Naliona jimbo la Moshi mjini likirudi CCM

Naliona jimbo la Moshi mjini likirudi CCM

Abunuas

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2011
Posts
8,812
Reaction score
1,824
Wadau kama mtakumbuka hivi majuzi kwenye kura za maoni CCM wamempitisha kijana tajiri David Mosha (ambaye anasemekana ndio wa kwanza na wa mwisho kununua gari ghali zaidi na la kifahari hapa Tanzania-lamborghini) na CHADEMA wamempitisha aliyekuwa meya wa Moshi Mjini na diwani wa Uswazi (Pasua, Matindigani co.) masikini mwenzangu Jafary Michael.

Davis Mosha ni mtu wa level ya akina Mzee Ndesa pesa ambaye kiuhalisia pesa zake zilikuwa zinambeba sana kwenye ubunge pamoja na kuwa alikuwa hawezi kufanya chochote kutokana na umri wake.

2010 wakati Ndesa-CHADEMA akishindana na Salakana-CCM alifikia hatua kwenye kampeni anawaambia wana-Moshi kuwa ''huyu Salakana alikuwa mfanyakazi wangu kwenye sheli. leo hii hiki kiburi cha kushindana na boss wake amekitoa wapi''!

Na kwa kweli wana Moshi bila ajizi walimpa kura mzee Ndesa, na kwa sababu hiyo basi, wana-Moshi sera yao ni kuwa kiongozi masikini atahubiri umasikini na tajiri atahubiri utajiri na pengine kuwaambuza huo ukwasi.

Naziona mwaka huu kura wana Moshi zikimuangukia kijana tajiri David Mosha kwenye ubunge.

Msije kusema sijawatonya.
 
We gari hujaliona eti inasemekana amenunua kama gari lake hulifaham bila shaka hata yeye humfaham na hata ulicho post hukifahamu ila endelea kulala uote ndoto nyingine
 
Mungu muepushe mwanangu asije kuwa na akili za mazuzu kama vijana wa ccm!!
Mosha magari ni yake pesa ni yake ubunge moshi ata mjomba wake hawezi mpigia kura ila pesa italiwa bila nidhamu ya uwoga !!
Mosha ni nanii pale moshi anajuwana na nani zaidi ya kuja mwezi wa 12 tu kama kunawatu ambao hawakuwaza ni david mosha kwenda kugombea moshi bora angeendelea kunywa zake bia dar es salaam kwenye bar za mikocheni moshi siyo chalinze !!
 
Watu wa moshi sio mabwege kama unavyodhani.. huo mtazamo wako. moshi ni jimbo litakalotawaliwa na wapenda mageuzi halisi na sio wa kuja. hakuna tofauti kati ya davis mosha na salakana. ila wote wameletwa tu wala sio wakazi wa moshi. CCM will never win Moshi and must go and rest in peace.
 
Moshi watu walianza kuchanganya za kuambiwa na zakwao siku nyingi sana mosha ni mchumba tu pale moshi!! Ubunge atausikia kwenye radio !!
 
Abunuas naona unaota zile ndoto zako,unaifananisha Moshi na sehemu zingine sio?Moshi ni Mji wa Wagumu muulize Thomas Ngawaiya na Mama Minde nini kiliwapata,Moshi hawachagui mtu anaekaa na kuishi Dar hata siku moja. Huyo Mosha hela zake zitaliwa na Ubunge hata upata kudadadeki zake.
 
jafary amejenga jina lake vizuri sana kwa kipindi chote akiwa meya so ngoja uone millioneA WAKO ATAKAVYOMWAGWA
 
Mosha ni bilionea. Je kawasaidia nin watu wa Moshi na huo ukwasi wake? Kajenga shule? Hospitali? Au yeye ni kununua magari tu kama Ronaldo na Mayweather?
 
