Sasa huyo Chama si amekuwepo kwenye mechi kama hizo nyingi tu za CAF hatua ya robo fainali na kushindwa kuwa hiyo x factor?
Ni kweli Simba inakosa ubunifu eneo la kati, pembeni na mwisho. Ukiacha Mpanzu, inakosa watu wa kuforce mpira uende mbele bila kuupoteza. Juzi kwenye goli la Mpanzu kule Misri, pamoja na kuona clip ya dkk 1, niliona hilo tatizo bado lipo.
Ningekuwa mimi, hata Kibu ningeachana naye nikatafuta mchezaji aina ya Mpanzu wa ku patna naye.
Janshalewa anatakiwa atumie muda mwingi mazoezini kufanya mazoezi ya faulo. Kama ulichunguza, kuna kipindi hadi Valentine Nouma akaanza kuingilia faulo zake azipige yeye maana aliona nyingi anapoteza na kibaya zaidi anakuwa hayupo hata on target halafu anapenda kufunga mwenyewe. Chama kwa sasa angekuwa na faida eneo hilo ila wakimrudisha watapata shida tena ya kuanza kutafuta replacement yake baada ya mwaka. Ni vizuri kuendelea kujaribu hawa wapya au kutafuta wengine hadi apatikane mtu sahihi.