi, sio lazima ahimize kikundi kama Mungiki kikafanye mauaji..ila anapokua anafuja hela za nchi na kuacha kuimarisha huduma kama za afya na kusababisha watu hasa watoto na akina mama kufariki dunia kwa kukosa huduma ni uaji mbaya zaidi. Wanafanya mauaji kwa watu wasioweza kujitetea..bora wakinivamia kutaka kuniua nitajitetea, ila jamani wale watoto kwa maelfu wanaofia hospital kwa kukosa dawa, kwa kukosa madaktari wa kuwatibu wanaweza kujitetea kweli??

Mie nadhani hawa jamaa wana kesi za kujibu...hawawezi kuchakachua hela yote ya nchi na kujilimbikizia wao wachache then tuwaache waondoke tuu na kutamba...
 
tuliwambia mtashinda hapa jf tu.
Picha mtaziona kila ofisi muhimu mtakazoingia.
Wote mtakuwa watumwa wake
pia ndo muajiri mkuu waserikali.
Mtajiju na sifa zenu hizo.
Na mtaumia sana tena kwa miaka 5 kama hammupendi.
Kwangu mimi nokicheko japokuwa naichukia ccm siku nyingi zilizopita.
Acha kwanza mkione cha moto.

nakuchukia hata wewe
 
Aisee poleni sana

Ila mimi nimefurahi kupita kiasi .......................... MAPINDUZII!!!!!!!!!!!!!!!!! DAIMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

teh teh.,....POLENI SANA MTAZOEA


Mwenye matatizo utamjua kati ya wote waliochangia ni wewe tu.

Utazoea wewe na familia yako sie tunamchukia kweli kweli.

Aibuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
why hate him?jifunze kuheshimu wengine,actually unaonekana uko frustrated tu na matatizo binafsi,umaskini pengine....fanya kazi achana na kikwete utakufa njaa.
 
Mi hadi anavunja baraza la mawaziri kipindi kile nilikuwa na imani nae. Baada ya hapo mh! Nilikuwa namtegea labda anaweza kuja na surprise yoyote ila nimegundua ni lile dude la kibisa. Kwa afanyayo sasa ni kama kuruhusu kuchezewa makalio na mafisadi
 
Mi simchukii as personal, Ila simuungi mkono anayoyafanya, No!!
I'm for Tanzania and anybody against Tanzania welfare is against me.
So JMK have set himself against me!
 
Hivi kikwete anasoma hizi thread? Au wasaidizi wake wanasoma lakini wanaishia kumsifu na kumficha ukweli kuhusu wanachosema wananchi
 
Toka kumalizika kwa zoezi la uchaguzi na kutangazwa matokeo ya Udiwani, Ubunge na Urais, namchukia sana Kikwete. Sipendi na wala sitaki hata kuona picha yake, wala kusikia habari zake mahali popote. Ninakacha kuangalia taarifa za habari kwenye Runinga, sisikilizi habari kwa njia ya Radio; na magazeti ndio sitaki kununua kabisa kwa kuchelea kukutana na habari zake.

Amenifanya niwe na wakati mgumu na hii yote ni kwa sababu ametumia madaraka yake vibaya kwa kushirikana na NEC na hao wengine, kuchakachua kura za watanzania.
Nahisi dunia inaenda mbele nyuma. Sijui wenzangu hali ikoje kwenu?
kikwete hana shida yakupendwa napaka kama wewe,mradi cc watanzania tulio na akili timamu tunampenda na tunamuhitaji,we hatutaki umpende,nakama hutaki kuona hatapicha yake hama nchi nenda kandahar ukaishi,maana kikwete ataendelea kuwepo ktk nchiyake ya tzania mpaka mwisho wamaishayake,mungu ampe afya njema na umri mrefu rais wetu mpendwa Aaaamen!
 
Toka kumalizika kwa zoezi la uchaguzi na kutangazwa matokeo ya Udiwani, Ubunge na Urais, namchukia sana Kikwete. Sipendi na wala sitaki hata kuona picha yake, wala kusikia habari zake mahali popote. Ninakacha kuangalia taarifa za habari kwenye Runinga, sisikilizi habari kwa njia ya Radio; na magazeti ndio sitaki kununua kabisa kwa kuchelea kukutana na habari zake.

Amenifanya niwe na wakati mgumu na hii yote ni kwa sababu ametumia madaraka yake vibaya kwa kushirikana na NEC na hao wengine, kuchakachua kura za watanzania.
Nahisi dunia inaenda mbele nyuma. Sijui wenzangu hali ikoje kwenu?


Wewe anakupenda nani.
 
Mie siku nyingi huwa simsikilizi hata kidogo kwani nothing good can come out of him. Uwezo wake up steaz ni mdogo saaana na source ya yote tunayolalamikia hapa. Hivi unafikiri kwa nini alichakachua hata mdahalo wake. He knowz nothing.
 
Back
Top Bottom