Mungu muepushe mwanangu asije kuwa na akili za mazuzu kama vijana wa ccm!!
Mosha magari ni yake pesa ni yake ubunge moshi ata mjomba wake hawezi mpigia kura ila pesa italiwa bila nidhamu ya uwoga !!
Mosha ni nanii pale moshi anajuwana na nani zaidi ya kuja mwezi wa 12 tu kama kunawatu ambao hawakuwaza ni david mosha kwenda kugombea moshi bora angeendelea kunywa zake bia dar es salaam kwenye bar za mikocheni moshi siyo chalinze !!
mkuu hiyo kali tena. octoba usije ukakimbia humu. maana maneno miingi. subiria uone maamzi ya wanamoshi ndo hapo utakaposhangaa.
 
We gari hujaliona eti inasemekana amenunua kama gari lake hulifaham bila shaka hata yeye humfaham na hata ulicho post hukifahamu ila endelea kulala uote ndoto nyingine
mkuu kama huna cha kuchangia ni bora ungepita tu. nilichoandika humu nina uhakika wa 100%
 
Mosha ni bilionea. Je kawasaidia nin watu wa Moshi na huo ukwasi wake? Kajenga shule? Hospitali? Au yeye ni kununua magari tu kama Ronaldo na Mayweather?
mkuu akija huko ndo atafanya hayo yote.
 
Moshi watu walianza kuchanganya za kuambiwa na zakwao siku nyingi sana mosha ni mchumba tu pale moshi!! Ubunge atausikia kwenye radio !!
mkuu mbona umekuwa mkali hivi aisee. subiri muda ufike usije ukatoweka humu.
 
hiyo ni dalili mojawapo ya trakoma mkuu! wahi UKAWA ukapatiwe chanjo ya uhakika.
mkuu kama ukawa imekuwa chanjo kuweni makini. maana chanjo yenyewe itakuwa imefanyiwa majaribio kwenye panya. sidhani kama ni sahihi kuiruhusu kwenye matumizi ya binaadamu. unless kama mmeamua kuwa animal model.
 
Mosha hawezi kushinda moshi mjini wachaga hawana uswahili wa watu wa pwani pesa yake watakula kura kwa cdm
 
mkuu akija huko ndo atafanya hayo yote.
Kama anawathamini watu wa Moshi, hahitaji kuwa mbunge kuyafanya hayo. Kwani kipi kinamzuia kuyafanya kabla hajawa mbunge?

Sina ubaya na Mosha, ila nakosoa kasumba ya ngozi nyeusi kujenga nyumba ya ghorofa 3 ya kuishi wakati ana mke na watoto wawili tu. Vyumba vingine anaishi nani? Hii ni lugha ya picha, maana yake badala ya kujenga mahekalu ya kuishi tunaweza kujenga hospitali kubwa au shule tukaajiri watanzania wenzetu na tukapata pesa zaidi maana huo ni uwekezaji wakati jumba la kuishi ni liability. Badala ya kununua 'car toys' angejikita katika kubadilisha maisha ya watanzania na wana Moshi kwa kuwekeza KILA SENTI anayopata. Mambo ya Lamborgini angewaachia watukutu na wasio na majukumu kwa jamii zao kama kina Baloteli.

Chris Rock anasema Niggers spend money like the shit is gona rot-yaani weusi tunatumia hela kana kwamba usipozitumia zitaoza. Mfano mzuri ni Mayweather-100 cars, private jets,etc. Sasa mtu gari mia za kutembelea za nini? Kuna ngozi nyeusi inayokula hela ya babu yake (kwamba bado hajaanza kula za baba yake na zakwake anazozalisha) kama wahindi, wazungu? That is why black people can only get rich, but never wealthy!

So anaahidi kuifufua timu ya Ushirika stars (aka Washirika) akiupata ubunge. Mwambieni Kaka (mhindi) aliifadhili Tukuyu Stars (Banyambala) na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa Tanzania mwaka 1986 na hakuwa mbunge.
 
Back
Top Bottom