Namba za wakuu wa police wa mikoa katika magari yaendayo mikoani

Jun 17, 2011
20
5
Naona watanzania wamefurahi sana kuona hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na ajali barabarani, mimi pia ni mmoja wa watanzania lakini nina uwalakini na namba hizo.

Hofu yangu ni kuwa tuwije kuishia kuwa namba bila huduma,nikimanisha aidha ukapiga namba inaita lakini haipokelewi au inapokelewa lakini ikawa kwa ajili ya kuongeza kipato kwa asikari wa usalama barabarani ni kimanisha tatizo likasoviwa nyuma ya gari kati ya konda,dereva na trafic.

Suala la simu kutokupokelewa ninakuwa na mfano mzuri kabisa wa ajali iliyo ua mamia ya watanzania huko Zanzibar ya meli iliyotikea hivi karibuni,sikuwepo ndani ya meli lakini nikiwa nasikia shuhuda aliyekuwemo ndani ya meli hiyo, kutoka katika moja ya kituo cha Radio hapa nchini, anasema alipoona hali si shwari mapema kabisa kabla hata meli haijazama,alipopiga namba ya dharua lakini ilikuwa haipokelewi, na badae ikazimwa kabisa.sasa angalizo juu ya namba hizo pia.
 
Back
Top Bottom