Namba za simu zimeniponza

kabatimpya

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
231
250
Habarini wakuu.
Kama nilivyoelezea hapo juu.niende mwenye hoja.
Wiki iliyopita nilileta humu matatizo yangu ya kusumbuliwa na ugonjwa wa koo.
Nilielezea kwa undani tatizo lilivyo na vipimo nilivyoishafanyiwa.
Niliomba humu msaada wa ushauri au mwenye kuelewa hili tatizo dawa yake.
Nikaeleza kuwa hata nauli nimeishiwa.nilijiroga kuweka namba zangu za simu humu.
Nasema nilijiroga sababu niliambulia majibu mengine yenye dhihaka ndogo na kubwa.
Eti nipeleke beberu bikra na kuku mzee mwenye manyoya ya kijani.mwingine akaja kivingine kabisa.Tezi Dume na kuumwa koo wapi mpaka wapi? Tena nipimwe kwa njia ya asili mmhhh.
Tuwe tunajaribu kuwa na maono.mie sikuomba msaada na Yale mapovu mnayosemaga humu.hata hivyo kikubwa niliomba ushauri au aina za dawa zitakazonisaidia..
 
ipyax

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,728
2,000
Kacheki hospitali isijekua ni cancer ya koo mkuu, ikigunduliwa mapema basi na uwezekano wa kupona ni mkubwa zaidi.
 
kabatimpya

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
231
250
Kacheki hospitali isijekua ni cancer ya koo mkuu, ikigunduliwa mapema basi na uwezekano wa kupona ni mkubwa zaidi.
Nimeishapimwa Mara sita sasa ct scan.na ENT Mara mbili mbili Tasisi ya moyo na kipimo kingine kinaitwa OGD.Nimeambiwa nirudi tens 20/6 ili wakajidiane was ENT na OGD.Sijui nitaambiwaje tena.
 
hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
41,051
2,000
Dah! ! Hapa sitii neno aise. .Nisije kumtia was wasi mtoa mada
Kacheki hospitali isijekua ni cancer ya koo mkuu, ikigunduliwa mapema basi na uwezekano wa kupona ni mkubwa zaidi.
 
Johnny Impact

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
2,233
2,000
Habarini wakuu.
Kama nilivyoelezea hapo juu.niende mwenye hoja.
Wiki iliyopita nilileta humu matatizo yangu ya kusumbuliwa na ugonjwa wa koo.
Nilielezea kwa undani tatizo lilivyo na vipimo nilivyoishafanyiwa.
Niliomba humu msaada wa ushauri au mwenye kuelewa hili tatizo dawa yake.
Nikaeleza kuwa hata nauli nimeishiwa.nilijiroga kuweka namba zangu za simu humu.
Nasema nilijiroga sababu niliambulia majibu mengine yenye dhihaka ndogo na kubwa.
Eti nipeleke beberu bikra na kuku mzee mwenye manyoya ya kijani.mwingine akaja kivingine kabisa.Tezi Dume na kuumwa koo wapi mpaka wapi? Tena nipimwe kwa njia ya asili mmhhh.
Tuwe tunajaribu kuwa na maono.mie sikuomba msaada na Yale mapovu mnayosemaga humu.hata hivyo kikubwa niliomba ushauri au aina za dawa zitakazonisaidia..
Ulikuwa unazama chumvini nini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom